NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, October 16, 2010

TUTALITATUA LINI TATIZO LA LUGHA YA KUFUNDISHIA MASHULENI ? (SEKUNDE 54 TU)

 • Asanteni Haki Elimu kwa juhudi zenu. Pengine siku moja watunga sera wataamua kulishughulikia swala hili ambalo kwa maoni yangu ni suala la muhimu mno kwani linaugusa moja kwa moja mkakati wetu mama wa ukombozi na maendeleo - elimu bora!

3 comments:

 1. Niliwahi kuandika makala kwenye gazeti la mwananchi kuhusu athari zitokanazo namfumo wetu wa elimu uliojikita katika lugha ya kiswahili katika utoaji wa elimu ya awali na msingi.

  Mkanganyiko unakuja pale mwanafunzi anapojiunga na elimu ya sekondari, ambapo lugha ya kufundishia sasa ni kiingereza kwa masomo yote isipokuwa somo la Kiswahili. Hili huathiri kwa kiwango kikubwa uwezo wa wahitimu wetu kilugha.

  Hapa kinachotakiwa lugha moja itumike kuanzia mwanzo hadi mwisho, kama ni kiingereza basi iwe ni kiingereza kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu na kama ni kiswahili basi iwe ni kiswahili kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu. Vinginevyo tutabakia kuwa vilema wa mfumo mbovu wa elimu yetu.

  ReplyDelete
 2. Bwana Matiya - mengi yameshasemwa kuhusu suala hili. Tafiti za kila aina zimeshafanywa na mapendekezo mazuri sana yameshatolewa. Lakini inavyoonekana kuna kutojali kwa upande wa watunga sera. Na wanaoathirika zaidi na sera hii kanganyifu ya lugha ni watoto wa masikini na hasa wale wa kijijini ambao hawana uwezo wa kuhudhuria "academy" na shule za "English Medium" zilizoenea mijini. Mtu waweza kushawishika kuamini kwamba sera hii ya lugha sasa inatumiwa kama njia mojawapo ya kuendelea kuwadidimiza watu wa tabaka la chini na kuhakikisha kwamba wanabakia huko huko chini. Sera hii ni lazima ibadilishwe!

  ReplyDelete
 3. Mabwana Matiya na Nzulilima mnawaonea watunga sera wetu. Nani atamvisha paka kengele iwapo watunga sheria yaani wabunge ndiyo mabingwa wa kiswanglish? Mambo yamezidi kuongezeka. Wabunge na mawaziri, kwa sasa, wanaongoza kwa kughushi vyeti vya kitaaluma na hakuna anayewagusa! Kuondokana na hili ni kuwa na serikali ya watu wenye ubongo wenye rutuba na si mafisadi wenye kutumia matumbo yenye rutuba kuiba. Hawa wana vichwa vilivyodumaa ambavyo hawavitumii zaidi ya matumbo yao. Nimehisi aibu pale Kalonzo Musyoka yule kibaraka wa Moi aliposema eti Tanzania ichukue walimu kutoka Kenya. Alinogewa na kusema kuwa watanzania wamchague Kikwete kwa vile anahitajiwa na Afrika Mashariki ili atuchuuze vizuri kwa wakenya na wengine huku akichekacheka. Tuanze kufundisha kiingereza vilivyo vinginevyo vijana wetu wataisikia jumuia ya Afrika Mashariki magazetini. Hawatanufaika nayo. Hata Burundi na Rwanda walioanza kutumia kiingereza jana wanaanza kutupita! Hayo ndiyo mafanikio ya kujivunia ya CCM.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU