NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, October 19, 2010

MNAWAKUMBUKA VIRANJA NA UNOKO WAO???

 • Nimeiona hii picha ikanikumbusha ukali (a.k.a unoko) wa viranja. Shule ya msingi kulikuwa na kiranja mkuu aliyekuwa mkali kuliko hata walimu wenyewe na adhabu zake zilikuwa balaa tupu. "Mheshimiwa" huyu darasani kidogo alikuwa hajiwezi na baadaye tuligundua kwamba alikuwa na chuki binafsi kwa wanafunzi waliokuwa na uwezo zaidi yake - kwa bahati mbaya nami nikiwa mmojawapo. Pengine hii ndiyo sababu alikuwa akiniandama sana kiasi kwamba ilikuwa nadra mno kwangu kupitisha siku bila kupewa adhabu kali na "mheshimiwa" huyu.
 • Baadaye nilikuja kugundua kwamba hii ndiyo asili yetu binadamu - hatupendani na kuoneana wivu, kutakiana na hata kutendeana mabaya ni jambo la kawaida tu. Na sasa hali imekuwa mbaya zaidi kiasi kwamba hata ndugu mliyetoka naye tumbo moja na kunyonya titi moja mambo ni yale yale. Pesa hatimaye zimefanikiwa kuvuruga ule moyo wa upendo na undugu tuliokuwa nao.
 • Pengine ni vizuri tukiwa wenye matumaini na kumakinikia zaidi mema ya binadamu badala ya upande wake wenye giza. Mimi binafsi nimegundua kwamba kukumbuka mambo mema ni bora zaidi kuliko mabaya na nimeweza kujiepusha na migogoro isiyokuwa ya lazima kwa njia hii ingawa kusema kweli "Homo Sapiens" pengine ndiye kiumbe tata kuliko wote; na pengine uwezo wake wa kufikiri pamoja na utashi wake vimegeuka kuwa lulu ya thamani lakini iliyofichwa katikati ya moto mkali wa bomu la Nyuklia!

  10 comments:

  1. Kweli hata mimi umenikumbusha mbali sana hali hiyo duh! viranja walikuwa wakali sana, na kweli ulikuwa si ukali wa kawaida ni visa tu. Kwani nakumbuka pia nilikuwa na wapinzani wengi na ambao hawakuwa viranja ila walikuwa na chuki sana, Na ilikuwa ni kama mashindano.Ila hali hiyo ya viranja hadi kukamata viboko imekuwa mbaya sana mwaka jana nilipokuwa nyumbani binti yangu alisoma hiyo miezi tuliokuwa nyumbani na alisimulia na pia niliona mengi sana. Hali imekuwa mbaya mno. Ahsante kwa kumbukumbu.

   ReplyDelete
  2. Wakati huo hata viongozi walikuwa wakali katika kuhimiza uadilifu na maadili. Leo wanafunzi wengi wanaongoza kwa uvutaji bangi, udokozi na umalaya. Walimu ndiyo usiseme japo si wote. Hivi karibuni nchini Kenya walimu zaidi ya 500 walifutwa kazi kwa kuwatundika mimba wanafunzi. Kama unoko umetuvusha hapa tulipo, ni heri kuliko uholela unaotupeleka motoni. Mwalimu mkuu JK Nyerere aliwahi kumramba bakora waziri wa sheria Abdallah Fundikira. Unategemea viranja wangefanya nini katika hali hii?

   ReplyDelete
  3. niliwachukia viranja na wengine niliwatwanga baada ya shule

   ReplyDelete
  4. Kamala una hatari. Hata husamehi ndugu yangu! Mie niliwapenda maana walisaidia kuondoa utukutu usiokuwa na sababu.Laiti wangekuwapo leo wakawachapa hawa mafisadi wetu ningefarijika.

   ReplyDelete
  5. Viranja wengine walikuwa dangerous. Kulikuwa na mdada mkuu pale Nganza Mwanza alikuwa anatuchukia sisi watoto tuliotoka familia za kifisadi na tuliomzidi uzuri. Tuliamua kumkomoa kwa kuhakikisha kwamba kila boyfriend anayempata tunamchukua. Mbona mwenyewe alibroo na kutuomba msamaha. Unoko hautakiwi maishani and if your family is not rich, wewe learn ufisadi ili mtajirike and the solution is not to hate on the ones who are blessed!

   ReplyDelete
  6. Mafisadi wana uzao uliolaaniwa. Yaani hamkuogopa hata ngoma! Wewe dada uliyeandika hapa unauza uchi wako bei gani na je umepima?

   ReplyDelete
  7. Ngoma haichagui mafisadi wala nini. Mbona tupo tu na some of the girls masikini kutoka vijijini walishaondoka na ngoma? Wao walikuwa wanapapatika wapate mwanaume wa kuwanunulia redio, pasi na TV wakati vitu hivi kwa sisi watoto tuliotoka kwenye familia zenye neema (aka blessed) si mali kitu.

   Ufisadi unalipa and I will never blame my father for stealing mali ya bure ya umma. It doesn't make sense eti mtu upewe shirika halafu uondoke masikini. I will always be proud of my father. Nyinyi masikini mtapiga makelele ufisadi, ufisadi, who cares? Eti mafisadi wana uzao uliolaaniwa, who told you that? We are rich, happy and satisfied. Nyie wachovu kaeni tu mpige makelele yenu, sie twatanua.

   ReplyDelete
  8. Dada changudoa fisadi,
   Nyinyi hamtanui bali mnatanuka. Kuna siku mtalipia dhambi yenu hiyo ya uroho niamini. Wako wapi kina Mobutu na Bokassa? Unayoongea hayatoki moyoni na unajua unavyojidanganya ukidhani utawadanganya na wengine. Umekuwa mtumwa wa vitu kiasi cha kuvigeuza miungu yako maskini nyani wa kike.

   ReplyDelete
  9. Naona wachovu masikini mmeshaanza matusi.

   Just remember that "dua la kuku halimpati mwewe". You will keep on shouting while we are literary EATING the country. Ufisadi, ufisadi my foot. Wewe na umasikini huo tukikupa uwaziri kweli utaacha kuiba ili kuinua your family? Usipoiba basi utakuwa very stupid!!!

   Kalagabaho!. Keep on shouting wakati nchi TUNAILA.....

   ReplyDelete
  10. Thanks anonymous aka Ridhiwan Kikwete

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU