NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, November 5, 2010

MBUNGE WANGU KWELI "NGANGARI": SASA ANAUTAKA USPIKA!

 • Mambo ya siasa (na hasa uchaguzi) yamenichosha sasa lakini hili la mbunge wangu limenivutia. Ni mwenyewe Mheshimiwa Andrew Chenge (aka Mzee wa Vijisenti). Na sasa anautaka Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na sitashangaa kama ataupata.
 • Ni mambo kama haya ya kutojali na kudharau maoni ya wananchi wa kawaida ndiyo hatimaye yatachangia kuiangamiza CCM. Inavyoonekana chama hiki kikongwe na chenye historia ya pekee hakijajifunza lolote la maana kutokana na misukosuko kiliyoipata katika uchaguzi wa mwaka huu. Picha na habari zaidi kutoka Burudan Blog.

4 comments:

 1. "Ni mambo kama haya ya kutojali na kudharau maoni ya wananchi wa kawaida ndiyo hatimaye yatachangia kuiangamiza CCM"

  Well said. I hope that they are listening. Otherwise in 2015 Kiyama kitawashukia tu.

  ReplyDelete
 2. Mimi nadhani hawa mafisadi pengine wanawatumikia wananchi majimbo yao vizuri bila sisi kuelewa kwa undani. Matondo, wewe unamfahamu vema mzee wa vijisenti unaonaje mchango wake kwa wapiga kura wake?

  ReplyDelete
 3. Bwana Matiya: Kusema kweli wapiga kura wa kijijini nilioongea nao mwezi wa sita hawakuwa na la kuonyesha kuhusu maendeleo ambayo wameyapata kwa Mheshimiwa huyu.

  Kitu pekee walichomsifia sana ni ile tabia yake ya kuwatatulia matatizo yao kwa mtindo wa papo kwa papo kwa kuwapa pesa na vitu kama baisikeli, nguo, mabati n.k. Yeye hufanya hivi hata kama siyo wakati wa kampeni. Akiweko nyumbani watu hujidamka asubuhi kwenda kutatuliwa shida zao - wenye wagonjwa mahospitalini, wasio na karo za kusomeshea watoto wao n.k. Kijana mmoja jirani yetu ambaye alikuwa mlemavu yeye alinunuliwa baisikeli ya walemavu. Kwa hivyo kusema kweli wapiga kura wanampenda sana.

  Mimi binafsi ningependelea kama angekuwa anatumia mapesa haya kuwatafutia wapiga kura wake masuluhisho ya kudumu kwa matatizo yao mf. kuwachimbia visima vya maji, kuwaboreshea zahanati zao, kujenga madarasa n.k.

  Chenge anasifika pia kwa kupunguza nguvu za UDP ambayo kabla hajawa mbunge ilikuwa inatamba sana. UDP ina matatizo yake ambayo yalisababisha isipendwe na wapiga kura wengi na Chenge anaonekana kama shujaa kwa kuwaokoa.

  Mradi mkubwa wa kimaendeleo ambao ulikuwa mbioni kutekelezwa ni ujenzi wa barabara ya kutoka Bariadi kwenda Lamadi ambako itaungana na barabara inayotoka Mwanza kwenda Musoma na hatimaye Kenya. Mwezi wa sita tayari kulikuwa na Wachina waliokuwa wamepiga kambi tayari kuanza ujenzi huo. Natumaini kwamba hayakuwa mambo ya kampeni tu. Kama barabara hii itajengwa basi utakuwa ukombozi mkubwa sana kwa wananchi wa Bariadi kwani wakati wa mvua usafiri wa kwenda Mwanza huwa ni kazi kweli kweli.

  ReplyDelete
 4. Kimsingi anachofanya Chenge kwa mujibu wa maelezo ya Matondo ni kuwahonga na kuwapofua wapiga kura wake. Anaiba sana ili awahonge sana nao wamchague sana. Je kipi muihimu-kutatua matatizo ya mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla? Kwanini kuiba pesa ya nchi ili kuwahongo watu wa eneo lake?
  Hakuna kimenishangaza kama alivyoonyesha jeuri ya kifisadi hadi kufikia kugombea hata uspika. Ili iweje? Tujalie mbunge wa upinzani aje na hoja ya kutaka kujadili wizi wa rada, Chenge kama spika kweli ataruhusu hiki kitanzi kivikwe shingoni mwake? Je wabunge wetu nao watakuwa wameishiwa kiasi gani kumchagua mtuhumiwa wa uhujumu hivi? Yetu macho na nani ajuaye iwapo ufisadi nchini mwetu umehalalishwa huku uadilifu ukiharamishwa?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU