NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, November 8, 2010

MDAU ANAULIZA: JAMII FORUMS NI MALI YA CHADEMA? INATUMIWA KUFANYA UCHOCHEZI? NI ZE UTAMU MPYA?


Jamani eeh! Mjumbe hauwawigwi. Nauweka ujumbe huu kama ulivyo...

****************

JAMII FORUMS NI MALI YA CHADEMA? INATUMIWA KUFANYA UCHOCHEZI? NI ZE UTAMU MPYA?

Dr. Matondo. Kila siku huwa natembelea blogu yako kwa sababu kuu mbili. (1) Iko balanced. Huegemei CCM wala CHADEMA na unakosoa na kusifia pande zote bila upendeleo kila inapobidi na kustahili. Napenda pia staili yako ya uandishi wa ki-summary, wenye kufikirisha sana na uliopangiliwa vizuri. (2) Collection nzuri ya blogu zote muhimu tena ziko arranged kufuata topics. Huwa napita kuangalia headings za blogu mbalimbali kabla sijaamua kuchagua mada au blogu ya kusoma. Hata kama blogu yako haina wasomaji wengi, usikate tamaa. You are making a difference kwa watu wachache wanaopenda mambo ya maana na mawazo ambayo yako mature.

Leo hata hivyo nataka kuleta hoja hapa kuhusu hawa jamaa wa Jamii Forums a.k.a "Home of Great Thinkers" Binafsi nilikuwa memba wa Jamii Forums kwa muda mrefu sana mpaka hivi karibuni nilipoamua kujitoa na kukimbilia Wanabidii baada ya forum kupoteza mwelekeo na kugeuka kuwa another Ze Utamu. Ni wazi kwamba Jamii Forum sasa inatumiwa kama ukumbi wa CHADEMA na inafanya kazi ya uchochezi. Kwa nini nimefikia conclusion hii?

(1) Huko Jamii Forums hoja na mawazo mbadala sasa haviruhusiwi. Ukijaribu kuleta mawazo na hoja mbadala na ukajaribu kuikosoa CHADEMA au kumsema vibaya kiongozi wao (Dr. Slaa) basi utatukanwa na kushambuliwa sana hata kama unatoa hoja nzuri na kwa njia za kistaarabu. Kwenye Jamii Forums CHADEMA na Dr. Slaa ni miungu wanaoabudiwa. Slaa anaitwa rais mteule, masihi wa Tanzania, mkombozi wa wanyonge n.k. Ukisaili tu uhalali wa madai haya basi wewe ni msaliti, msenge uliyeleweshwa kasumba za CCM na ni mtu wa kuonewa huruma. Na matusi utakayotukanwa basi hutakaa uyasahau. Wakati huo huo ni sawa kuwatukana viongozi wa CCM na taifa letu bila wasiwasi wo wote. Huko rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatukanwa, anabezwa na kuitwa majina mbalimbali. Yote hii ni sawa lakini kamwe huwezi kumgusa masihi wao Dr. Slaa. Kwa nini? Ni kwa sababu hii, naamini kwamba Jamii Forums ni mali ya CHADEMA. Kama hii ni kweli basi waendeshaji wake inabidi waseme hivyo ili kila mtu anayekwenda huko ajue. Na hii inaonyesha hasa CHADEMA inaundwa na watu wa aina gani. "Great Thinkers" huwa hawatumii matusi kama silaha bali hutumia hoja. Hata wewe utakapoweka hoja hii si ajabu ukaishia kutukanwa na kutishwa.

(2) Katika kipindi cha uchaguzi na baada ya matokeo kutangazwa, Jamii Forums imeibukia kuwa chombo cha propaganda za CHADEMA na chombo cha uchochezi. Ni chombo cha watu wenye jazba, hasira na mihemko mikali kiasi kwamba wengine wanasema eti wako tayari hata kufa ili kutetea na kuipigania nchi yao na kura zilizoibwa (wanaita kuchakachuliwa). Kila mbunge wa CCM aliyeshinda uchaguzi basi ni lazima amechakachua kura na hatua ni lazima zichukuliwe ili kuhakikisha ushindi kwa CHADEMA unapatikana. Jazba na hasira zilizoonyeshwa huko mpaka zinatisha. Sote tunajua nafasi ya vyombo vya habari katika kupalilia na kuchochea misukosuko kule Rwanda, Burundi na sehemu zingine zenye machafuko. Jamii Forums inaingia moja kwa moja katika vyombo vya aina hii na inashangaza kuona kwamba mpaka hivi leo serikali imekaa kimya tu inaangalia. Mpaka lini?????

Jamii Forums ni mtandao ambao ulianza vizuri sana na una nafasi kubwa mno katika kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii yetu. Hata hivyo kwa sasa mtandao huu umegeuka na kuwa genge la wahuni wenye jazba na hasira kali, wahuni ambao wako tayari hata kuleta machafuko nchini ili kufikia lengo lao la kisiasa kupitia CHADEMA na Padri wao mteule.

Natumaini kwamba serikali inau-monitor mtandao huu ili usije ukaiingiza nchi yetu katika matatizo makubwa. Natumaini pia kwamba serikali haitachelewa kuchukua hatua kama walivyofanya kwenye Ze Utamu. Amani tuliyonayo si mali ya CHADEMA wala ya Dr. Slaa na haipaswi kuchezewa na mtu ye yote yule. Waendeshaji wa Jamii Forums inabidi watambue kwamba mikono yao italowana damu kama jazba na uchochezi wanaoufanya utavuvumka na hatimaye kuwasha moto katika nchi yetu iliyozoea utulivu na amani.

Asante na natumaini kwamba hutaogopa kubandika ujumbe huu. Mungu Ibariki Afrika. Mungu Ibariki Tanzania!

Ni mimi Mtanzania Halisi (aka Kalumekenge)

Mbeya (Tz)

22 comments:

 1. Wakati mwingine siasa ukiingiza katika `imani' na kutawala hisia zako unaweza `ukawa na chongo ukaliita kengeza.
  Hata wanataaluma wakasahau utaaluma wao kwasababu ya kitu `kupenda', kalamu wakaigeuza pakuandikia pakawa juu!
  Wakati mwingine uanweza kusema ni sawa kwa vyovyote iwavyo wote hatuwezi kuwa weupe, au weusi,na nyoyo zetu halikadhalika, lakini `mpaka' hasa unapoitwa `mwanataaluma' unatakiwa kuzingatiwa!
  Lakini tukubali kuwa katika uchaguzi, kila mtu ana mapendeleo yake, na angefurahi mapendeelo yake yapendwe na wote, uwe kama mimi au mwanata-aluma, na kwahiyo juhudii hufanywa kibanafsi, wengine kwa dhahiri wengine kwa uficho, ili...ili...!
  Mimi labda kwa uoni wangu kama `utaaluma' wako ni wa watu wote wakati mwingine inabidii `ufe na tai shingoni' simamia haki, na haki hiyo iwe sawa, ili mwisho wa siku kama si leo watu wakupe mkono wa `ushujaa', na hata wasipokupa, lakini kumbukumbu zako zitaheshimika milele na milele!
  Nimewaza tu mkuu!

  ReplyDelete
 2. WANA jamii Forum,sio chadema-hata CCM tumo-ni mtandao pekee TZ ambao watu wameamka-wengi wetu tumeshatembea nje na kuona maendeleo yanatakiwa vipi? KAMA amani itavurugika,so be it-sacrifices have to be made ili nchi yetu isonge mbele-mimi leo sipati usingizi wakati miaka lukuki baada ya uhuru majority ya watanzania hawapati square meal,hawana matibabu safi na hawana nyumba bora

  ReplyDelete
 3. Ndugu K/Kenge, fikra za wana Jamiiforums zinawakilisha fikra za sehemu kubwa ya watanzania wenye ufahamu wa kutosha kuhusu nchi yetu. CCM wameendelea kutumia umbumbumbu wa watanzania kama mtaji wao wa kisiasa. Ukiwagusa tu, watatumia karata za 'udini', 'amani yetu' na nyingine kama hizo. Wewe mwenyewe unatoa hoja zinazoonyesha dhahiri UCCM wako. Kama sio umbumbumbu wako, basi utakuwa unafaidi nchi kwa ufisadi unaopata malezi kutoka CCM na serikali yake. Si wote walioko Jamiiforums ni CHADEMA. Nakupiga mkasi, rudia 'homework' yako wewe K/Kenge

  ReplyDelete
 4. huyo anae jifanya k/kenge mbona anaenda nje ya mstari tena kama ni mwandishi ana maana gani kusema huyo padri wao slaa, naona yeye ndio anataka kusababisha vita ya mapadri na mashehe, ameandika kwa jazba, ajue kuna wengi wenye jazba kama zake sasa hatutafika mbali, usihusishe chadema na hao jamii forum, hao labda ni watu binafsi, nilichosikia chadema wakisema ni serikali itoe elimu bure, watu makazini wawajibike, rushwa isiwepo sasa kuna wanaosema eti kusema hivyo ni uvunjaji wa amani na udini wapi na wapi, wenye udini wanaonekana

  ReplyDelete
 5. Kalume kenge hana ajualo! Si ndio yule yule aliyefananisha ngoma kubwa na mat...o* makubwa katika zile pcha za Mheshimiwa Rais kule Mwanza??? Mtu huyo kweli anaweza kuwa na perspective sahihi kwa chochote anachoona ama kusoma ama hata kusikia? Watu kama hawa ndio huwa wanavuruga amani!

  ReplyDelete
 6. Tusimbishie aka Kalumekenge yeye amesema ukweli ndani ya Jamii Forum kuna matusi kibao tena kwa Rais, kabila lake,n.k. ameshaapishwa na analiongoza Taifa lililomchagua. sitapenda lugha za Jamii Forums tuziingize humu kwa matondo

  ReplyDelete
 7. Haswaa. Nina-mwunga mkono huyo mchangiaji wa mwisho. JAMII FORUM imekuwa ya CHADEMA na si uwongo. Tena inawezekana ikawa imeanzishwa na wale CHADEMA papa wa Ulaya na Amerika ambao walipiga hesabu zao za kuingia Ikulu kwa idadi ya Wakristo nchini Tanzania. Kumbe, amesahau kuna Walutheri, Waprotestanti, Waangalikana, na kadhalika. Mawazo yao walifikiri kwamba hii nchi ni ya Wakatoliki na Wakristo wote ni Wakatoliki. Halafu rais anapotaja suala la udini limeotokea wao wanambishia na kusema kwamba eti hana lolote ameishiwa la kusema na anachosema si cha kweli wakati hali kaiona. Mkumbuke kwamba yule ni rais wa nchi na yote yanayotokea lazima taarifa awenazo! Udini ulikuwepo na hata Kabwe alikiri kwa hilo. LAKINI, CHADEMA waliowengi hili hawalitaki na wala hawakubaliani nalo kama jinsi wanavyopinga katika chama chao kuwa ni cha watu wa kaskazini. Ukiuliza watakwambia, oh, mbona Kabwe, Mbona nani sijui. Yaani, utapewa very minor number ya watu wa kanda zingine zaidi ya kaskazini. Jamani, tunasubiri mtakachokifanya katika majimbo yenu kwa miaka hii mitano na mtupe takwimu ya shule, maghorofa, miradi, mabarabara, mahospitali, na uwezeshaji wa wananchi mliofanya katika miaka mitano yenu mlioyonayo kwa sasa. Sina mengi kwa sasa,

  Wenu,

  Muddyb

  ReplyDelete
 8. wewe kweli ni kenge, wa kukimbia mvua na kukimbilia mtoni. ccm si chama, ni kichaka cha mafisadi wanaoiba rasilimali ya nchi hii huku wakitupumbaza na wimbo wa amani, ukiongea ukweli unaonkana mvunja amani, wakiishiwa hoja wanakimbilia udini ukabila. kumbuka cuf walivyoandamwa na tuhuma hizo za udini na ugaidi. ukombozi haupatikani kwa kuichekea ccm, na ukombozi wa ukweli unapatikana kwa damu, lazima watu wajitolee hata kufa (kujitoa kafara)

  ReplyDelete
 9. Mimi sina wasiwasi wowote kwamba mtizamo na muelekeo mzima wa wamiliki wa Jamii Forum ni wa kichadema. Hilo wala halihitaji kupoteza mda kulijadili kwa mtizamo wangu. Na hilo lenyewe kama lenyewe sio tatizo maana kila anaeanzisha mtatandao wake anakuwa na malengo yake. Ambacho ningependa kuwaomba wamiliki wa mtandao huu ni kuendelea kutupa nafasi wachangiaji wengine ambao sio Chadema kutoa hoja zetu hata kama zinapingana na mtizamo wa Chadema. Kwa hilo kwa muda wote ambao nimekuwa mwanachama wa Jamii Forum nashukuru kwamba limekuwa linazingatiwa kwa kiasi cha kuridhisha. Jambo moja nitaendelea kulilalamikia siku zote. Wamiliki wa jamii Forum wanaruhusu maandiko ya baadhi ya wachangiaji wao yanayokashifu wachangiaji wenye fikra tofauti nao. Mara nyingine wamekuwa wakiwakashifu hata watu wengine walionukuliwa na vyombo vingine kutoa maoni kinyume na Chadema. Mfano mzuri ni mijadala inayoendelea kuhusiana na kauli za Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mzee Mkono kuhusiana na madadiliko ya Katiba.

  George Jinasa

  ReplyDelete
 10. Kevin (a.k.a Mwenye Busara)January 8, 2011 at 6:43 PM

  Naungana na George Jinasa. Jamii Forums imeshapoteza mwelekeo na naomba iache kujiita eti Home of Great Thinkers! Badala yake iwe Home of wachochezi na wapiga majungu. Na sijui kwa nini serikali inaiachia iendelee kueneza chuki namna hii.

  ReplyDelete
 11. Jamii forums wanaongea ukweli mtupu kwa kila kitu, na hawa watu kila wanachokijadili wanatoa evidence,hawa ni watu makini sana.Wewe kalumeKenge tatizo lako uliingia kule kwa gia ya uccm.Yote yaliyojadiliwa kule ni ukweli mtupu, na kama kunamada ambayo si ya kweli mtu huyo anashushuliwa na kuulizwa umepata wapi habari hiyo.Kwa vile wewe kilakitu unalipiwa na resikali ndo mana huoni kinachojadiliwa kule,pole sana,ipo siku utakujagundua kuwa kumbe Jamii forums walikuwa wakisema kweli.

  ReplyDelete
 12. wezi na wabadhilifu wa mali za umma mnapoona kuna watu wanawapinga huwa makimbilia hoja za udini, uhuni ,uvunjifu wa aman . Jamii forum ni forum pekee ya wana jamii inayo wafungua macho watanzania waamke kudai haki zao.na ahdema ni chama pekee kinachotaka kumkomboa na kumletea maendeleo mtanzania hilo ndilo linalopelekea mtazamo wa wana jamii forum na chadema vifanane Hongera sanna jamii forum. hongera sana chadema

  ReplyDelete
 13. usiache mbachao kwa msala upitao....u were great thinker kabla hata ya chadema,so continue to be a great thinker sababu upo ndani ya chama kongwe CCM.

  ReplyDelete
 14. Tatizo ni kwamba kila chama kinachoonekana kina nguvu na uwezo wa kuitoa CCM madarakani kinapachikwa swala la udini, kumbuka CUF waliambiwa ni chama cha waisilamu na sasa CHADEMA wanasema cha wakristo. Udini ni mbinu tu ya watawala (CCM) kuwagawa wananchi wakati wa uchaguzi. Kwa sababu sasa CUF wamefungwa mdomo kwa muafaka wa Zanzibar sisikii wakiendelea kusema CUF ni cha udini (Uisilamu) sijui CUF kimekua chama cha nini sasa?

  ReplyDelete
 15. Matondo posti yangu kule si geni kwako kwani wewe ulishawahi kulitotea majibu ni kuhusu majibu mepesi ya JK kwa maswali makini. Si kweli kwamba JF ipo kwa ajili ya kutetea Chadema, labda kwa wachangiaji lakini mimi nadhani moderators na wamiliki wa forum ndiyo kikwazo. Kusema ukweli posti zangu zote walizotiwa kapuni ziliwagusa wachangiaji na hivyo akajitokeza mwanamama mmoja pale ambaye inaonekana ana nguvu kubwa, kwa vile ni JF premium member huyu alianza kuwafundisha wachangiaji kiswahili badala ya yaliyomo kwenye posti. Haikupita muda mara posti yangu ikatoweka pamoja nakuchangiwa na wadau wengi tu. Kwa kifupi ni hayo yaliyonisibu kule JF kabla sijapigiwa BANNED!! japo binafsi nilikuwa nikiombea hilo litokee kwa maana nilishawachoka. Haiwezekani posti zangu ziwe zikitoweka kimiujiza bila ya mimi kuelezwa kosa langu, pamoja na kuwa naamini sikutumia lugha chafu wala kumkashifu mtu.

  ReplyDelete
 16. JAMII FORUM = CHADEMA haina ubishi

  ReplyDelete
 17. jamii forum ni mali ya chadema na wa wakriso kwani ukiwa muslim ukatoa mchango wako pia utashambuliwa mm wananiboa!!!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 18. Hebu watanzania wanaotoka mkoan wa ruvuma wajaribu kwa umakini kuibana serikali kurekebisha masuala ya umeme. Ni aibu hata pale tunaoiona hospitali ya mkoa kushindwa kufanya kazi ya kuokoa maisha ya watu kwa eti umeme ndio sababu....

  ReplyDelete
 19. Jamani, ndani ya mtandao wa Jamii Forum sikutarajia kukutana na watu wenye mawazo mgando kama ya ndugu yangu Karumekenge. Ndo hawa hawa wanaosema amani inatishiwa pale tu Watanzania walio hai kifikra wanapojitokeza kuielimisha jamii ya Watanzania wachache walio katika lindi la usingizi wa kutokujua haki na wajibu wao kwa viongozi dhaifu hapa nchini. Ni dhahiri huyu atakuwa katumwa na maskini fikra walio madarakani ambao wanaamini maendeleo yetu yatapatikana endapo nchi tajiri zitaendelea kuwekeza kwa sharti fulani fulani ambazo kimsingi hazina maslahi kwa taifa letu. Apuuzwe jamani huyu Karumenyoka tena swira.

  ReplyDelete
 20. ndugu k/kenge nimeona unalalamika watu kutumia lugha za matusi.........uko sawa haina ubishi lakina cha kushangaza katika one of the older posts wew ni mmoja wa watu walotumia matusi mfano ni kwenye zile picha za kikwete akipiga ngoma......au ndo kusema ya kwako ni matusi matakatifu????????kabla hujatoa kibanzi kwa mwenzako ondoa kwanza boriti jichoni mwakoooooooo.

  ReplyDelete
 21. SIO JAMII FORUM HATA RAIA MWEMA UKITOA MAONI YANAYOIREKEBISHA CHADEMA HAYAWEKWI HADHARANI ILA SO LONG WANAYASOMA IKO SIKU WATABADILIKA SINA UHAKIKA KWAMBA KUZUNGUMZA NI KUTENDA LA HASHA PATRICK CHILUBA ALIPANGA MAWAZO VIZURI AKAWEZA KUMWONDOA KENETH KAUNDA NAFIKIRI KWA KIZAZI CHA DOT COM KUELEZA HAYA NI SAWA NA KUTWANGA MAJI KWENYE KINU CHILUBA ALIVURUNDA NCHI BAADAYE ALIONDOLEWA SI AJABU KUTOKANA NA UZEE CCM JICHO MOJA LIMEPOFUKA NI CHONGO HIVYO UENDESHAJI WA GARI NI MATATIZO LAKINI WEHU KUMRUHSU KIPOFU AENDESHA GARI ZENU WOTE MUJIANDAE KUELEKEA KUZIMU TUNAANGALIA MAMBO MENGI KAMA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA CHENYEWE TOKA SHINA HADI TAIFA ,RASILIMALIWATU,SERA;UZALENDO,KUVUMILIANA ,UADILIFU . NA MENGINEO SI VEMA KUJARIBU KUFA WALIOKUFA MBONA HAWARUDI WAKATUPATIA MSHINDO NYUMA

  ReplyDelete
 22. Siwezi kukupinga wala kukubaliana nawe! Waswahili wanamsemo wao usemao: "Mwamba goma huvutia upande wake" Kama umesoma Russian Revolution au French Revolution utagundua kitu, Watanzania wanamatatizo mengi sana ambayo hayaandikiki wala kuelezeka mbele za watu. Na wanaamini Serikali iliyopo madaraka haiweze kuyatatua. Sasa basi anapotokea mtu yoyote akawaambia kuwa matatizo yao anaweza kuyatatua, iwe kasema kweli au la huyo kwao ni Mkombozi. Ni sawa na mgonjwa atafutaye dawa, ukimwambia kuwa mavi yake ni dawa ya ugonjwa wake atakula tu. Nadhani hata wewe utakuwa shahidi wa kile kilichotokea Loliondo. Tuludi ndani: Sasa basi Watanzania kuwatukana Viongozi wao hasa Rais wao katika mitandao mbalimbali ni sawa na yule mgonjwa. Wanaamini ndiyo njia yao ya kumaliza hasira zao dhidi ya matatizo yao au kupata nafuu ya maisha yao. Kwa maana hii si sawa kulinganisha JF na CHADEMA. Chadema ni Mkombozi wa baadhi ya Watanzania kwa mtazamao wao na JF ni sehem tu ya makutano ya Watanzania kwa ujumla kujadili matatizo yao bila kujali itikadi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU