NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, November 20, 2010

UTAFITI: JOTO LA LAPTOP LINAUNGUZA KORODANI NA HIVYO KUHARIBU RUTUBA YA MBEGU ZA KIUME.

 • Je, wewe ni mwanaume? Unayo tabia ya kutumia laptop yako ikiwa mapajani mwako? Pengine itabidi uache tabia hiyo mara moja kwani unaweza ukawa unaangamiza kizazi kijacho. 
 • Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la Fertility and Sterility unaonyesha kwamba joto la laptop ni hatari kwa sababu linaunguza korodani na hatimaye kuharibu na hata kuangamiza kabisa mbegu za kiume. Joto hilo limetajwa kuwa sababu mojawapo inayosababisha kuongezeka kwa utasa katika nchi zilizoendelea. 
 • Mbegu za kiume zilizoathiriwa na joto la laptop hazina vichwa, hazina mikia na zingine zina mikia mifupi; na kwa hivyo haziwezi kuogoelea na kulifikia yai la mwanamke ili kuweza kulirutubisha. Kwa ujumla, joto la laptop linaweza kusababisha utasa wa kudumu kwa wanaume. 
Ni mwogeleaji mmoja tu hodari ndiye atashinda hapa...
  • Ushauri wa watalaamu: Kama ni lazima uweke laptop yako mapajani, basi panua miguu yako. Hii inasaidia korodani zisiunguzwe na joto la laptop kwa haraka. Njia ya uhakika zaidi ni kutumia dawati au meza kila unapotumia laptop. Utafiti huu unapatikana hapa na hapa.

  6 comments:

  1. mmesikia mwenye tabia hii acheni au fuateni ushauri uliotolewa....

   ReplyDelete
  2. Tafiti nyingine ni TISHA TOTO!

   Ukifuatilia utapata BERIBERI

   Na ukifuatilia utasikia tafiti inayoshauri usitumie simu,....

   ----wakati nyingine inakwambia akchwali simu poa!

   Nyingine ikakuambia Tumia mboga mboga,....
   ....wakati nyingine inakuambia usipotumia RED meat utaathirika.

   Nyingine inakuambia usimchape mtoto katika kumfundisha,....
   ....na nyingine inakuambia mpaka ni kwanini siku hizi MAREKANI ni wazembe ni bikozi zeispeadi ze rod kwa WATOTOZ.

   Nyingine ina kuambia bomba mwanamme awe na mwanamke mmoja,....

   ....na nyingine inakuambia kwanini waliotukuzwa na MUNGu kwenye BIBLIA hata pia KORANI kama akina ABRAHAMU , King DAVID, KING SOLOMON,... MOHAMED .... hawakuwa na mwanamke mmoja na ndio maana husikii malalamiko ya wake zao.

   Kuna mpaka tafiti idaiyo Dr Slaa alishinda,...

   ....na kuna ikuambiayo Dr KIKWETE kwa uhendsamu tu ANGESHINDA hasa kura za wanawake wote na kupata Urais kwakuwa eti Dr Slaa na Dr KIKWETE wakimendea raisi kukubaliwa ni Dr Jakaya.

   Hapo ndipo jiulize pia NI NANI anatafiti na MADHUMUNI YAKE ni nini,...

   .... kwa kuwa WATAFITI wengi katika kutafiti hata bila WAO WENYEWE kujua ,....


   ....wafanyacho ni kutaka kuhalalisha waaminicho TAYARI kwa hiyo kama MIYE ni Muislamu ,....


   ....ni kifanya utafiti wa dini gani kati ya UKRISTO na UISLAMU ndiyo itapeleka watu MBINGUNI,...

   .... kirahisi CONCLUSION itakuwa ni dini yangu ya KIISLAMU ndiyo yenye bonge la haiwei ya kwenda kwa Sir GOD.:-(

   Kwa hiyo kuhusu hiii au zile zidaizo sijui ukifanyaje toto lako la kiume litakua SENGE,...
   .... mimi siziamini mpaka nitafiti mwenyewe.

   Kwa kihivyo nakiri miye TOMASO na ingebidi Yesu anionyeshe makovu ya kupigiliwa MSALABANI niamini hakukuwa na STUNT double.:-(   Samahani kwa KUPAYUKA hapa katika kijiwe MWANANA cha Mkuu MATONDO!:-(

   ReplyDelete
  3. @Mtakatifu;

   Nimekupata vizuri sana. Hata mimi huwa nazikoromea tafiti nyingi tu hasa hizi zinazohusu lishe. Leo kula hiki, kesho usile hiki, leo fanya hivi, kesho usifanye hivi n.k. Tafiti nyingi huwa zinashindwa kuzingatia mazingira ya Kiafrika hasa kuhusu mambo ya vyakula; na mengineyo. Ndiyo maana mimi na Dr. Chib tiliwahi kumkoromea Yasinta alipoleta utafiti unaosema eti Chai inapunguza mshtuko wa moyo (tazama link hapa chini):

   https://www.blogger.com/comment.g?blogID=3332600689383679139&postID=7343994074813027234


   Kwa hili la joto la laptop nimelifikiria vizuri na nikaona kwamba pengine lina uwezekano mkubwa wa kumuathiri mtu ye yote bila kujali mazingira na athari nyinginezo.

   Lakini pia inawezekana kwamba korodani za Waafrika zinavumilia joto kali kwani tumezoea kushinda juani na kwa hivyo hili joto la mnunurisho wa laptop halifui dafu. Tutalijua hili tukifanya utafiti wetu wenyewe.

   Hivi karibuni kulikuwa na utafiti Tanzania (uliripotiwa kwa Michuzi na Mjengwa kama sikosei) ambao unaonyesha kwamba "rutuba" ya mbegu za wanaume wa Kibongo inapungua kwa kasi. Wadau wengi walilaumu unywaji wa bia na kuendekeza maisha ya deko. Pengine kunaweza kukawa na sababu zingine kama hizi za joto la kompyuta hasa kwa wakazi wa mjini kama Dar ambako utafiti huo ulifanywa.

   Japo kwetu ni watu wachache sana wenye laptop si vibaya tukianza kujua madhara yake - hasa kwa vijana ambao wanashinda wamezipakata kwani wanaweza kuwa wanakaanga mbegu za kizazi kijacho.

   ReplyDelete
  4. Mhh, lakini wahenga wansema `lisemwalo lipo, kama hlipo laja. Chukua mfani unawasha TV, wakati inawaka weka mkono wako kwenye uso wa TV, kuna kitu unahisi...hii ni mionzi, kama sikosei, je ile mionzi haiathiri...sijui, mimi sio mtafiti, msininukuu!
   Ila kama inawezekana kuchukua tahadhari ni bore kwani wanaseme wapare
   `USINITI NANGA, UNETI KEBA..(Usiposema `eheri ningeli, utasema afadhali nime...' kitu kama hicho!

   ReplyDelete
  5. eeeeh basi mie nguvu zote kwishney coz miaka kibao naweka hapo laptop duh.

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU