NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, November 6, 2010

TUDUMISHE UTAMADUNI WETU: MH. J.K ALIPOONJA UHONDO WA NGOMA ZA KISUKUMA

 • Wamasai na Watindiga ni mojawapo ya makabila yanayovuma sana kwa kuendelea kudumisha utamaduni wao - japo nayo yananyemelewanyemelewa na utandawazi. Wasukuma nao bado wanajikongoja na mojawapo ya mambo wanayoendelea kuyadumisha ni utamaduni wao wa kucheza ngoma zao za kienyeji.
 • Kule wilayani Bariadi, kwa mfano, kila tarehe 30 mwezi wa tano makundi makuu mawili kinzani ya Bagika na Bagalu hukutana na kushindana usiku mzima na mshindi huamuliwa nyakati za mchana majira ya saa 11 siku inayofuatia. Mashindano haya huvutia watu wengi sana na yamekuwa kama sehemu ya sikukuu kwa Wanyantuzu. Katika mashindano haya mamanju huonyesha ubingwa wao wa madawa na uchawi; na anayeelemewa ndiye hushindwa.
 • Kama mkereketwa wa maswala ya utamaduni, nimefurahi kumwona Mh. J.K. akifurahia ngoma hizi za Kisukuma siku alipotembelea makumbusho ya Wasukuma yaliyoko Bujora jijini Mwanza.  
 • Utamaduni ndiyo utambulisho wetu hapa duniani na mtu asiye na utamaduni wake mwenyewe ni mtu aliyepotea na asiyejielewa. Japo utamaduni wetu umo katika pigano na unatishwa kuangamizwa na utandawazi, inafurahisha sana kuona kwamba baadhi ya vipengele vyake kama hiki cha michezo ya jadi vinazidi kudumishwa. Tusonge mbele.
J.K. akiangalia majina ya Watemi. Picha zote kutoka Blogu ya Ikulu.

*****...******

Msikilize Ng'wanakanundo hapa chini, manju mashuhuri wa Kisukuma kutoka Mwanza.3 comments:

 1. Nimeziangalia hizi picha vizuri na kama mtaalamu wa Saikolojia nimebakia na swali moja kubwa sana: Mbona Mheshimiwa hapigi ngoma zile ndogo? Naona amelishupalia lile lingoma likubwa tu, kwa nini?

  Wasukuma nanyi kweli mna mambo!

  ReplyDelete
 2. Kwa mtazamo wa Psychoanalysis (Sigmund Freud), JK kung'ang'ania kupiga lingoma likubwa inawezekana anahusudisha sana wanawake wanene au wenye mat*** makubwa. Angalieni wapenzi zake halafu mniambie.

  Lakini pia yawezekana ni ile ego: Yeye ni Mkuu wa nchi na kwa hivyo ni lazima apige lingoma likubwa. Mwenye analysis nyingine aseme but I think I am right!

  Hongera rais wetu mpendwa kwa kuchaguliwa tena. Usisikilize maneno ya watu. Unayo miaka mitano zaidi ya kujenga legacy ya nguvu. Ongeza vita dhidi ya ufisadi na imarisha maslahi ya watu wa kawaida. Cha muhimu zaidi usimruhusu huyu mhuni aitwa=ye Slaa kuharibu amani ya nchi. Ikibidi muweke ndani ajifunze siasa. We wabt peace in our country!!!

  ReplyDelete
 3. "Ngoma kubwa na mat... makubwa!!!!" Yaleyale ya jina la blog "Chakula kitamu na kichungu..." kufananishwa na ngono! Kazi ipo!!!! Sorry Kalume Kenge. Mie ni mtani wako, dont worry. Ila natamani uniambie kwa kirefu kanuni za Freud. Serious mtani.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU