NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, October 18, 2010

MANJONJO YA WAHAYA (UCHESHI)

 • Baada ya kumaliza degree yake ya sheria mlimani Bwana Rwegoshora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya kuhudumia clients (wateja).
 • Siku ya kwanza wakati ndio amefungua ofisi yake,alimuona kijana mtanashati anakuja kuelekea ofisini kwake. Hapo ndipo alipoanza kunyanyua mkono wa simu ya TTCL, wakati anajizungusha kwenye viti virefu.
 • Wakati kijana “Mjaluo” alipokaribia Rwegoshora alionesha kumkaribisha wakati anaongea na simu, alisikika akiongea ''no, Absolutely no, You tell those clowns in New York that I won't settle this case for less than one million. (pause). Yes, yes. The Appeals Court has agreed to hear that case next week, I'll be handling the primary argument and the other members of my team will provide support. Okay. Pliz don't forget to tell the State Prosecutor that I'll meet with him next week to discuss the details." 
 • Yule kijana ametulia tu anamuangalia bwana Rwegoshora anajinyonganyonga kwa muda zaidi dakika 5.
 • Baada ya kumaliza kuongea na simu, bwana Rwegoshora alielekea kwa huyu jamaa. ''Samahani sana, kwa kukupotezea muda wako, unajua tena kazi zetu hizi zinaumiza kichwa sana, kama unavyoona tena mwenyewe hapa, yaani niko busy sana, ninapokea simu mpaka nimechoka mwenyewe. Enh by the way, what can i do for you?
 • Jamaa alijibu. ''Mimi ni Onyango, mfanyakazi wa TTCL. Nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani''

6 comments:

 1. Hahahahahahaaaa! Kwi kwikwikwikwiiiiii! Haha hahahahahaaaaaaa!! Mama mbavu zangu weeeee!!!
  Asante Mwalimu kwa kutuamsha na kicheko asubuhi hii! Nadhani siku itakua na baraka tele!!!!

  ReplyDelete
 2. Ndio kusema mbio za mwongo ni fupi!

  ReplyDelete
 3. Unatutafuta eeeeeeeeee?
  Hahahahaaaaaaaaaaaaaa

  ReplyDelete
 4. Mzee wa Changamoto, siwatafuti bwana. Pengine ni kweli kwani kwa manjonjo nyie mko mbali sana.

  ReplyDelete
 5. hapo sawa wala hututafuti ni kweli kwa kujifanya tunajua hata ambaye hajaingia darasani basi utakoma asante matondo

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU