NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, October 9, 2010

.....NATAKA KUWA BONGO FLEVA....

  • Wanaoshabikia hii staili ya "Bongo Fleva" kama Kiraka hapo juu sijui wanajua kwamba ilianzia magerezani kule Marekani ambako mikanda hairuhusiwi; na kwamba ilikuwa njia mojawapo ya kuonyesha tabia ya kishoga kwa wafungwa?
  • Baadaye mtindo huu uliigwa na wanamuziki wa kufokafoka, na baadaye ukaingia mitaani hasa kwa Wamarekani weusi. Wanaharakati wengi wanaopigania maslahi ya Wamarekani Weusi wameupinga mtindo huu kwa muda mrefu wakidai kwamba unawadhalilisha vijana weusi. Bill Cosby, kwa mfano, amewahi kuwalaumu wazazi wanaowaruhusu watoto wao kuvaa mitepesho, akiihusisha tabia hii na malezi mabovu yanayotolewa na Wamarekani Weusi kwa watoto wao. 
  • Katika baadhi ya miji hapa Marekani kama  kule Dublin, Georgia, kuvaa mitepesho sasa ni kosa linaloweza kusababisha mvaaji kupigwa faini ya dola 200. Na sisi masikini, kama kawaida yetu, tunajiigia tu hata bila kujua undani hasa wa kile tunachokiiga.

2 comments:

  1. Hapa tatizo ni ushamba ulimbukeni na ujuha. Vijana wetu wanadanganyika na maisha ya Hollywood wakidhani Marekani yote ni Hollywood wasijue kuna watu wanasota. Kwao kujiharibu kwa kutoga masikio midomo na kila sehemu za mwili au kutembea uchi au nusu uchi ni kuwa mmarekani hasa wale ma-superstars. They are but goons and lost brethren of ours.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU