NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, October 14, 2010

SWALI: NENO KITIMOTO LINATOKANA NA NINI?

 • Mwanafunzi wangu Mmarekani alikuwa Dar es salaam, Mbeya na Bukoba na leo kaniuliza kama ninafahamu neno kitimoto linatokana na nini. Kusema kweli sifahamu na sikutoa jibu la maana.
 • Kuna anayejua neno hili lilianzaje? Kuna uhusiano gani kati ya kiti na moto; na nyama ya nguruwe? Natanguliza shukrani zangu.

7 comments:

 1. Tafsiri niliyonayo mimi ni kuwa, nchini Tanzania kilikuwepo kipindi kinarushwa kwenye kituo kimoja cha runinga kilichopewa jina la "Kiti Moto" ambapo watu maarufu na hasa wenye nyadhifa za uongozi nchini Tanzania, walikuwa wakialikwa kisha wananchi waalioweza kufika studioni wakapewa fursa ya kumwuliza maswali mheshimiwa huyo bila ya yeye kufahamu swali atakaloulizwa, kisha alipaswa alitolee majibu au ufafanuzi. Kilikuwa kikiendeshwa na mtangazaji Adam Lusekelo au Julius Nyaisangah nk.

  Baada ya historia hiyo ndefukidogo, sasa niweke -connection- yake na nyama ya nguruwe.

  Kutokana na jina la "kiti moto" kuwa maarufu, basi jina hilo likahamia mitaani katika migahawa viosk kuwa kwa wale ambao kula nyama ya nguruwe ni haram, (Waislam, Wasabato nk) basi yeyote ambaye alizidiwa na tamaa na kujikuta akiila kwa siri na kwa kujificha ficha, alikuwa akifanya hivyo kama vile "ameketi kwenye kiti moto" kwani anaweza kuonwa na yeyote anayemfahamu kisha akapigwa maswali ya chap chap (kama ya "kiti moto") kuelezea sababu hasa ya kufanya kufuru na kula nyama hiyo.

  Hivi ndivyo nijuavyo mimi asili ya neno "kiti moto" na uhusiano wake na " nyama ya nguruwe". Wengine wataelezea wanavyofahamu wao.

  ReplyDelete
 2. Nami nilivyosikia ni kama Da SUBI alivyoelezea.

  Na kwenye kiti moto kwa kawaida kunakuwa na majadiliano motomoto lakini.:-)
  DUH nimeimisi hii kitu na nyama choma:-(

  ReplyDelete
 3. haswaa subi ndivyo hivyo. nadhani pia na paschal mayala alikiendesha.

  ReplyDelete
 4. Da Subi: Jibu mwafaka kabisa. Yaani sikuwa hata na fununu. Asante sana.

  Mtakatifu: huko Uswidi hakuna kiti moto? Au tatizo ni kukosekana kwa majadiliano motomoto?

  Mwaipopo: kipindi hiki naona mimi kilinipita kabisa. Nyote asanteni.

  ReplyDelete
 5. Hata mimi nilikuwa sijui. Asanteni. Blogu kweli ni shule. Me love yo blog a lot. Keep up da gud job!!!

  ReplyDelete
 6. Kwa kuongezea ni kwamba, hii nyama ni tamu sana kuliko nyama zote,kwahiyo iliitwa kiti moto kwakulinganishwa na kile kipindi cha kiti moto maana watu wengi walikuwa wakivutwa sana na kusisimka mara tu kipindi kile kilipoanza na pia waliamua kutumia jina hilo ili kuficha makali unapolitamka kwa wale wasiotumia.

  ReplyDelete
 7. Asanteni wadau maanony. kwa nyongeza zenu. Msichoke kutoa michango yenu...

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU