NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, November 24, 2010

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI: MASWALI MAWILI YA KIZUSHI + ANGALIZO

Mh. J.K. akitangaza Baraza la Mawaziri leo

Swali la Kwanza

Vijana wako wapi? Akina Ndungulile, Kigwangalla, Nkamia, January na wengineo?  Mbiu ilikuwa ikipigwa kwamba baraza hili litakuwa la aina yake kwa kuhusisha sura mpya nyingi na hasa vijana. Kumetokea nini?

Swali la Pili

CCM wana mtindo wa kuandaa wenyeviti na maraisi wao mapema. Kwa kuangalia hili baraza la sasa, ni nani ambaye anaweza kujivika u-Shekhe Yahaya hapa akatutabiria ni yupi anayendaliwa kubeba mikoba ya CCM hapo 2015 baada ya Mh. J.K. kumaliza ngwe yake?

Angalizo

Baada ya kutembelea blogu mbalimbali na vyanzo vingine vya habari, watu wengi wanaonekana kufurahishwa sana na uteuzi wa Mh. John Pombe Maghufuli kurudi tena katika Wizara ya Ujenzi. Inasemekana kwamba Mheshimiwa huyu pengine ndiye waziri mchapakazi kuliko wote. 

Uteuzi mwingine unaoonekana kuwakuna watu ni ule wa Mh. Dr. Harrison Mwakyembe, Mh. Profesa Anna Tibaijuka na Mh. Samweli Sitta. Nadhani sababu za waheshimiwa hawa kufagiliwa zinajulikana. Na wengine waliokuwa wakipigiwa tetesi sana kama huyu naona wametupwa nje. Mungu Aibariki nchi yetu!

8 comments:

 1. hata mimi kurjea kwa mzee wa takwimu a.k.a Magufuli ni habari njema sana, bara bara zitamalizika zote!

  ReplyDelete
 2. Rais anayeandaliwa bila shaka ni kutoka Zanzibar na huyu si mwingine ni Nahodha Vuai. Kapewa ubunge wa kuteuliwa halafu kapewa wizara nyeti ya mambo ya ndani.

  Nahodha Vuai -TZ Prezidaa in 2015...Kama mnabisha kamuulizeni Sheikh Yahaya atawathibitishieni!

  ReplyDelete
 3. Shukurani sana ndugu Matondo kwa hizi habari pevu. Wewe ni mtu mwenye akili sana na Mungu akulinde wewe na familia yako.

  ReplyDelete
 4. @ Kamala. Ndiyo Magufuli anafagiliwa sana kila kona. Ni wazi kwamba anakubalika kiasi kwamba kuna waliodhani kwamba pengine angeweza hata kuukwaa uwaziri mkuu.

  @anony wa pili: Kweli wewe umejivika u-Shekhe Yahaya. Mungu Atuweke hai mpaka hiyo 2015 tuone kama uko sahihi.

  @ anony wa tatu: Mbona kama nakufahamu vile? Mimi huwa sipendi kupakwa mafuta mgongo wa chupa na kama kweli ni wewe yule ninayekuhisi sawa kwani pengine naamini unaamini unachokisema. Japo kusifia na kusifiwa si vibaya, tabia hii ikiendekezwa inaweza kuduwaza akili ikakosa uchambuzi wa mambo na kujivika ngao ya uhasama na upinzani kiasi kwamba ukikosolewa kidogo tu unaona kama vile umetukanwa eti kwa sababu umezoea kusifiwa. Hili ni tatizo kubwa kwa wanasiasa wengi wa Afrika ambao wanapenda sana kusifiwa hata pale wasipostahili.

  Anyway, asante kwa maoni yako na ujumbe wako umefika. Ubarikiwe!

  ReplyDelete
 5. Ndugu yangu Matondo kuhusiana na swala la kwanza nitakujibu hivi.
  Swala la kwanza.
  Kwanza kabisa rejea na kauri ya Rais wetu aliposema kuwa ilimchukua miaka mitatu kuelewa jinsi ya kuiendesha nchi kama rais, Ni mtu huyo huyo aliyeanza siasa wakati akiwa shuleni kama yeye asemavyo na akawa katika baraza la mawaziri kutoka 1988 mpaka 2005, tunaongelea miaka 17, katika muda wote hakujua rais anaendeshaje nchi.
  Pili, Kumbuka ahadi nyingi alizozitoa katika kampeni ambazo zilikuepo kwenye irani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 na zingine ambazo zilikuja wakati akiwa njiani kwenye kampeni zinahitaji kutimizwa katika miaka minne na miezi minane hivi.
  Katika fikra zangu, kutokana na sababu hizi, nafikili ameamua kutokuwa na darasa la mawaziri badala yake ameamua kuchagua watu ambao wataanza tu kazi za uwaziri haraka iwezekanavyo badala ya kusubiri miaka miwili na ushee ya mafunzo na watu hawa kwa historia ya maisha yake katika utendaji kisiasa lazima tu watakuwa wazee.

  Swala la pili.
  Nafikili CCM wameshindwa kupata ufumbuzi mapema wa swala hili kutokana na kuwa na mivutano mingi kati ya ''wanamtandao na watamaduni''. Mivutano hii imeanzia katika kampeni za uchaguzi wa rais wa awamu ya tatu(Mkapa)imekuwa mikubwa zaidi katika kipindi chake cha mwisho.
  Inasemekana nguvu ya Mwalimu tu ndiyo iliyosababisha Mkapa kuchaguliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM. Kwa sasa CCM haina mtu kama Mwalimu.
  Nafikili Ndugu yangu Matondo ushawahi kugusia kuhusu CCM kukosa mtu ambaye anaweza akasimama juu ya kisiki na kuongea halafu wana CCM na wananchi wote wakamsikiliza. Kutokana na hili, CCM ya sasa haina kioo cha uongozi wa baadaye.
  Kwa swala hili Ndugu yangu nasema ni vigumu kutabili kwa sababu CCM ya sasa haitabiliki na uwanja wa siasa Tanzania unabadilika kutokana na CCM kuendelea kujiua yenyewe. Usishangae rais ajaye akatoka Chadema, CUF au Chama cha Ndugu yangu Cheyo(UDP).

  Nakubaliana na angalizo la watu, Hakuna waziri mchapakazi na anaeijua kazi yake kama Mzee Pombe. kuijua kazi nina maana jinsi ya kuruka viunzi vya siasa ya Kiafrika(Tanzania). kama ujuavyo, siasa za kiafrika zimejaa majungu na visasi. Mzee Pombe ni kati ya mawaziri wachache sana ambao ni wasafi na hawapo katika kundi lolote la ''wanamtandao au watamaduni''
  Siwezi kusema lolote juu ya Harrison Mwakyembe, silka za binadamu wengi ni kubadilika pindi wapatapo kile ambacho katika maisha yao yote walikuwa wanakitafuta. najua watu wengi watasema ni mjasiri, aliongoza tume iliyotoa majibu kuhusiana na swala la Richmond mpaka Waziri mkuu kujiuzuru. Nafikili kiongozi makini hapimwi kwa swala moja tu. Tusubiri...

  Samuel Sitta (Ushirikiano Afrika Mashariki). Nafikili Rais hakuwa na uchaguzi(choice) kutokana na yale yaliyotokea kwenye sakata ya uspika, hata Sitta hakuwa na uchaguzi(choice) katika siasa ndo maana ameamua kuikubali hii nafasi kwa vile ni aibu kubwa kukaa bungeni katika viti vya wabunge wa kawaida ukimtazama na kumsikiliza mtu aliyekuwa makamu wako akikupa mwongozo bungeni hasa katika siasa za Afrika.

  Tusibiri tuone utendaji wa Profesa Anna Tibaijuka kama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. ukiangalia hii ni wizara ngumu kutokana na swala la ardhi kwa sasa Tanzania. ninatumaini atafanya vizuri lakini pia utendaji kazi za umoja wa kimataifa ni tofauti na vizingiti vya siasa za Afrika(Tanzania) hasa katika swala ambalo ni zito kwa sasa Tanzania(Ardhi)
  Wabeja!

  ReplyDelete
 6. @Ng'wanaMwamapalala: Asante kwa uchambuzi wako wa kiuoni. Uchambuzi na mtazamo wako kuhusu swali la kwanza wala sikuwahi kuufikiria. Wapo watu wanaolalamikia baadhi ya sura kongwe zilizorudi lakini kulingana na maelezo yako hapo juu, pengine ni lazima kuchanganya - wale wapya na wanaojua kazi tayari + uchapakazi.
  Naona watu wengi wanalisifia sana baraza hili ukiachilia mbali madoa ya hapa na pale. Ngoja tuone litakavyofanya kazi na kama kweli litatimiza matarajio ya wengi.

  Kuhusu swali la pili napenda kuongezea kidogo tu kwamba uwezekano wa CCM kubakia madarakani utategemea uwezo wake wa kusoma alama za nyakati na hasa kuelewa mapito na matakwa ya Watanzania wa sasa. Kama CCM wataendelea na dharau, kutojali, kujiamini kupita kiasi - na wakapuuzia hali halisi kiasi cha kuchagua mtu mwenye jina kubwa tu bila kujali ukubalifu wake kwa jamii, watapata msukosuko mkubwa zaidi kuliko walioupata mwaka huu. Kwa hali hiyo nakubaliana nawe pengine kwa hali ilivyo sasa ni vigumu kuweza kutabiri ni yupi anayeandaliwa kubeba mikoba.

  Kuna wengine wanaoamini kwamba bila kuwa na katiba mpya haitawezekana kuiondoa CCM madarakani kwani mazingira yaliyopo (kuanzia wakuu wa mikoa, polisi na tume ya uchaguzi - ambayo imelalamikiwa sana safari hii) yanaipendelea. Naamini kwamba hata CCM safari hii wameshaona upepo wa mabadiliko na watachukua hatua za dhati kujishabihisha nayo. Siasa!

  ReplyDelete
 7. Ndugu yangu Matondo ninakubaliana na wewe katika hilo lakini Siamini kwamba bila katiba mpya CCM haiwezi kuondoka au kuondelewa madarakani, ninachoamini ni kuwa kwa mazingira ya katiba ya sasa itachukua muda mrefu sana kwa CCM kuondoka au kuondolewa madarakani. Na kama ionekanavyo kwa sasa ni CCM yenyewe itakayojiondoa madarakani badala ya wapinzani kuiondoa.
  Tanzania ya sasa haina watu katika kambi za upinzania wenye nia, uwezo na moyo mathubuti wa kuwatumikia wananchi, kambi za upinzani zimejaa watu wanaotafuta ajira na utajiri kwa mgongo wa siasa na hii inasababisha kuwepo na migogoro kila kukicha.

  ReplyDelete
 8. hakuna anaebisha kuwa Magufuli mchapa kazi na wengine wawili watatu tunaowafaham mtu kama Mwakyembe angepewa wizara sio kunaibu, anaonekana ni mtu anaeweza kutoa shauri au kuamua mambo mazito kutegemea akili na commonsense naona jina lake lilipachikwa dakika za mwisho, sasa mawaziri kama Malima, Mwinyi,Sophia Simba,Ghasia,Ngeleja na wengine kwa uhodari upi wamepewa tena wizara, wengine hao inapofika maamuzi mazito ndio wanaotegemea kuuliza tu hawajui wafanye nini ii mradi waziri, mbona wasomi wengi na wachapa kazi

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU