NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 1, 2010

NJIA RAHISI YA KUPUNGUZA UFISADI HII HAPA.

Picha hii inapatikana hapa
 • Ufisadi - tatizo sugu na hatari linalodidimiza maendeleo ya Afrika kumbe linaweza kupunguzwa kwa kutumia njia rahisi tu. Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia unaonyesha kwamba serikali zenye wanawake wengi madarakani (mf. Wabunge, Mawaziri) zina viwango vidogo vya ufisadi ukilinganisha na zile zilizosheheni wanaume. Rwanda - nchi ambayo inaongoza duniani kwa kuwa na wanawake wengi bungeni na serikalini inatajwa sana kuwa mfano wa kuvutia kuhusu suala hili. Ni kwa sababu hii kujitokeza kwa wanawake wengi kugombea ubunge na uwakilishi kule Haiti katika uchaguzi wa mwaka huu kumeleta matumaini makubwa kwamba pengine ufisadi utapungua.
 • Tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba wanawake wana huruma kuliko wanaume, wana moyo wa kujinyima, wanaaminika zaidi na ni wepesi wa kuona na kukiri makosa na hatimaye kuomba msamaha. Pengine ni kutokana na sababu hizi wanawake pia wana uwezekano mdogo wa kuiba mamilioni ya pesa za umma na kuwaacha wananchi wanyonge wakiteseka (wengi wao wanawake wenzao; na watoto). 
 • Serikali zenye wanawake wengi madarakani pia zina uwezekano mkubwa zaidi wa kuendeleza sera imara zenye kumakinikia sekta za afya na elimu ya watoto, usawa kwa wanajamii wote na kuendeleza uchumi imara.
 • Pengine nasi inabidi tuige mfano wa Rwanda ili tuone kama visa vya ufisadi vitapungua. Utafiti huu wa Benki ya Dunia unapatikana hapa.

6 comments:

 1. Kumkemea joka aliyekubana namna hiyo, haitoshi. Yahitajika mapambano ya nguvu au kivitendo na wala sio maneno pekee, hapo ndipo ufisadi tutautokomeza

  ReplyDelete
 2. Chib: Au unataka huyu mkemeaji atangulize "Kwa Jina la Bwana" katika ukemeaji wake? LOL!

  Ni kweli. Tatizo letu maneno mengi, vitendo sufuri.

  ReplyDelete
 3. Aisee nilikuwa sijalifikiria hili. Inawezekana ni kweli kwani hata katika majina yanayovuma kwa ufisadi nchini hakuna mwanamke hata mmoja. Now I know that it is not a coincidence.

  ReplyDelete
 4. ...ni kweli lakini si kwa wanawake wenye hulka na tabia kama Sophia Simba anayedai kuwa wanawake wa CCM wawanyime unyumba waume wao watakapowapigia upinzani....

  hakiyanani, nke wangu akifanya hivo namrudisha kwao akalime pamba....lol!

  kigezo cha kuwa mwanamke tu hakitoshi... uchambuzi yakinifu unatakiwa ili kupata wanawake makini wasioweza kushawishiwa hata na waume wao ili wakwibe mali ya umma. Motion seconded....lol!

  ReplyDelete
 5. Mpiganaji Chacha na anony wa October 1, 2010 3:13 PM. Hongereni sana kwa maoni yenu ya kina yanayo kidhi haja. Huyo ndugu yetu aliyetekwa fikra za kiitikadi ya vyama, mimi nampa pole nyingi.

  Wakati watu tunafikiria namna ya kuikomba nchi amabayo toka utumwani wa mafisadi yeye bado yupo kwenye usingizi wa kuongelea habari za vyama vya siasa.

  Hivi ni aibu iliyoje kwa raisi kuwanadi hadharani watuhumiwa ambao waliachia ngazi nyadhifa zao serikali kwa tuhuma za ubadhirifu. Leo hii yeye anathubutu kusema ni wachapa kazi.

  Ama kweli sikio la kufa halina dawa.

  ReplyDelete
 6. Lazima na wanawake mafisadi watakuwepo lakini si kwa kiwango cha kutisha kama cha wanaume. Wanaume mko very agressive halafu hamna aibu. Kama Chenge, Mramba na Lowassa wangekuwa wanawake sidhani kama wangegombea tena.

  We need more women. Nakubaliana 100% na huu utafiti wa World Bank!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU