NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, November 3, 2010

TUSIPOKUWA MAKINI NCHI INAWEZA KUINGIA MATATANI...

 • Wakati ule tulikuwa na Mwalimu Nyerere ambaye, kulingana na "uzito" wake katika jamii, aliweza kutuepusha na misukosuko mingi, tukasonga mbele na kuendelea kuishi kwa amani. Mzee yule alifikia hata kuwatungia watu vitabu alipoona kwamba nchi ilikuwa inapelekwa ndiko siko. Na mara nyingi hakuogopa kukikemea chama alichokianzisha yeye mwenyewe - tena kwa maneno makali kabisa. Nyerere pengine alikuwa ndiye mtu pekee ambaye angeweza kusimama juu ya kichuguu akapaza sauti na Watanzania wote tukakaa kimya na kumsikiliza tena bila kujali itikadi zetu za kisiasa.
 • Leo hii nchi yetu inapita katika kipindi kipya na muhimu cha utanuzi wa demokrasia na kwa upande wangu sioni "kichwa cha busara" ambacho kinaweza kuchukua nafasi iliyoachwa na Mwalimu Nyerere, kichwa ambacho kinaweza kusimama, kikajitoa katika kunguku la ushabiki wa kisiasa, kikaweka maslahi ya taifa mbele na kurekebisha mambo. 
 • Kuna kutojali kwingi. Kuna kujiamini kupita kiasi kwingi. Kuna kudharau kwingi. Kuna kiburi kingi. Kuna kulewa madaraka kwingi. Kuna kuchemka kwingi. Kuna ....Na hali hii hasa katika mazingira tuliyonayo sasa ambapo watu wamo katika jazba kutokana na uchaguzi huu wa Kihistoria, si nzuri. 
 • Ati, kama kweli Dr. Slaa atayakataa matokeo ya uchaguzi wa uraisi kwa madai kwamba "yamechakachuliwa", nini kitatokea? Ni kichwa gani cha busara kitakachoweza kusimama, kikakemea na kuwatuliza Watanzania katika moto huu wa kisiasa unaowaka? Hiki ndicho kinachonitia wasiwasi. Mungu Aibariki nchi yetu ili, pamoja na matatizo yetu yote, angalau tuweze kuendeleza amani tuliyonayo, amani ambayo  nadhani tunaichukulia "for granted". 
 • Na kama nilivyowahi kusema hapa , mfumuko wa matabaka kati ya wale wanaoshindia mlo mmoja (ambao ndiyo wengi) na wale wachache wanaomwaga viporo majalalani umewasha moto unaotokota chini kwa chini. Pengine matokeo ya uchaguzi huu na jazba hizi tunazoziona ni ishara hafifu tu za moto huu. Tufanye nini?
  *******.......*******

   Sitayatambua Matokeo ya Urais - Dk. Slaa

  MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

  Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

  "Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa.

  Chanzo: Mwananchi. Tazama pia hapa.

10 comments:

 1. huyo umwitaye Munga ashatubariki, unahitaji baraka gani tena>??? najiuliza

  tuna wasomi kama wewe, hii sio baraka?? ila sasa mnakaa pembeni tena ughaibuni wakati watu wasio na uwezo wanaendelea kututawala sisi! acha kumlilia Mungu, take action

  ReplyDelete
 2. Nakumbuka uchaguzi wa mwaka jana, watu walilalamika, wakafnya waliyofanya wakaitwa `wakorofi' Leo hii natuma hata wale waliokuwa nyuma ya kutoa kauli hiyo ya `ukorofi' wamejionea!
  Swali ni je ifanyike nini ili `ukorofi' huo usionekane, watu waridhike ....natuma ipo njia hata ikibidi kuomba misaada nje kwa ajili ya hili tutapata!
  Swali ni je `nani wa kumvika paka kengele', kwasababu leo wewe ukipata utawaona wengine wakorofi ukikosa lazima utalalamika!
  Haki , haki , haki ipo wapi na ili haki iwepo ifanyike nini?

  ReplyDelete
 3. @ Kamala. Sijui kwa nini nahisi kama vile hukuelewa (au pengine ume-ignore) nilichokuwa najaribu kusema hapa.

  Kukaa ughaibuni si tatizo na ndiyo maana wengine tulianzisha hizi blog ili nasi tuweze kushiriki katika ujenzi wa jamii yetu kwa ukaribu zaidi. Huoni kwamba huu nao ni mchango mkubwa?

  @ emu-three. Angalizo zuri. Unaposema "tuombe misaada nje" unamaanisha nini? Tuombe misaada ya nini? Watu kutoka nje waje kutuimarishia demokrasia yetu? Ukifafanua nitachangia mjadala vizuri zaidi. Asanteni.

  ReplyDelete
 4. ndio, tuombe msaada kwenu mlioko nje, na ninasema hivi< nyie mje nanyi muingie kwenye nafasi za maamuzi na sio kuanzisha blogu za kuwasema wafanya maamuzi tu, au??

  ReplyDelete
 5. Kamala: Nyinyi mlioko huko mmeingia kwenye maamuzi? Kama hammo, ni kipi kinachokufanya uamini kwamba sisi tukirudi tutapewa nafasi ya kuingia kwenye maamuzi?

  Sote hatuwezi kuwa katika nafasi za kufanya maamuzi. Tunachopigania ni kwa wale tuliowapa nafasi za kufanya maamuzi basi wawe wanafanya maamuzi ya busara na yenye kuzingatia na kutunufaisha sote. Na hili ni jukumu la kila mmoja wetu - awe ndani au ughaibuni haijalishi!

  ReplyDelete
 6. Slaa ni BOMU! What makes him think that ni lazima awe rais. Hata kama kura zimechakachuliwa so what? Aondoke zake asije akatuletea vita sisi.

  Na kwa msisamamo wake huu wa kipuuzi basi ajue ameshajiharibia na safari nyingine akigombea hata ubunge hataupata. Padri Mpora wake za watu hana hata aibu.

  ReplyDelete
 7. DK SLAA = MZINZI = DISAPPOINTMENT.

  As far as I am concerned, HE IS DONE!!!!

  ReplyDelete
 8. Karumekenga na anonymous kama tutaangalia rekodi za uzinzi wa mtu basi mteule wenu ndiye shehe mkuu wa wazinzi acha mbali huyo padri. Je nyie ni salama kuhusiana na tuhuma hizi? Isije kuwa nyinyi ni wasenge wa kawaida tu.

  ReplyDelete
 9. Wa anony. wa mwisho. Ndiyo upuuzi wenu watu wa CHADEMA. Kwa matusi na vitisho hamjambo. Please msituletee upuuzi wenu wa kwenye Jamii Froums hapa.

  Mmekazana Slaa Slaa for what. Tabia za kitoto mpaka anazira kuja kusikiliza matokeo ya urais. Mnashabikia haya mambo and I have a sense kwamba wengi wenu hamjasikia hata AK 47 inavyounguruma. Shabikieni tu huo upuuzi wa Slaa wenu wa kukataa matokeo lakini I hope mna ndugu zenu wanawake na watoto. AK 47 huwa hazichagui CHADEMA wala CCM. Kumbukeni hili mnaporoka na jazba zenu na huyu padri wenu mzinzi!

  ReplyDelete
 10. Hebu tufike mahali tukubaliane na matokeo kwani ni lazima kuwa Rais? hata kura zirudiwe kesho JAKAYA KIKWETE atashinda, tuliambiwa kuna m-lori (Container) hivi kweli ukishakuwa msemaji utasema bila kuhalalisha, kura zimepigwa za kwenye mitandao, JK hayumo sasa tumepiga wa-TZ wote nawaombeni yaishe sio mpaka anayetukanwa akasirike, kila mtu akashike jembe (ustaarabu wake) tukutane 2015 tafadhali Dr Matondo waelimishe wa TZ hata wa- USA, UK wanaridhika tuwe waungwana.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU