NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, October 5, 2010

UTAFITI: WANAUME HUVUTIWA ZAIDI NA SURA WANAPOTAFUTA MKE LAKINI HUVUTIWA NA UMBO WANAPOTAFUTA MWANAMKE WA "KUCHEZEA"

  • Mabinti: Siri imeshafichuka na inavyoonekana wanasayansi tayari wameshafumbua lile fumbo tata la nani mwoaji na nani mbabaishaji tu mtaka uroda.
  • Siku nyingine mpenziyo mpya akikuambia kwamba sababu yake kuu ya kukupenda ni miguu yako, macho, kiuno, matiti, umbo namba nane au sababu zingine za kiumbo, kuna uwezekano mkubwa kwamba huyo njemba si mwoaji bali ni mtafuta uroda tu.
  • Utafiti mpya uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Texas, Austin unaonyesha kwamba wanaume hutumia vigezo tofauti wanapotafuta mwenzi.
  • Kama lengo ni kutafuta mwenzi wa kudumu (mf. mke) basi wanaume wengi hupendelea wanawake wenye sura nzuri lakini kama lengo ni uhusiano wa muda mfupi tu (mf. kutimiza tamaa za ngono za muda mfupi) basi wanaume wengi hutafuta wanawake wenye maumbo mazuri wayatamaniyo.
  • Watafiti hawa wamegundua kwamba, japo umbo ni muhimu kidogo katika mahusiano ya muda mrefu, uso ni muhimu zaidi kwa sababu ndicho kiashiria kizuri cha umri na “rutuba” ya mwanamke.
  • Swali: Kuna ukweli wo wote katika utafiti huu? Kinachonishangaza mimi ni kwamba suala la tabia  ya mwanamke - na hata Noeclexis- halitajwi kabisa katika utafiti huu, jambo ambalo nafikiri lilikuwa (na pengine bado) ni la muhimu katika jamii nyingi za Kiafrika. 

1 comment:

  1. me naona ni kweli kwasababu mwanaume hapend kuwa na mwanmke ambae kila mtu anatamani kupitia, ila sura mara chache sana mwanaume kuwa na mwanamke mzuri wa sura kwa starehe zake bianafsi

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU