NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, November 19, 2010

FIKRA YA IJUMAA: TUITAFAKARI TABIA YA HUYU MDUDU

"Kuna methali ya Kipare inasema, yule mdudu caterpillar aliyetulia kuliko wote ndio mla mbegu za mahindi yaliyopandwa. Kwa hiyo ukiona kimya ujue ndio hivyo tena................mbegu zinaliwa!!!!

Albert Ngusaru (Kutoka Facebook)

******

Angalizo

Kwa hivyo ukiona mipango yako mingi haiendi vizuri, chunguza pengine kuna kiwavi (caterpillar) anayemung'unya mbegu za mipango yako kimya kimya. Na usishangae ukigundua kwamba wakati mwingine kiwavi huyo anaweza kuwa ni wewe mwenyewe!  

Wikiendi njema.

4 comments:

 1. Kwa kawaida kiwavi sio MTU mwingine!:-(  Wazo pembeni kidogo:
  Mie kama MPARE nimesikia aibu kwa kuwa nilikuwa sijui methali hiyo ya KIPARE!:-(

  Wikiendi njema kwako pia Mkuu!

  ReplyDelete
 2. ni kweli kaka. Kiwavi mkuu kwa kawaida ni wewe mwenyewe kwani wale viwavi wengine mara nyingi una uwezo wa kuwatimua. Ni ujumbe uliotulia kaka.

  ReplyDelete
 3. Swali: Caterpillar (aka kiwavi) wa CCM ni nani?????

  Hii inafikirisha sana!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU