NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, October 31, 2010

UJUMBE KUTOKA KWA MABINTI: "UCHAGUZI MWEMA WATANZANIA WENZETU !"

 • Naona tumefanikiwa kuwaaminisha mabinti hawa kwamba, japo walizaliwa hapa, kimsingi wao bado ni Watanzania na ni muhimu wautambue utamaduni wa Kitanzania (ikiwemo lugha ya Kiswahili). Matunda ya juhudi hizi tumeanza kuyaona kwani sasa wanajivunia kuwa na wazazi wanaotoka Tanzania, wanajibidisha sana kujifunza Kiswahili na hawauonei aibu utamaduni uliowakuza na kuwalea wazazi wao!
 • Malaika hawa wa Mungu basi wanawatakia Watanzania wote uchaguzi mwema na wa amani leo hii. Nasi tunaungana nao na kuendelea kumwomba Mungu Aendelee kuibariki nchi yetu na kuipa "Mnyanyua Mikono" mwenye upeo mkubwa na mwenye uchungu wa dhati na nchi yetu. Kila la heri Watanzania wenzetu. Mungu Awabariki sana!!!

8 comments:

 1. Naamini Mungu yupo pamoja na atawaongoza wananchi wake kuchagua kiongozi mwenye kufungua macho .Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

  ReplyDelete
 2. Naamini tulichagua wema wa kuilinda mali asili ya nchi hii ili kizazi hicho na kinachokuja kije kiikute..Amina , twaomba dua ikibalike

  ReplyDelete
 3. Profesa umebarikiwa sana. watoto wazuri na hekima tayari.

  ReplyDelete
 4. Hongera kwa kutowaruhusu vijana wetu kuwa walowezi huku kimila. Kwa wazazi tulio na watoto waliozaliwa huku, inahitaji moyo na muda kuhakikisha wanaijua lugha yao na kujijua vile vile kutokana na imani potofu ya huku kuhusiana na Afrika. Hata hivyo tuwalaumu watawala wetu wachafu wanaoruhusu watu kuitumia Afrika kutengeneza pesa huku majuu.

  ReplyDelete
 5. Wapendwa;

  Asanteni nyote. Kulea watoto huku nje ni mtihani kweli kweli. Tunajaribu kuwafanya wawe na utamaduni wao wenyewe ambao wanaweza kujivunia na kujipambanua nao. Hatutaki wahangaike kama hawa Wamarekani Weusi ambao hawana utamaduni na hawajijui wao ni nani - huku hawako na kule hawako ali mradi vurugu tu mtindo mmoja. Kama asemavyo Ngugi wa Thiong'o, usipokuwa na utamaduni wako mwenyewe hapa duniani basi wewe si lolote si cho chote.

  @emu-three: Kweli mmechagua na matokeo yake tumeyaona. Mungu Aendelee kuibariki nchi yetu tukufu!

  ReplyDelete
 6. @mumyhery: Naona Mwanza mmefanya kweli. Dah!!!

  @anony: Asante! Kama nilivyosema hapo juu, malezi ya watoto hapa ni changamoto kweli kweli. Tunajaribu na tunamshukuru Mungu kwa kutupa jukumu hili tukufu.

  @Mwalimu Mhango: Ndiyo ni kazi sana. CNN na FOX News zimeshawafunza hawa malaika kwamba Afrika ni mahali pa shida. Mwanzoni walikuwa wanaogopa kusema kwamba wazazi wao wanatoka Afrika mpaka tulipowaelezea na kuwafundisha uzuri wa Afrika na Tanzania. Basi sasa wanamwambia kila rafiki waliye naye kwamba wazazi wao wanatoka kule kule kwenye Mlima Kilimanjaro, Serengeti, madini ya Tanzanite na kunakozungumzwa ile lugha tamu ya "Hakuna Matata", jambo n.k. Tukazane nao hivyo hivyo tu.

  @Da Mija na Yasinta. Asanteni. Naona dua za mabinti zimesikiwa na uchaguzi umepita kwa amani (mbali na ulubuti wa hapa na pale). Mungu Aendelee kuibariki Tanzania!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU