NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, November 4, 2010

PENGINE "USHABIKI" WETU WA KISIASA INABIDI UWE HIVI.

 • Nimeiona picha ya huyu mdau hapo juu ikanifikirisha. Ati, ni lazima "tushabikie" chama kimoja tu cha siasa? Vipi kama kile chama kingine ambacho hukipendi kina mgombea anayekukuna na ambaye unaamini kwamba atakuletea maendeleo? Au wakati ambapo chama chako kina sera zingine mbovu ambazo huzipendi na kile chama cha wale wengine kina baadhi ya sera nzuri kabisa katika masuala muhimu kama elimu na maendeleo ya vijijini? 
  • Ndiyo maana Mzee Mustafa Jaffer Sabodo amevutia watu wengi kutokana na ukweli kwamba yeye ni kada wa CCM lakini amejitolea kuvisaidia vyama vya upinzani hasa CHADEMA ili viweze kusimama dede kwani mbali na azima yake ya kuimarisha upinzani, amekiri kwamba sera za CHADEMA zinamvutia. Na huu ndiyo ukomavu wa kisiasa!

  7 comments:

  1. Ushabiki wa kihivyo mgumu kidogo Tanzania kwa kuwa hatuaminiani. Ukiwa CHADEMA ukaonekana unampigia makofi JK kuna watu wataamini wewe ni CCM na CHADEMA umetumwa kuvuruga mambo.Kwa kuwa mpaka sasa na mpaka marafiki wa karibu waaminio Prof Lipumba ni CCM na hata Mrema alivyotoka CCM alikuwa katumwa tu kuvuruga upinzani.

   Lakini naamini kuna hatua fulani imepigwa katika uchaguzi huu.

   ReplyDelete
  2. Demokrasia yetu hii ya kuchakachuana bado inajikongoja. Pengine huko mbele ya safari hili litawezekana. Kwa sasa hukionekana tu kwenye mkutano wa chama cha upinzani basi tayari ushajiharibia. Tutafika tu

   ReplyDelete
  3. Hii nimeipenda, na imekaa vizuri sana huyo jamaa hapo juu kuna mambo mawili:
   Jambo la kwanza huenda yeye anamkubali Kikwete lakini kwa upande wa mbunge anamkubali mbunge wa chadema.

   Jambo la pili huenda yeye ni shabiki tu,kila mkutano yuko na hata hiyo T-shirt ya chagua Kikwete kapewa bure kama shabiki tu,ukimuuliza kampigia nani kura usije kushangaa jibu likawa sikujiandikisha kwa hiyo sina niliempigia.

   ReplyDelete
  4. Kwa inavyoonekana isije ikawa ni wale wanaotupiwa makombo ya hela za ufisadi ili wawe wapambe wa chama cho chote kile. Kuna watu ambao hawana kazi kwa vile uchaguzi umeisha na sasa hawajui wataishije. Anyway, the pic is interesting!

   ReplyDelete
  5. Kamala: Mbona umeshadanganyika tayari? Kalagabaho!

   ReplyDelete
  6. Jambo la msingi ni kugundua kuwa umedanganyika na kukataa kudanganyika tena!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU