NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, October 11, 2010

UTAFITI: ETI WATOTO WANENE HUKUA NA KUWA "VIWEMBE"

 • Hii mada ya leo nitajaribu kuifupisha. Ni hivi: Utafiti mpya uliofanywa na wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Northwestern nchini Marekani unaonyesha kwamba watoto wa kiume wanaopata lishe bora na kunenepeana hasa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo hutoa kiasi kikubwa cha homoni muhimu ya testosterone.
 • Kutokana na sababu hii watoto hawa hukua haraka, hubalehe mapema, huanza ngono kabla ya wenzao na wana uwezekano mkubwa wa kuwa na wapenzi wengi maishani mwao (a.k.a kuwa viwembe!).
 • Utafiti huu unapatikana hapa kwa kifupi. Wazazi mpo? Lishe bora ni muhimu ati!

5 comments:

 1. duhu kazi ipo ila sijui kama ni kweli maana mimi nimeanza late. ila sasa mtoto mweneye lishe bora ana akili huwa bora na kumbuka kutongoza sio lelemama

  kakwangu kananyonya madhiwa ya mama vegetarian, yamekamilika na kana afya kweli kweli kwa hiyo duhu nitakaleta kaishi jirani na mabinti zako!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 2. Interesting! Sasa check new fathers out there who are going to find out about this...I am just saying...

  ReplyDelete
 3. Duh! dada Andy nawe kwa mistari, ha ha ha umewaza nini?? kwa kweli niseme tu kwamba siku hizi mazingira yanabadilisha sana kanuni ya maumbile, sina hakika ni kwasababu hiyo au vipi. lakini kwa utafituo uwezekano upo kwakuwa binadamu jamani tuna yetu atiiii. sasa sijui itakuwaje hapo katoto ka kaka kamala kakiwa a.k.a kidume cha njiwa kikianza kupepea kama tiara.

  ReplyDelete
 4. We Kamala wewe - shauri yako. Katawaweza mabinti wa Kimarekani?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU