NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, October 24, 2010

HUYU KIBAKA KANIFURAHISHA KWA UBINADAMU ALIOUONYESHA

 • Juzi tarehe 22 Oktoba, katika mji wa York katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani kibaka mwenye bastola alimwamru jamaa mmoja aitwaye Larry Sanderson ampe kila kitu alichokuwa nacho. Larry akatoa waleti yake, simu ya mkononi, kichezeshi chake cha MP3 na sigara; na kumpa yule kibaka.
 • Kibaka yule (pengine baada ya kuona kuwa alikuwa amepata vitu kiduchu) alimwuliza Larry kama alikuwa amempa kila kitu alichokuwa nacho. Larry alimweleza yule kibaka kwamba ni kweli alikuwa ametoa kila kitu alichokuwa nacho kwani yeye hana makazi (a.k.a homeless).
 • Yule kibaka aliguswa na habari hizi na alimrudishia Larry vitu vyake vyote na kuondoka zake. Ubinadamu! Kisa hiki kinapatikana hapa.

7 comments:

 1. Wakati nimechoka binadamu huwa stori kama hizi huendelea kunipa moyo kuwa BINADAMU anaubinadamu bado na labda kunamatumaini bado hapa duniani na si lazima tusubirie Mbinguni.:-(

  ReplyDelete
 2. Kitururu umesema vyema. Ila, ujue. Angekuwa kibaka wa bongo angekunywa kila kitu na kumkata mambanta. Angekuwa kibaka wa Kenya bado angemtia ngeu kwa kutokuwa na zawadi za kutosha za wazee. Huoni mafisadi wetu matajiri wa kutupwa kama Kikwete, Chenge na Lowassa ambavyo bado wanafukuzia EPA na Richmond nyingine?

  ReplyDelete
 3. @NN Mhango - unaboa sasa. Everywhere you go ni name calling. This shit of your is becoming tiresome. Hata kama topic doesn't deserve name calling. May be you need to loosen up a little bit. You are bitter and I doubt if you are OK. Jeez!!!

  ReplyDelete
 4. Whoever anonymous is, do you think you can intimidate me? Kama nakuboa nitakuboa zaidi for my name calling. A bugger-cum-goon like you will nary cower me so to speak. Siogopi mbwakoko wanaotumiwa na mafisadi mbuzi tulio nao. Wewe unatumika kama nepi nami nasema ukweli. Wapi na wapi. Kama wewe kidume au jike kweli kwanini ufiche jina lako?

  ReplyDelete
 5. @NN Mhango:

  Sometimes unapo-argue na mwehu watu wanaweza wasijue who is who. For the seasoned, educated and rational people kama mimi it is better just to be quiet. Umeshinda kaka. Domo ni lako and you can shout as much as you want. Blessings!

  ReplyDelete
 6. Anonymous mwoga unayeficha jina lako ili usijulikane ujuha wako,

  My you perish. Usisingizie wala kujitia usomi usiokuwa nao. Kusoma si kupoteza muda darasani. Tunao maprofesa waliopoteza muda kwenye darasa kama wale wa REDET na wengine wengi kama mawaziri waliosaini mikataba ya kijambazi na wanasheria walioisimamia. Hawa na wewe kwangu si wasomi bali wasomi nepi. Njoo na hoja na utaje jina lako kama kweli unajua unachofanya. Tatizo la watu waliokeketwa akili ni kudhani wanaweza kumtisha mtu. Mie si mtu wa kutishwa na vineno viwili vitatu vya uongo au kujitia tia unajua.

  ReplyDelete
 7. Mtakatifu: Hata mimi kisa hiki kilinigusa sana ndiyo maana nikakiweka hapa. Binadamu ni mnyama lakini pia tunajua kwamba ni mnyama ambaye ana ubinadamu.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU