NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, October 10, 2010

KISWAHILI KINAZIDI KUCHANJA MBUGA MAREKANI - TANGAZO LA KAMPUNI YA SUBWAY (SEKUNDE 32 TU)

3 comments:

 1. Kaka kwa kweli lugha hii inakwenda mbali. na naamini kuwa inasonga na kuwa lugha ya wote. ile mantiki iliyopinda kwamba kiswahili hakifai itaondoka polepole.
  hakika tunasonga

  ReplyDelete
 2. Ila kama kawaida, waliotumika ni wale wanaoaminika kuwa WAASISI wa kiswahili. Jambo ambalo ni kinyume na ukweli.
  WAMEANZA NA MATANGAZO HAYA, WANASONGA NA KILIMANJARO NA KABLA HATUJASHITUKA, TUTAKUWA "WAFUASI" BADALA YA WAASISI

  ReplyDelete
 3. Markus - sisi hatuithamini sawasawa lugha hii vinginevyo tungekuwa tumeshaanza kuitumia katika ngazi za juu za mfumo wa elimu yetu. Badala yake tumebakia kuwa "vizabinazabina" tu huku tukiendesha mfumo wa lugha usioleweka - kwenye Kiswahili hatuko na kwenye Kiingereza hatuko. Matokeo yake watoto wa Wakulima na Wafanyakazi (ambao ndio wengi) ndiyo wanaathirika zaidi na mfumo huu wa lugha ya kufundishia. Tazama hapa:

  http://matondo.blogspot.com/2010/01/mauaji-ya-halaiki-ya-watoto-tanzania.html

  Muhula huu nafundisha darasa la Isimu Jamii (Language in African Society) na mojawapo ya mada ni sera ya lugha rasmi katika nchi mbalimbali duniani. Sera yetu (na pengine Waethiopia) inavyoonekana ndizo sera za ajabu kabisa hapa duniani.

  Mzee wa Changamoto: Sina la kuongezea isipokuwa tu kukuomba utembelee hapa:

  http://matondo.blogspot.com/2010/10/hata-kujitangaza-vizuri-hatuwezi.html

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU