NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, November 24, 2010

UTAFITI: HABARI NJEMA KUHUSU MAPAMBANO DHIDI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI


Picha hii inapatikana hapa
 • Watafiti, madaktari, wanaharakati na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI "wanashangilia" baada ya utafiti mkubwa mpya uliochapishwa katika jarida maarufu la tiba la New England Journal of Medicine kuonyesha kwamba watu wanaokunywa dawa iitwayo Truvada ambayo ni mojawapo ya madawa ya kuongoza nguvu kwa watu walioathirika na UKIMWI inaweza kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa asilimia 44 kwa wanaume mashoga wanaofanya ngono bila kutumia kondomu.
 • Na kama dawa hii ikitumiwa kwa uangalifu kila siku (yaani bila kukosa hata siku moja) basi inaweza kupunguza uwekezano wa kuambukizwa UKIMWI kwa asilimia 90! Washiriki katika utafiti huu walikuwa ni wanaume mashoga kutoka katika nchi sita - Brazil, Ecuador, Peru, Afrika Kusini, Thailand na Marekani. 
 • Cha kufurahisha zaidi ni kwamba Truvada ambayo ni mchanganyiko wa madawa mawili yanayozuia virusi vya UKIMWI kuzaliana yaani Tenofovir na Emtricitabine tayari inapatikana katika nchi nyingi duniani. Hapa Marekani dawa hii hutengenezwa na kampuni la madawa la Gilead Sciences na inaweza kugharibu kati ya dola 12,000 na 14,000 kwa mwaka. Katika nchi masikini ambako ndiko kuna maambukizi mengi ya UKIMWI dawa hii inaweza kupatika kwa bei ya senti 40 (dola za Kimarekani) kwa kila kidonge. 
Vidonge vya Truvada
  • Truvada bado ni ghali sana hasa katika nchi masikini kama zile za Afrika na swali kubwa linaloulizwa ni kuhusu gharama kubwa za dawa hii hasa ukizingatia kwamba kati ya wagonjwa wa UKIMWI wanaokadiriwa kuwa milioni 33 duniani kote ni milioni 5 tu ndiyo wanatumia madawa ya kuongeza nguvu.
  • Mbali na matokeo haya ya kutia moyo, watafiti hawa wanaonya kwamba huu si wakati wa kuacha kutumia kondomu na kuzingatia mbinu zingine za kujikinga na maambukizi ya UKIMWI. 
  • Makala kuhusu utafiti huu yanapatikana hapa, na ikisiri (abstract) ya utafiti huu kama ilivyochapishwa katika jarida la New England Journal of Medicine inapatikana hapa.

  3 comments:

  1. Kweli hizi ni habari nzuri, lakini tuendelee kuwa waangalifu. Isitoshe hii dawa ni ghali sana. Wangapi wanaweza kujigharamia?

   ReplyDelete
  2. Kweli ni habari nzuri, lakini ni kama kujaribu kibiri kuwa kinawaka ndani ya pipa la petrol!!!

   ReplyDelete
  3. Ukweli bado uko pale pale kwamba UKIMWI hauna tiba wala kinga - unless otherwise stated. This is good news lakini we have to remain diligent and upbeat. Ni no sex au kondomu kwa sana!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU