NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, November 30, 2010

SAKATA LA SAFARI ZA NJE: OBAMA NAYE AWEKA REKODI YA KUSAFIRI SANA KWA MARAIS WOTE WA MAREKANI. ALALAMIKIWA!

 • Rais wetu alishawahi kulalamikiwa sana kwa safari zake za nje za mara kwa mara. Wapo waliohoji manufaa ya safari hizo kwa taifa hasa ukizingatia kwamba zinatafuna pesa nyingi za walipa kodi. Wachambuzi wengine makini waliona kwamba safari hizo zilikuwa na tija kwa taifa letu. Kutokana na utata huu, Rais mwenyewe aliamua kupunguza idadi ya "wapambe" katika misafara mbalimbali ya viongozi. 
 • Rais Obama naye ameweka rekodi ya kuwa rais anayesafiri sana kwa kipindi alichokaa madarakani. Yeye amevunja rekodi ya kusafiri ya maraisi wote wa nchi hiyo kwa kutumia siku 55 akiwa safarini katika kipindi cha miaka yake miwili aliyokaa madarakani. Rekodi ya mwanzo ilikuwa inashikiliwa na rais George W. Bush (II) aliyetumia siku 54 akiwa safarini nje ya nchi katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ya utawala wake. 
 • Baadhi ya mambo yaliyoibuliwa katika safari hizi za Obama ni pamoja na ukweli kwamba dege lake la Air Force One linatafuna karibu dola 181,000 kwa saa moja!. Hizi ni pesa ambazo zinamtosha Mmarekani wa kawaida kuweza kununua nyumba nzuri ya vyumba vitatu!
 • Inasemekana pia kwamba safari yake ya hivi karibuni aliyoifanya katika nchi za Asia ilikuwa inatafuna karibia dola milioni 200 kwa siku moja. Hiki ni kiasi kikubwa cha pesa hasa katika wakati huu ambapo hali ya uchumi inalegalega kiasi kwamba nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi wote wa serikali imependekezwa kupigwa marufuku.
  • Sitaki kuibua upya mjadala huu lakini nadhani "common sense" inabidi itumike na kutanguliza matakwa ya taifa mbele kwa kuepuka safari ambazo si za lazima. Agizo la rais la kupunguza wapambe katika safari hizi pia ni hatua nzuri sana ya kupunguza gharama. 
  • Malalamiko kuhusu safari za Obama yanapatikana hapa; na kama kawaida malalamiko haya yanatoka kwa wahafidhina wa Fox News.

     4 comments:

     1. nukuu "dola 200 kwa siku moja" (aya ya 4). nina wasiwasi na figure hiyo nadhani kuna 'kaneno' kamerukwa. vinginevyo ni kiasi kidogo sana kwa rais wa marekani.

      my comment: MASIKINI AKIPATA MATAKO HULIA MBWATA

      ReplyDelete
     2. Je atakuwa amevunja rekodi ya Vasco da Gama wa Tanzania Mheshimiwa rais Dr. Kikwete. Watanzania kwa kupamba watu na title. Eti, Mheshimiwa, Rais, Dr.

      Matondo hajanipa jibu hadi leo ni kwanini yeye hapendi kuitwa Dr. au Prof.kama ilivyo jadi kwa watanzania kuwaita watu kwa title zao. Nakumbuka aliwahi kutuonya kutotumia hizi title na kusema atatolea ufafanuzi ni kwanini hapendi kuitwa hivyo. Ni kitambo sana na mimi nasubiri ufafanuzi huo kwa hamu.

      ReplyDelete
     3. @Mwaipopo: Angalizo zuri. Ni kweli kulikuwa na kaneno kalikokuwa kamerukwa na kaneno hako ni MILIONI. Kwa hivyo ilipaswa kusomeka dola milioni 200 kwa siku. Imesharekebishwa na asante sana!

      Hiyo methali yako hiyo nayo...

      @ Matiya - Obama analalamikiwa kwa sababu wapinzani wake wanadai kwamba hizi safari anazofanya hazisaidii cho chote kwani heshima na nguvu za kiuchumi za Kimarekani zimefifia sana duniani.

      Kuhusu watu kupenda "title" nadhani wanasaikolojia na watu wa utambuzi wanaweza kutupa jibu zuri zaidi. Unakumbuka title walizojipa Idd Amin, Bokasa na hata Mobutu? Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini baadhi ya viongozi wetu mpaka wanashutumiwa kwa kughushi vyeti na kujipatia Ph.D za bure ili tu waweze kujipachika title ya u-daktari (wa falsafa)?

      Ndiyo maana nampenda Mwalimu kwani yeye hata Uheshimiwa hakuutaka. Yeye alitaka tu aitwe mwalimu huku akiamini kwamba kiongozi ye yote kimsingi alikuwa ni mwalimu kwa watu wake. Baadaye jamaa wakaibuka na kutaka waitwe waheshimiwa na wakati huo huo falsafa yao elekezi bado ni ile ile ya Ujamaa na Kujitegemea - falsafa ambayo ilitutaka Watanzania tuitane ndugu!

      Hilo swali la pili nitalijibu baadaye lakini mimi naamini kwamba binadamu sie tu wanafunzi wa kudumu hapa duniani (the truly educated never graduate!) na baadhi ya vyeo hivi vinawafanya watu wajione kuwa wameshakifikia kilele cha usomi na maarifa jambo ambalo si kweli.

      ReplyDelete
     4. Vasco da Gama wa Tanzania, dah! Nyie wadau nyie. Mkuu alisema kwamba kama siyo zungukazunguka yake huku na huko mngekuwa mmekufa na njaa.

      Bila Vasco da Gama kugundua njia ya kwenda India si ajabu Ureno na mataifa mengine ya Ulaya yasingeendelea....Kumbukeni hilo. His voyage opened up the whole new world!

      ReplyDelete

     JIANDIKISHE HAPA

     Enter your email address:

     Delivered by FeedBurner

     VITAMBULISHO VYETU