NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, November 8, 2010

HABARI NDIYO HIYO: TAKURURU YAMSAFISHA RASMI MBUNGE WANGU. NJIA YA USPIKA SASA NYEUPE?

 • Siasa za Tanzania kuna wakati zinashangaza, zinatatanisha na hata kuchanganya. Mbunge wangu (Mzee wa Vijisenti) sasa kasafishwa rasmi na TAKURURU kwamba hakuhusika na kashfa ya rada. Je, hii ina maana kwamba ndiyo ameshasafishiwa njia ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kuna nini ambacho kinawafanya CCM wamkumbatie sana mbunge wangu huyu mwenye kashfa na kesi ya mauaji mahakamani? Ni kweli hakuna wanachama wengine wenye uwezo na wasio na madoa wakagombea nafasi hii muhimu? Baada ya misukosuko waliyoipata katika uchaguzi huu mtu ungedhani kwamba CCM wangejitathmini na kurekebisha baadhi ya mambo muhimu yaliyowafanya wasukwesukwe, mojawapo likiwa hili la kufungamanishwa na ufisadi. Inashangaza sana!
 ************

YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA

Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.

TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.

Imetolewa na

Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010
S. L.P. 4865,
Dares Salaam. Simu: 2150043-6/2150360 Nukushi: (022) 2150047 Baruapepe:dgeneral@pccb.go.tz
Mtandao www.pccb.go.tz
************

Taarifa hii ni kutoka Lukwangule Entertainment.Kwingineko: Mh. Chenge mwenyewe anagombea USPIKA kwa sababu

"...nagombea kiti cha uspika nikiamini kwamba ninao uwezo wa kutibu majeraha makubwa yaliyoumiza Bunge na Taifa, wananchi na chama changu (CCM) kwa sababu tu ya kuwa kiongozi aliye tayari kujitafutia na kujitwalia umaarufu au ushujaa wake binafsi kwa njia ya kuwahujumu, kuwaumiza na kuwachafua wengine kwa kutengeneza tuhuma na kashifa za kila namna. Tiba ya uongozi wa aina hii ni kuchagua kiongozi bora wa bunge...."

Nukuu hii ni kutoka Wavuti.

Kwa habari zaidi kuhusu sakata hili soma hapa

5 comments:

 1. Kimsingi anachofanya Chenge ni kutaka kulinajisi bunge kwa kuwapa mafisadi wenzake sehemu ya kujisafishia na kupanga dili nyingine kubwa zitakazoliacha taifa msambweni kama si kaburini. Anasifika kwa kuwahonga na kuwapofua wapiga kura wake. Anaiba sana ili awahonge sana nao wamchague sana. Je kipi muihimu-kutatua matatizo ya mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla? Kwanini kuiba pesa ya nchi ili kuwahongo watu wa eneo lake?
  Hakuna kimenishangaza kama alivyoonyesha jeuri ya kifisadi hadi kufikia kugombea hata uspika. Ili iweje? Tujalie mbunge wa upinzani aje na hoja ya kutaka kujadili wizi wa rada, Chenge kama spika kweli ataruhusu hiki kitanzi kivikwe shingoni mwake? Je wabunge wetu nao watakuwa wameishiwa kiasi gani kumchagua mtuhumiwa wa uhujumu hivi? Yetu macho na nani ajuaye iwapo ufisadi nchini mwetu umehalalishwa huku uadilifu ukiharamishwa?
  Na kwa kumsafisha, kama NEC, TAKUKURU imethibitisha dhana kuwa ni Taasisi ya Kudumisha na Kutetea Rushwa basi.
  Chenge hafai hata kuwa spika wa kijiwe cha kahawa achilia mbali bunge letu tukufu.

  ReplyDelete
 2. Tanzania, Tanzania
  Ninakupenda kwa moyo wote...
  Nilalapo nakuwaza
  Jina lako ni tamu sana....

  CCM kweli kiboko!

  Wapinzani anzeni kujijenga mapema. Operesheni sangara iendelee ili mwaka 2015 Kabwe aingie ikulu. Tumechoka sasa!!!

  ReplyDelete
 3. CCM are full of surprises! tegemea surprise nyingine kwa kumuidhinisha chenge kugombea uspika. Kama katika uchaguzi mkuu wananchi walishindwa kuuona ufisadi kuwa ni kitu kibaya na hivyo kutowatupilia mbali mafisadi (kama hakukuwa na uchakachuzi), CCM hawataogopa tena na watamuidhinisha chenge. CCM huwa hawaamini kukosea. Bado wanadhani kukwiba pesa za watanzania ni haki yao. Kama mwenyekiti wa CCM taifa alimnyanyua mkono chenge kumnadi kuwa ni mtu safi watashindwa nini kumthibitisha angombee ubunge. hakika hawaoni kuwa wana dhambikwa watanzania. watampitisha chenge ili wakwibe vizuri alaf come 1015 nyimbo za tanzania ina 'amani na utulivu'titatawala tena.

  go chenge go!

  ReplyDelete
 4. mimi nimesoma habari hii nikazimia. ndio sasa hivi nimeanza kurudia hali ya kawaida!!! Hii ni kufuru!!! lakini pia inaweza kuwa baraka nyuma ya pazia - maana atazima hoja za wapinzani hali ambayo itawapa sababu ya kwenda kuwashitaki kwa wananchi. Kweli sasa nimepata akili, tupige debe mzee wa vijisenti apewe uspika.

  ReplyDelete
 5. Kwani Spika lazima atokee chama tawala, mimi kwanza nawaza kwanini kiongozi wa wabunge atoke ndani ya chama, kwanini asitoke nje ya chama...ingekuwa fair play!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU