NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, November 27, 2010

MMEZAJI KUWA MMEZWA??? - 2015 ITAWEZEKANA???

Ni yale yale ya mwinda kuwa mwindwa? Na hilo jina la mmezaji limenifurahisha. Hii ni kazi ya Said Michael.

4 comments:

 1. Si kila kimezwacho kina maana na si kila amezae ni wa maana!

  ReplyDelete
 2. Ng'wanambiti - kama kimezwacho hakina maana na mmezaji si wa maana, pengine basi hata kumezana kwao hawa jamaa hakuna maana yo yote na wanatupotezea muda bure tu!

  Au pengine inabidi tuchukulie ile kanuni ya kihisabati kwamba hasi mbili zikigongana eti zinazaa chanya; na kwamba katika kumezana huku ambako kunaweza kuonekana kuwa hakuna maana yo yote ndimo chanya yetu kama taifa imefumbatwa.

  Maoni yako mafupi yanafikirisha. Asante!

  ReplyDelete
 3. Kuna aina fulani ya vyura kule manyara wana sumu kali sana kiasi kwamba hata nyoka huwa wanawakimbia. Sina uhakika kama huyu CHA-DEMU ni chura mwenye sumu ya aina ile...ngoja tusubiri tuone lakini ni wazi joka limeduwaa japo kwa muda tu!

  ReplyDelete
 4. Hili joka siku moja litauliwa tu kwa sababu ya kiburi chake na UZEE. Nobody lives for ever!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU