NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 22, 2010

KUNA ANAYEJUA ALIKO DA KOERO BINTI MKUNDI?


 • Ni karibu mwezi mzima sasa Mwanablogu wa kike nambari wani Tanzania Koero Mkundi (a.k.a. Mama Mchungaji) hajaonekana kibarazani kwake. Kuna anayejua aliko? Au Bwana mdogo Fadhy na Mwanafalsafa wa Lundu wameamua kubeba kimoja na hatimaye kumpiga marufuku kublogu?
 • Litakuwa pigo kubwa kama Koero atatokomea moja kwa moja na kutoweka katika uwanja wa blogu Tanzania kwani  - bila kujali jinsia - ni mmojawapo wa wanablogu wachache (wa kike) niwapendao sana. Makala zake nyingi ni pevu, fikirishi na haogopi mtu; na kama anavyosema Da Mija - yeye ni mwanamke wa Shoka.
 • Koero, natumaini na kuamini kwamba uko salama; na ukibahatika kusoma ujumbe huu tujulishe uliko. Hata kama ni michango ya harusi baadhi yetu tuko tayari kutoa. Koero, rudi ulingoni - hata kama Fadhy au Mzee wa Lundu hawataki. Tunakutahiji! !!!

9 comments:

 1. Ameeeen!!!!  Hivi hiyo ilikuwa ni sala ama maombi? Vyovyote iwavyo arejeshwe. Nimemuandikia emails hajibu. Sijui kulikoni?
  Labda ndio yaleyale ya kurejea akisema "huyu mjomba wenu"
  Hahahahaaaaaa
  Rejea dada. Twakukumbuka. Lakini kwa sasa, popote ulipo na lolote JEMA ufanyalo..... UBARIKIWE

  ReplyDelete
 2. Matondo, unadhani kama tuhuma hizo unazotoa kwa Fadhy na Msee ye Lundu ni kweli hawastahili kutupa 'NGWEKWE'?


  Mie nilitaka kutangaza gazetini kabisa...lol!

  ReplyDelete
 3. Sasa naamini watu huwa tunawaza mawazo sawasawa nimeamka hapa nilitaka nami niuliza nani anajua waliko hawa wapendwa, mdogo wangu wa hiari Koero, mtanii wangu Fadhy na mngoni/mmanda mwenzangu Markus. Je huko mliko mpo salama maana sms, mail na hata kuwapigia simu hamjibu je mko salama? Tafadhalini au chondechonde jitokezeni tunawa-miss

  ReplyDelete
 4. Asanteni. Wito wangu umefanikiwa. Da Koero tayari ameshachoropoka huko aliko na ameshabandika tangazo kibarazani kwake kutujulisha kwamba hajambo - japo hajagusia kuhusu suala la Fadhy na Mwanafalsafa wa Lundu; na kama atarudi rasmi ulingoni hivi karibuni ama la. Kasema tu eti yuko bize "anajichomea kamuhogo kake na familia yake"

  We Ng'wanambiti nawe. NGWEKWE watauweza akina Fadhy na mwenzake kweli? We ulitandikwa NGWEKWE nini na wazee wa Maswa? Umenikumbusha juzi juzi tu hapa jamaa walikuja kuchukua Ngwekwe kwa jirani yetu na kwa vile hakukuwa na ng'ombe wala mbuzi basi wakaishia kuchukua kitanda, godoro, baisikeli na cho chote cha thamani walichokiona kinazubaa hapo nyumbani. Utamaduni.

  ReplyDelete
 5. Nafikiri mawazo ya marafiki wa kweli yanafanana, kwani unapoona mwenzako kajiandikisha kwako kama rafiki na haonekani mwezi mwaka, kuna haja ya kutafuta `kwanini'
  Labda kama wazo hakuna njia ya kupeana mawasiliano mbadala kama mtu hajaonekana muda akajuliwa hali. huwezi jua kuna kuumwa, kuna misiba kuna matatizo , na haya yote yanahitaji kusaidiana!
  Mimi naamini sisi wanablog ni ndugu na marafiki wa kweli ndio maana tumeamua kupeana ya moyoni kwetu, kwa kuandikkia kila linalokugusa. Sasa nafikiri tuguswe na kila linalotokea kwa wenzetu.
  Swali kubwa ni je utajuaje mwenzako ana tatizo na je kama analo utawasilianaje naye? Kwa marafiki wa kweli inawezekana, labda cha kusema ni `nani atamfunga paka kengele'
  Naona nitoe kisa kimoja, ...mmh, nitakitoa kwenye blog yangu karibuni, kuhusiana na hili!

  ReplyDelete
 6. MMN: Ngwekwe nilitoa kabisa, niliijua hata kabla sijabeba kwani kabla hujaingia ulingoni si lazima ufanye SWOT analysis?....lol!

  Kama kapatikana basi ni vema ila ngwekwe yetu lazima tupate hata ikiwezekana tuile, tuinywe na kufurahia...lol!

  ReplyDelete
 7. Mmmh!! ha ha ha ha ha ha naogopa sana vyeo. Kaka Matondo, hakika kuniita MWANAFALSAFA ni hatari kwangu, naogopa sana cheo haki ya mnyasa hivi sitanii.

  Jamani afadhali kaka Matondo amesema wazi kuliko ile mwanzo alidonoa kwamba mtani wangu Fadhy na Mimi limzee mcharuko la nyasa pale LUNDU tumemficha Mama Mchungaji. Duh!! huyu mwanamke wa shoka naye Koero yuko bize kama MBU we acha tu jamani siku hiziiiii

  ReplyDelete
 8. Profesa wacha matatizo ha ha hahah

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU