NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, November 17, 2010

MWALIMU NYERERE ALIWAHI KUULIZA MASWALI MAZITO KUHUSU OFISI HII

Ofisi rasmi ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

************** 

7 comments:

 1. Nasikia ofisi inaulaji sana hii ndio maana Marais wengi Afrika hawataki kuiachia.:-(

  ReplyDelete
 2. Yoweri Museveni ni mmojawapo wa viongozi wasiotaka kuiachia ofisi hii. Sijui kuna nini.

  Mwalimu Nyerere alimkoromea Mzee Rukhsa akitaka kujua biashara iliyoko katika ofisi hii ambayo itamwezesha kurudisha mapesa aliyosemekana kuwa ameyakopa.

  Wengine inasemekana waliitumia ofisi hii kufanyia biashara na wametajirika kweli kweli. Sitaki kujadili watu kwani this office is bigger than people who occupy it. I, however, like the current occupant. Amejitahidi sana!

  ReplyDelete
 3. Ndugu yangu Matondo, Mwalimu alikuwa anauliza maswali wakati majibu alikuwa anayafahamu, cha kushangaza zaidi alikuwa anauliza wananchi ambao katika muda wa ukaaji wake katika ofisi hii hawakujua utendaji wa ofisi hii ukoje kwa vile wakati wa utawala wake uhuru wa vyombo vya kuihabarisha jamii haukuepo na kama ulikuepo ulikuwa una mlengo mmoja tu ambao ni kueleza mazuri tu ambayo yalikuwa yanafanywa katika ofisi na mkaaji wa ofisi hii.
  Nakumbuka wakati nikiwa nasoma shule ya msingi kule kijijini miaka ya 80 ilikuwa ni kama sala baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku kusikiliza hotuba ya mkaaji kwenye ofisi hii kwa vile hakukuwa na ''choice'' ya radio zingine ambazo zilikuwa zinatangaza kwa lugha ya kiswahili Tanzania. Matondo kumbuka msemo usemao mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, kwa hiyo katika mazingira hayo tulijikuta tukiamini kama mkaaji kwenye ofisi hii kila alisemalo ni kweli tu.
  Naamini hata kama Mwalimu hakunufaika na ukaaji kwenye ofisi hii, kuna watu au jamii ambayo ilinufaika sana. Nakumbuka Ndugu yangu Matondo uliishawahi kuleta hoja ukisema je Azimio la Arusha lilichochea rushwa kwa viongozi Tanzania?.
  Ningependa pia kuiuliza jamii ya sasa swali, kama hii ofisi ina matatizo na siyo ya kuikimbilia, Kwa nini alikaa hapo kwa miaka zaidi ya 24 mpaka upepo wa kisiasa na kiuchumi wa mashariki ulipovuma kuelekea upande mwingine ndipo akaamua na yeye kuufuata kwa shingo upande kwa vile hakuwa na ''choice'' na kusema anagh'atuka na siyo kustaafu kwa vile jamii ya kitanzania karibu yote, kwanza ingepigwa na mshangao mkubwa na imani aliyoijenga kwenye jamii kama angesimama jukwaani na kuanza kuhubiri sera na misingi ya kibepari ambayo mpaka kipindi hicho tokea aanze kujishughulisha na siasa alikuwa anazipinga kwa nguvu zake zote na katika mkoba wake alikuwa anatembea na biblia na kitabu cha Azimio la Arusha.
  Nafikili kama isingekuwa huu upepo wa mashariki Mwalimu angeendelea kuwepo kwenye hii ofisi kama kawaida ya wakaaji wa ofisi hii katika nchi za nyingi za kiafrika.(Kenya,Uganda, Zambia,Sudan,Misri,Libya,senegal)nikiendelea kuzitaja itanichukua siku nzima.
  Nampongeza kwa kuleta mtaani msemo wa nagh'atuka badala ya kustaafu.
  Binadamu tumeumbwa siyo wakamilifu, tuna mapungufu kama ilivyodhilika katika biblia(wasoma biblia)Adamu na Hawa(tunda la mti wa katikati). Na Mwalimu naamini alikuwa na mapungufu yake tofauti ni kuwa mazingira kwa wakati wake hayakuruhusu jamii kuyachambua mapungufu yake, sifahamu kama hili lilikuwa ni jambo zuri kwa mstakabali wa nchi, nitawaachia wachambuzi wa maswala ya kisiasa na kiuchumi kutoa kunitolea ufafanuzi.
  Kwa upeo wake sikutegemea kama angeuliza swali kama hili kwa sababu naamini alifahamu tatizo siyo tatizo kwa kila mtu. hii ina maana kuwa, katika jamii yoyote, mazingira ya kisiasa na kiuchumi yanaweza kupunguza ufumukaji wa matatizo na pia yanaweza kurahisisha utatuaji wa matatizo.
  Mwalimu aliiona ofisi hii ina matatizo makubwa kwa sababu mwelekeo wa kisiasa na kiuchumu aliokuwa ameuchagua na kuusimika katika jamii ya Tanzania ulikuwa na matatizo mengi ambayo kila ufumbuzi wa tatizo ulikuwa unazaa tatizo kama siyo matatizo mengine na ndio maana Tanzania aliyoiacha baada ya ''kugh'atuka'' maendeleo yake yalikuwa duni ukilinganisha na raslimali asilia zilizokuepo kwa wakati huo.
  Niataendelea Kumpenda na kumuenzi Mwalimu kwa mazuri aliyolifanyia taifa na nitaendelea kumchukia kwa mabaya aliyolifanyia taifa hata kama siyo kwa makusudi kwa sababu mpaka sasa awamu zote tatu zimeendelea kuyashughulikia ili kuyapatia ufumbuzi.
  Obeja.

  ReplyDelete
 4. Ndugu yangu Matondo, Mwalimu alikuwa anauliza maswali wakati majibu alikuwa anayafahamu, cha kushangaza zaidi alikuwa anauliza wananchi ambao katika muda wa ukaaji wake katika ofisi hii hawakujua utendaji wa ofisi hii ukoje kwa vile wakati wa utawala wake uhuru wa vyombo vya kuihabarisha jamii haukuepo na kama ulikuepo ulikuwa una mlengo mmoja tu ambao ni kueleza mazuri tu ambayo yalikuwa yanafanywa katika ofisi na mkaaji wa ofisi hii.
  Nakumbuka wakati nikiwa nasoma shule ya msingi kule kijijini miaka ya 80 ilikuwa ni kama sala baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku kusikiliza hotuba ya mkaaji kwenye ofisi hii kwa vile hakukuwa na ''choice'' ya radio zingine ambazo zilikuwa zinatangaza kwa lugha ya kiswahili Tanzania. Matondo kumbuka msemo usemao mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, kwa hiyo katika mazingira hayo tulijikuta tukiamini kama mkaaji kwenye ofisi hii kila alisemalo ni kweli tu.
  Naamini hata kama Mwalimu hakunufaika na ukaaji kwenye ofisi hii, kuna watu au jamii ambayo ilinufaika sana. Nakumbuka Ndugu yangu Matondo uliishawahi kuleta hoja ukisema je Azimio la Arusha lilichochea rushwa kwa viongozi Tanzania?.
  Ningependa pia kuiuliza jamii ya sasa swali, kama hii ofisi ina matatizo na siyo ya kuikimbilia, Kwa nini alikaa hapo kwa miaka zaidi ya 24 mpaka upepo wa kisiasa na kiuchumi wa mashariki ulipovuma kuelekea upande mwingine ndipo akaamua na yeye kuufuata kwa shingo upande kwa vile hakuwa na ''choice'' na kusema anagh'atuka na siyo kustaafu kwa vile jamii ya kitanzania karibu yote, kwanza ingepigwa na mshangao mkubwa na imani aliyoijenga kwenye jamii kama angesimama jukwaani na kuanza kuhubiri sera na misingi ya kibepari ambayo mpaka kipindi hicho tokea aanze kujishughulisha na siasa alikuwa anazipinga kwa nguvu zake zote na katika mkoba wake alikuwa anatembea na biblia na kitabu cha Azimio la Arusha.
  Nafikili kama isingekuwa huu upepo wa mashariki Mwalimu angeendelea kuwepo kwenye hii ofisi kama kawaida ya wakaaji wa ofisi hii katika nchi za nyingi za kiafrika.(Kenya,Uganda, Zambia,Sudan,Misri,Libya,senegal)nikiendelea kuzitaja itanichukua siku nzima.
  Nampongeza kwa kuleta mtaani msemo wa nagh'atuka badala ya kustaafu.
  Binadamu tumeumbwa siyo wakamilifu, tuna mapungufu kama ilivyodhilika katika biblia(wasoma biblia)Adamu na Hawa(tunda la mti wa katikati). Na Mwalimu naamini alikuwa na mapungufu yake tofauti ni kuwa mazingira kwa wakati wake hayakuruhusu jamii kuyachambua mapungufu yake, sifahamu kama hili lilikuwa ni jambo zuri kwa mstakabali wa nchi, nitawaachia wachambuzi wa maswala ya kisiasa na kiuchumi kutoa kunitolea ufafanuzi.
  Kwa upeo wake sikutegemea kama angeuliza swali kama hili kwa sababu naamini alifahamu tatizo siyo tatizo kwa kila mtu. hii ina maana kuwa, katika jamii yoyote, mazingira ya kisiasa na kiuchumi yanaweza kupunguza ufumukaji wa matatizo na pia yanaweza kurahisisha utatuaji wa matatizo.
  Mwalimu aliiona ofisi hii ina matatizo makubwa kwa sababu mwelekeo wa kisiasa na kiuchumu aliokuwa ameuchagua na kuusimika katika jamii ya Tanzania ulikuwa na matatizo mengi ambayo kila ufumbuzi wa tatizo ulikuwa unazaa tatizo kama siyo matatizo mengine na ndio maana Tanzania aliyoiacha baada ya ''kugh'atuka'' maendeleo yake yalikuwa duni ukilinganisha na raslimali asilia zilizokuepo kwa wakati huo.
  Niataendelea Kumpenda na kumuenzi Mwalimu kwa mazuri aliyolifanyia taifa na nitaendelea kumchukia kwa mabaya aliyolifanyia taifa hata kama siyo kwa makusudi kwa sababu mpaka sasa awamu zote tatu zimeendelea kuyashughulikia ili kuyapatia ufumbuzi.
  Obeja.

  ReplyDelete
 5. Samahani wasomaji kwa kubandika maoni mara mbili. Hii yote ni matatizo ya kuwa na upeo wa karne ya 20 wakati niko katika karne ya 21.

  ReplyDelete
 6. @Ng'wanaMwamapalala: Huna haja ya kuomba msamaha. Ni jambo la kawaida tu.

  Umetoa uchambuzi wa kina sana kuhusu dhima na nafasi ya Mwalimu Nyerere. Kama mwasisi wa taifa hili na mwanzilishi wa falsafa nyingi zilizoshindwa,ni wazi kwamba anabeba lawama kwani matatizo mengi tunayopambana nayo mpaka leo yaliasisiwa chini ya uangalizi wake. Hata kung'atuka kwake ni kweli kuna maluweluwe kwani inasemekana hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana na ugomvi wake na IMF ulikuwa umefikia pabaya. Hakuwa na mahali pa kukimbilia.

  Kinachowavutia watu wengi ni ule ukweli wake na maisha yake aliyoishi. Miaka 23/24? aliyokaa ikulu ni mingi na kama angetaka kuiba na kujitajirisha angefanya hivyo na hakuna mtu ambaye angemgusa kwani wakati ule yeye ndiye alikuwa mungu mdogo na ye yote aliyedriki kumsaili kwa lolote lile aliishia matatani. Watu wengi wanaguswa sana na ukweli kwamba mbali na miaka yote ile, hakuitumia nafasi hii kujilimbikizia mali yeye na familia yake. Hii inaonyesha kwamba hakuwa ndumilakuwili na aliamini na kutenda kile alichokuwa akikihubiri (Ujamaa na Kujitegemea, Usawa, elimu kwa wote n.k.) - jambo ambalo ni nadra sana kwa wanasiasa.

  Nyerere pia hakuogopa kusema ukweli hata kama ukweli huo ulikuwa unamhusu yeye mwenyewe. Ukisoma kitabu chake cha UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA utaona jinsi alivyoicharukia CCM mbali na ukweli kwamba yeye ndiye alikuwa mwanzilishi wake.

  Kwa maoni yangu mambo haya mawili ndiyo yanampambanua zaidi kuliko wenzake wengi barani Afrika. Kwingineko alifanya makosa mengi tu na baadhi ya siasa zake kusema kweli zilikuwa hazitekelezeki (utopia).

  Waliomfuatia Mwalimu kila mmoja alijaribu kwa kadri yake. Mh. Mwinyi alipewa nchi iliyokuwa inakaribia kusambaratika kiuchumi na yaliyotokea wakati wake tunayajua. Chini yake ilikuwa huru kwa ye yote mwenye meno kung'ata na kumeza mpaka Watanzania wakambatiza 'Mzee Rukhsa". Kama hili ndilo lilifaa kwa wakati ule sijui lakini kuna watu wanaoamini kwamba pengine hali hii ilileta "stability" kidogo na kumfanya atawale kwa urahisi.

  Rais ambaye alifanya kazi kubwa sana katika kuinua uchumi na kuleta nidhamu serikalini ni Mkapa. Japo kuna makosa alifanya (na pengine yamegubika ufanisi wake), naamini kwamba huyu ndiye kiongozi ambaye kweli alifanya kazi ya kuonekana na bora kabisa pengine kuliko wote.

  Mh. Kikwete alikabidhiwa nchi yenye nidhamu kifedha na iliyokuwa inasimama dede kiuchumi. Huyu bado yuko madarakani na tumwache amalize awamu yake kabla ya kuanza kumhukumu. Katika miaka mitano ya mwanzo kwa kiasi kikubwa aliendeleza juhudi zilizokuwa zimeanzishwa na Mkapa. Kama mtangulizi wake kuna makosa yalifanyika ambayo yanatishia kufunika ufanisi wake (mf. suala la ufisadi kwa baadhi ya mawaziri katika serikali yake). Ndiyo tu ameanza awamu yake ya pili na bado anayo nafasi ya kurekebisha makosa yaliyotokea katika kipindi cha kwanza; na kuifanya historia itabasamu.

  ReplyDelete
 7. Mugabe, Museveni, Mobutu na wengineo wengi tu hawakutaka kuiachia ofisi hii...

  Lakini pia kuna Nyerere na Mandela, mifano bora kabisa. Penye giza pia kuna nuru. Kwetu Bongo ofisi hii imepita katika hatua mbalimbali na sasa I believe kwamba imo katika good hands na hali hii tumeisababisha sisi Wabongo wenyewe. Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yameleta msisimko na wote watakaoingia ofisi hii itabidi wawe macho na kufanya kazi kwa bidii sana.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU