NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, November 5, 2010

FIKRA YA IJUMAA: WHAT IS IN A NAME? JINA LA BLOGU "LINAPOKINAISHA"

 • Kabla ya kuanzisha blogu hii rasmi hapo tarehe 8/1/2009, nilitafakari sana kuhusu jina, lengo pamoja na mwelekeo wake. Baada ya kutafakari kwa kina niliiamua kutumia methali maarufu ya Kinaijeria isemayo " Chakuka Kitamu na Kichungu vyote Vinaweza Kumfanya Mlaji Akakunja Uso".
 • Nilichagua jina hili ili kuakisi hasa ukweli wenyewe kwamba blogu hii haipo hapa ili kumfurahisha mtu ye yote wala kikundi cha watu; na kama vile msumeno itakereza kote kote. Na kwa vile hakuna upande mmoja tu wa ukweli/ubaya, nilijua tangu mwanzo kwamba mambo nitakayokuwa nikiyaandika hapa yatakuwa matamu kwa wengine na yatakuwa machungu kwa wengine. Kwa wale watakaoyaona ni matamu si ajabu wakakunja uso kwa kufurahia, na watakaoyaona ni machungu kama shubiri basi nao watakunja uso kwa uchungu na kukinaika. Kwangu yote ni sawa!
 • Sasa nimeshangaa kugundua kwamba kuna wadau ambao wamekuwa wakikerwa na jina la blogu hii na hata kuikimbia kwa sababu eti jina lenyewe linaonekana limekaa "kingonongono." Wadau hawa wanasema kwamba japo wanaipenda blogu hii, huwa hawawezi kuitembelea wakiwa maofisini na hata majumbani (wakiwa karibu na watoto) kwa sababu ya kuogopa kushukiwa kwamba wanaangalia mambo machafu.
 • Ni kweli unapoisikia methali ya "chakula kitamu na kichungu vyote vinaweza kumfanya mlaji akakunja uso" picha inayokujia akilini mwako ni ya mambo ya ngono? Kabla hata sijaanzisha blogu hii rasmi, nililipendekeza jina hili kwa Da Mija (ambaye ndiye alinitia moyo hasa wa kuanzisha blogu). Da Mija hakukereka nalo na nakumbuka tu alisema kwamba inawezekanaje vyakula viwe tofauti lakini "reaction" iwe ni ile ile? Da Mija unakumbuka? Ulinitosa nini (utani tu!)?
 • Jambo hili hata hivyo linaakisi ukweli halisi katika maisha yetu hapa duniani: Hata siku moja usitende jambo lolote (hata liwe zuri namna gani) bila kutegemea kuwaudhi watu wengine. Hii inatokana na ukweli kwamba hatujui ukweli/wema hasa ni nini, na ukijumlisha na miingiliano ya kitamaduni, mazingira, malezi, hulka yetu kama wanyama na wakati mwingine kutoelewa mambo tu, mitafaruku ni ya lazima.
 • Nimalizie na swali la kizushi: Ni kwa nini tunaogopa (au pengine niseme tunaipenda) ngono namna hii hata kufikia hatua ya kuinusa kila mahali hata ambapo haikukusudiwa?
 • Wikiendi njema wadau. Kwa wale mliokuwa mkikerwa na methali hiyo ya Kinaijeria, samahanini sana. Haikukusudiwa iwe hivyo!

7 comments:

 1. Kama unawaza ngono 24/7 basi utaona ngono everywhere. Hata Mwanamke wa Shoka utatafsiri kuwa mwanamke wa shoka kitandani.

  The proverb is more philosophical and it made think twice. I never thought that it can be associated with sex!!!

  ReplyDelete
 2. Duh! Kusema ukweli mimi hata sikufikiria huko kabisa yaani kabisaaaaa! First time nilivyoona jina la blog, "chakula" nilitafsiri kama "mada mbalimbali" ambazo wewe kama blogger umeamua kuweka hapa na inategemea na mada yenyewe ikoje, lazima kutakuwa na positive and negative feedback kwahiyo hii ndio ilikuwa tafsiri ya kitamu na kichungu. Yaani huko watu wameenda mbali kweli yaani duh! People got interesting imaginations lol!

  By the way nimeshangaa tu leo naona kwenye blogs I am following then naona "COGITO ERGO SUM...", nilishusha pumzi baada ya kuangalia jina la Author...haha...anyway..just curious! :-)

  ReplyDelete
 3. Candy1 - habari ndiyo hiyo. Watu tuna mawazo tofauti; na mara nyingi mawazo yetu yanaakisi kile tunachokipenda/tunachokichukia.

  COGITO ERGO SUM inapaswa kuwa "blog description" na nilikosea nikaiweka kama blog name. Nimesharekebisha.

  COGITO ERGO SUM - ni kauli iliyotolewa na mwanafalsafa wa Kifaransa aitwaye René Descartes na kwa Kiingereza unatafsiriwa kama "I think, Therefore I am"

  Kwa sasa blogu hii itabakia tu kuwa Matondo. Asante sana!

  ReplyDelete
 4. Mkuu naona umekubaliana na mawazo ya watu. Lakini si kunauwezekano kuna ambao jina MATONDO nalo huamsha hamu fulani angalau kifikira ambazo ni matusi?

  ReplyDelete
 5. Mtakatifu: Hapa duniani nimeshajifunza kuchagua mambo ya kupigania na mambo ya kuachilia tu yapite na yaende kama yalivyo(I choose my wars). Ukiamua kupigania kila kitu basi utapigana vita vingi sana hata kwa mambo madogo madogo ambayo ukiangalia vizuri hayana maana sana.

  Kwa vile jambo hili linahusu mkanganyiko wa jina tu hakuna tatizo lolote. Wanaisimu wanaamini kwamba hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya neno na kirejelewacho. Ndiyo maana leo tukikoma kukuita Mtakatifu na tukaamua kukuita Mkalidayo au Mgalatia, hakuna kitakachobadilika. Sijui kama ni kweli.

  ReplyDelete
 6. @Mkuu Masangu Matondo Nzuzullima: Nahisi nilikuelewa hata kabla hujanijibu.Ni uchokozi tu Mkuu!Na kweli usipochagua vita unaweza kujikuta huishi kama wewe !:-(

  ReplyDelete
 7. Nimekupata Mtakatifu (au pengine nikuite Mgalatia!). LOL!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU