NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, October 5, 2010

WAKATI UMEFIKA WA KUZITUMIA LUGHA ZETU ZA MAMA KUTATULIA MATATIZO YETU YA KIJAMII

 • Nimeliona hili tangazo kutoka Shinyanga vijijini katika blogu ya "jamii" nikalipenda. Baada ya kuzipuuza lugha zetu za kiasili kwa muda mrefu, pengine wakati sasa umefika wa kuweza kuzitumia katika sekta rasmi hasa katika masuala nyeti ya kijamii kama hili la UKIMWI.
 • Anayetaka tafsiri aseme; au Da Mija anaweza kusaidia.

5 comments:

 1. Kaka umenusurika na hizo risasi? Maana naona ni kama shuleni kwako.
  Tupe full story.

  ReplyDelete
 2. Mwalimu Mhango, risasi zipi tena? Unaongea kitaswira. Sijakupata - fafanua.

  ReplyDelete
 3. Nilisoma sehemu kuwa kuna jamaa amevamia chuo hapo mjini kwako na kufyatua risasa na kuua mmoja na kujeruhi kadhaa kabla ya kujimalizia mbali. Kutokana na kihoro na mshawasha wa kutaka kujua kiniojiri huenda ni habari ya zamani. Kwa vile umejibu ni ushahidi kuwa u mzima. Vipi umeonaje jinsi Dk SILAHA alivyomlipua Lt Gen Shimbo na maulaji yao ya nyuma ya pazia? Kazi kweli kweli.
  Kila la heri

  ReplyDelete
 4. Mwalimu;

  Maisha ya hapa si unajua tena. Jamaa kacharuka tu kamtandika risasi babake, kaingia kwenye gari na kujitoma mtaani na kisha akaanza kutafuta wabaya wake na kuwatwanga risasi pia. Kuna watu waliokutana naye lakini akawaacha na inavyoonekana kuna watu aliokuwa anawatafuta. Polisi walipomzukia naye akajimaliza.

  Bunduki hapa ziko nyingi mno na hata sasa naweza kupita Wall Mart nikanunua nyama ya mkia wa ng'ombe na bastola au bunduki yo yote niitakayo. Ukizingatia na ukweli kwamba tofauti za kitabaka ni kubwa mno na maisha ni magumu kwelikweli hasa kwa watu masikini basi mtu anajikuta hana njia nyingine. Ni mambo ya kusikitisha sana.

  Tembelea hapa: http://www.cbsnews.com/8301-504083_162-20018541-504083.html

  ReplyDelete
 5. Shukrani. Nakutakia maajabu mengi ya kushuhudia uchawi na ushirikina wa Halloween. Upo hapo? Kama si uchawi ni nini hata kama unafanywa na watasha? Tafakari. Uzuri huku si kama KWETU wanakoonea vikongwe. Wao wanamalizana kwa shaba sisi mapanga ila kifo ni kifo na kuua ni kuua na uchawi ni uchawi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU