NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, November 11, 2010

LEO NI SIKUKUU YA MASHUJAA HAPA MAREKANI: ATI, SISI TUNAWAENZIJE MASHUJAA NA WAASISI WETU?

 • Leo ni siku ya mashujaa hapa Marekani na ni siku ya mapumziko. Jana kuanzia saa mbili asubuhi wazazi tulikusanyika shuleni ili kushuhudia michezo, nyimbo na maigizo ya watoto wa darasa la nne katika kuwakumbuka mashujaa wao. 
 • Tukio hili lilinivutia sana kwani wenzetu hawa wanajibidisha kwelikweli kuhakikisha kwamba watoto wao wanakumbuka historia ya mashujaa na waasisi wao. Nyimbo za kizalendo ziliimbwa, hotuba za maraisi mashuhuri wa Marekani zilisikilizwa, vita vilivyopiganwa vilionyeshwa, nukuu muhimu za watu mbalimbali zilirejelewa, matukio muhimu katika historia yao (mf. kutua mwezini, Space shuttle na bomu la kwanza la nyuklia)  yalizungumziwa na hata Historia ya Utumwa pia iligusiwa. Kulikuwa pia na mashindano ya kutaja majina ya maraisi wote 44 pamoja na majimbo yote 50 kwa mpangilio.
 • Mwishoni kabisa wimbo mmoja wenye maneno yasemayo "I love the USA" ulipokuwa ukiimbwa, niliweza kuwaona wazazi wengi wakidondokwa na machozi. Halafu wazazi wote waliowahi kwenda vitani waliombwa kusimama; na walishangiliwa kwa kelele na vifijo vya kila aina. Lilikuwa tukio la kusisimua sana!
 • Binti yangu ya kwanza yeye aliigiza kama Harriet Tubman, mwanamke shujaa mweusi ambaye alishiriki kikamilifu katika jitihaza za kutokomeza biashara ya utumwa hapa Marekani.
Kutoka kushoto: Susan B. Anthony, Martin Luther King Jr, John F. Kennedy (mbele ya mikrofoni), Eleanor Roosevelt (nyuma ya J.F. Kennedy) na Harriet Tubman.
 • Wakati nikitazama maonyesho haya, wazo moja lilikuwa likipitapita kichwani mwangu. Hivi sisi tunasherehekeaje sikukuu ya mashujaa wetu - akina Kinjeketile, Mkwawa, Mirambo, Nyerere na wengineo? Nilisikitika kidogo baada ya kukumbuka kwamba hata kutazama video za waasisi wetu na kusoma maandishi yao bado ni hati hati.  Inavyoonekana, hata kuwaenzi tu mashujaa na watangulizi wetu napo hatuwezi. Kwa mfano, kwa nini maandishi na hotuba za mashujaa na waasisi wetu ziwe adimu mpaka tunafikia hata hatua ya kuziwekea hati miliki kinyemela na kuwakoromea wale wanaojaribu kuziweka peupe? 
 • Nilitembelea pia ubao wa matangazo wa watoto wa darasa la kwanza. Hawa walikuwa wameambiwa kuandika juu ya umuhimu wa uhuru katika maisha yao kama Wamarekani. Hapa chini ni baadhi ya majibu yao:
imagebam.comimagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com

Mwisho, msikilize mtoto huyu akitaja majina yote ya marais 44 wa Marekani kwa mpangilio....

3 comments:

 1. Unajua historia yetu imegubikwa na sintofahamu nyingi, manake ukikumbukia hilo utakuta unawasuta wakoloni ambao ndio wafadhili wetu!
  Hata historia kamili imegeuzwa geuzwa ilimradi isitoe picha kamili. Sikukuu ya mashujaa hapa ipo, lakini...mmmh, Mkwawa , Mirambo, Kinjeketile, Sina Mangi na wengineo imebakia kama `hadithi fulani ya paukwa pakawa'.. Shujaa amabye labda anajulikana na anasifiwa ni baba wa Taifa, huyu tunashukuru siku yake inathaminiwa, lakini hawa waliofikia hata kumwaga damu kwa ajili ya kulinda ardhi ambayo tunaishabikia na kunadi sera zetu juu yake sisikii kwa saana tukikumbuka siku zao!
  Badi sisi tupo nyuma kwa kila kitu mapaka tufadhiliwe, na je atakufadhili nani katika siku ya `kuwakebehi, au kuwasema wao kama wakoloni'

  ReplyDelete
 2. Hata hiyo siku ya Nyerere ni unafiki mtupu. Mbona hotuba zake na maandishi yake bado ni vigumu kuzipata? Kumbukumbu ya Nyerere basically ni kwa wasomi tu lakini hata CCM yenyewe haijali.

  Problem ya Nyerere ni kwamba alikuwa anapinga sana ufisadi. Na hii ni fatal mistake kwa Makamba na kundi lake. That is why wanadhibiti mambo yake yasienee.

  We are not proud of ourselves, we are not proud of our culture, we are not proud of our history, we are not proud of our achievements (if any), WE ARE NOTHING!!!

  ReplyDelete
 3. The second child kwenye hayo maoni ya watoto is 100% right na kama kweli ni std 1 basi ni very impressive.

  "Freedom means to do what ever you want to do, but don't brake the law"

  Halafu tunacomplain eti kwa nini hawa jamaa wameendelea. Mfumo wao wa elimu ni bora sana. How about us?

  Aika nawe dah! WE ARE NOTHING! Una uhakika?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU