NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, October 3, 2010

JAMANI, HATA KUJITANGAZA VIZURI TU HATUWEZI ???

 • Nilipokuwa nyumbani mwezi wa sita nilikutana na kijitabu hiki kilichochapishwa na Hotels Association of Tanzania pale Giraffe Ocean View Hotel. Kijitabu hiki kimelengwa hasa kuwahabarisha watalii (wa nje na ndani) juu ya huduma za malazi nchini Tanzania. 
 • Kijitabu hiki pia kina maelezo mafupi juu ya miji mbalimbali ya Tanzania na vivutio vyake vya kitalii. Nilishangaa kidogo kuona kwamba maelezo yaliyotolewa kwa baadhi ya miji pengine yanakatisha tamaa badala ya kuvutia na sina uhakika kama hili ndilo lengo hasa la waandaaji wa kijitabu hiki (Tazama mifano hapa chini)
Dodoma (Ukurasa wa 19)
 • "...There is really very little to be said about Dodoma, except to note that any plan which involves bussing there from everywhere except Dar es salaam should instantly be dismissed as a bad idea. Unless you'are on some sort of esoteric quest that involves 'collecting' capital cities, Dodoma is eminently missable."
 • Angalizo: Ni kweli kwamba hakuna cha maana Dodoma? Ni kweli Dodoma ni "eminently missable" isipokuwa kwa watu "wanaokusanya" miji mikuu? Vipi kuhusu kilimo cha Zabibu? Vipi kuhusu makao makuu ya serikali na bunge? Mbona watalii wasipewe maelezo ya vivutio vilivyopo halafu waamue wenyewe?
Tabora (Ukurasa wa 22)
 • "...Tabora may be the oldest settlement in Tanzania's interior, but it hasn't a great deal to see or do. Its atmosphere is friendly and laid back, and its tree-shaded avenues put a welcome dent in the very hot daytime temperatures of the region, but it's unlikely you will want to visit it unless you'are on your way to somewhere else."
Ujiji (Ukurasa wa 22)
 • "...You would have to be an intrepid traveller and fanatical history buff to travel here just to visit Ujiji."
***
 • Kuhusu bakshishi (tip) watalii wanaonywa: Not obligatory but a tip for good service, a maximum of 10% - will be appreciated. Tip $10-$15 per day for drivers or tour guides but remember an excessive tip can make it difficult fo the next customer.
***
 • Swali: Kama Wakenya wana ubavu hata wa kudai kwamba Mlima Kilimanjaro na hata Serengeti viko kwao ili kuvutia watalii (na wakafanikiwa), kwa nini sisi tunafanya hivi?

3 comments:

 1. Masangu kumbe ulikuwa hujui! Hawa lengo lao siyo kuitangaza Tanzania kama ulivyodhani. Pia si kwamba hawajui wanachofanya. Kilichowasukuma wahusika 'kutunga' hicho kijitabu ni kutengeneza pesa. Kuna miradi mingi Tanzania hasa serikalini ambayo imefanywa si kuisaidia Tanzania bali kuiibia. Tanzania unapotoa wazo lolote la kufanya wahusika lazima wajiulize cha mbele kabla ya maslahi ya taifa. Hivyo kaka usishangae hiyo ndiyo Bongo. JIKUMBUSHE pale wafanyakazi wa shirika la Reli walipojitolea kuokoa pesa ya umma kwa kufufua vichwa vya treni jinsi walivyoijiwa juu na Kawa-MBWA yule bingwa kupiga magoti kumuombea kura JK au jinsi mradi unaoendelea wa JK wa kuwapiga tafu wenzake unavyozidi kupata kasi hadi majeshi yetu vihiyo kutoa tishio utadhani watam-intimidate yeyote.
  Hiyo ndiyo Tanzania iliyokuwa yako unayopaswa kuililia ingawa ina wachapakazi kama mbunge wako Chenge au Endelea Chenga kwa lugha rahisi.

  ReplyDelete
 2. Watanzania bwana, sijui nani katuroga kwani it seems there is nothing we can do right. Sasa kujikandia hivi ndiyo nini?

  No doubt kati ya hawa walioandaa hiki kitabu ni vilaza tu na hakuna hata mmoja aliyesoma mambo ya advertisements. Ndiyo tatizo la kupeana vyeo kiholela. Unakuta mtu kasomea udaktari eti anapewa kuwa waziri wa ulinzi, wa kilimo kapewa mambo ya nje. Vurugu tupu. Tumerogwa sisi na pengine Shekhe Yahaya anaweza kutuzindua!

  ReplyDelete
 3. Shehe Yahya naye karogwa sema hajitambui kama Kikwete

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU