NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, October 28, 2010

HAKA KABINTI KA MIAKA MITATU KAMENISHANGAZA!!!

 • Mimi nimekaa kimya nikimwangalia Zofa akilisakata gozi. Mara kabinti kangu ka miaka mitatu kakanijia na kuniomba simu yangu ili kachezee. Huwa kanapenda kucheza michezo ya SpongeBob na kutazama video za Dora the Explorer na Go Diego Go!. 
 • Muda si muda mara nashtukia naambiwa "Dad, say cheers!" na kabla sijakaa sawa tayari nikajikuta nimeshapigwa picha. Nimeshangaa kwa sababu simu hii huwa inawashinda hata watu wazima jinsi ya kuitumia. Hiki kizazi cha dot.com we acha tu!

5 comments:

 1. Ni kweli mkuu, kizazi hiki kinaelewa haraka sana, lakini wasiwasi wangu hasa huku kwetu mitaani ni kuwa wanajifunza mambo yasiyowasaidia zaidi. Kwa mfano kuna hizi internet cafe, sasa hivi wanaweka ma-game(michezo ya computa), sasa utakuta watoto wetu badala ya kwenda shule, au hata akiwa shule anafikiria hayo magame. Ni mchezo mizuri kwasababu inachangamsha kichwa, lakini kuwe na ratiba maalumu!
  Hii sayansi na `teke-linalotujia', ni nzuri kwa kujifunza, kama vitendea kazi kama computa zingewekwa mashuleni, viazai vyetu vingejua haraka sana, lakini `ahadi za siasa' ndizo nyingi majukwani, kuwa mashule yatajaliwa computer. Na hata hizi shule za kulipia za kati na kati, nazo wanasema shuleni kuna computa, lakini ni mbili tatu. Sisemi hizo za `matawi ya juu' !
  Oh, nimejisahau mkuu nikajiona kama natunga kisa!

  ReplyDelete
 2. watoto ni viumbe wa ajabu ni watundu na wawezaji sana. mimi nawamini sana.Kwani napata misaada mingi sana kwa viumbe hawa.

  ReplyDelete
 3. Watoto!we acha tu,nadhani sasa watoto wana ufahamu mkubwa kuliko miaka kama 35 hivi ya nyuma ilivyokuwa,nakumbuka mimi nilivyokuwa mdogo labda kumbukumbu na u7janja wangu ulianzia kwenye umri wa miaka sita hivi,hata hivyo sidhani kama pamoja na ujanja wangu wote kwa umri huo wawaeza kufikisha hata asilimia 30 ya mambo afanyayo huyo binti wa miaka mitatu.Joseph John Mbelwa Kigamboni Dar-es-Salaam(josembelwa@yahoo.com

  ReplyDelete
 4. Taifa la kesho hilo mkuu!
  Hata kupiga kura labda washushiwe umri!:-)

  ReplyDelete
 5. Matondo, nadhani ile dhana ya Tabula Rasa ya John Locke ni sahihi kabisa.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU