NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, November 15, 2010

ZOFA AIBUKA KIDEDEA KATIKA UANDISHI WA INSHA JUU YA SIKU YA MASHUJAA

 • Walimu wake wamevutiwa sana na insha hii ya binti yenu Zofa (Darasa la kwanza) na wamesema itachapishwa na kuwekwa katika kitabu chao cha kumbukumbu kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza darasa la mwaka 2010. Watoto hawa hawakupewa maandalizi yo yote. Waliambiwa tu wakasikilize vizuri kilichokuwa kinaendelea katika maonyesho ya kusherehekea siku ya mashujaa yaliyokuwa yameandaliwa na wenzao wa darasa la nne halafu waje waandike insha juu ya kile walichojifunza. Hongera Zofa!!!
 • Kama unavyoweza kuona, japo kuna makosa ya kisarufi na uandishi, walimu hawakuyagusa. Ni makosa ambayo yanaruhusiwa kwa sasa na watoto hawa wa darasa la kwanza hawapaswi kukosolewa kwa kila kitu. Katika hili (nami nikiwa mwalimu), nimejifunza kitu!

10 comments:

 1. Habari nzuri sana, na natoa hongera sana. Ni mwanzo mzuri, na dalili ya mvua ni mawingu. Sijui kama nyinyi wazazi ni Wagaalu au Wagiika, lakini naona mtoto anafuata nyayo :-)

  ReplyDelete
 2. She is going to be a powerful writer with no fear to express her mind, that's what I see and that piece of writing is amazing!

  Many congrats to her! :-)

  ReplyDelete
 3. Hongera Zofa.Yote haya yanatokana na msingi mzuri kuanzia kwa wazazi na mazingira ya mazuri ya shuleni pia. Hata mtoto wa darasa la saba katika shule zetu za Tanzania sidhani kama anaweza kuandika insha iliyotulia kama hii tena kwa lugha ya kiingereza. Wasiwasi wangu ni kwamba hata baadhi ya walimu wa shule ya msingi hawataweza kushindana na Zofa.

  ReplyDelete
 4. kwenda zako huo kwakuwa wamesomea nje ndo mana na elimu sio duni ndo mana wewe malkiory unayelinganisha huyo kinda na mwalimu wa primary akili zako ziko kwapani pole sana ila ukukmbke huyo mwalimu wa primary ndo alikutoa wewe ujinga wa kusoma na kuandika

  ReplyDelete
 5. Well done shangazi, i'm proud of you....huo ni mwanzo mzuri kama alivyosema Candy!hapo kichwa kinachakachuwa kweli kweli!wabongo kwa vijimambo mmmh!sasa haka kamsemo kameenea kweli,kazana shangazi nyinyi ndio mtakuwa viongozi wa baadae.

  Hongera pia kwa wazazi.

  ReplyDelete
 6. Dr.Matondo. Leteni ujuzi mliojifunza huko nje kuhusu elimu uje utusaidie. Hatuwezi kuendelea bila elimu bora na mawazo yenu mliyojifunza huko nje yanahitajika sana. Nikiwa rais mwaka 2015 nitawarudisha walimu wa universities, doctors and engineers mliotokomea. Rudini jamani tuje tusaidiane kuimarisha elimu ya nchi yetu.

  ReplyDelete
 7. Shangazi kutoka NorwayNovember 15, 2010 at 7:39 PM

  Inafurahisha sana! Hongera nyingi kwa Zofa. Kuna msemo flani wa kiswahili, hau sound vizuri (na hivyo sitauandika hapa) lakini kweli ule msemo una maana nzuri tu. Kwa sasa nnachoweza kusema tu ni.."as father as daughter...!"

  Kwa mara nyingine, naomba umhongereshe kabisa Zofa. Pengine umpe zawadi (motivation)????

  ReplyDelete
 8. Asanteni wapendwa;

  Jambo moja ambalo nimejifunza ni kwamba ili mtoto afanikiwe hapa - hata kama awe na akili namna gani - ni lazima mzazi uhangaike sana. Kuna homework za kufanya pamoja kila siku jioni, kuna hadithi za kusoma pamoja kila siku, kuna mazoezi kutoka vitabu vya kiada yanayopaswa kufanywa pamoja, kuna kujitolea shuleni, kuna kushiriki katika michezo ya mtoto n.k. Siyo kama nyumbani ambako watoto wanajiendesha wenyewe hasa enzi zetu. Na kwa vile hapa hakuna cha mjomba wala shangazi, basi ni wewe mzazi na mtoto wako. Mbali na kwamba hali hii inachosha lakini inajenga ukaribu na urafiki sana kati ya mzazi na mtoto. Na jambo hili lina faida nyingi sana - kimwili na kisaikolojia!

  ReplyDelete
 9. Safi sana shangazi yangu, endelea hivyo hivyo au zaidi.

  ReplyDelete
 10. Matondo bado watoto wako wana majina ya kizungu wakati wewe ni mwalimu wa lingustic kama kweli unaipenda Tz wape majina ya kisukuma na tuone kama watafukuzwa shule km Mwanamayu, Kashinde Chausiku, Asha, n.k

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU