NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, December 7, 2010

ASILIMIA 90 YA WATANZANIA HAWAKOPESHEKI - WASSIRA

"Asilimia 90 ya Watanzania Hawakopesheki" 
Patricia Kimelemeta

ZAIDI ya asilimia 90 ya Watanzania wanafanyakazi kazi zisizo rasmi, jambo linalowakwamisha wengi wao katika kupata  mikopo kutoka katika mifuko ya uwezeshaji, ili kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Utaribu), Stephen Wassira alipotembelea, ofisi ya Mpango wa Kurasimisha Rasiliamali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita).

Wassira alisema lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawezeshwa ili kuondokana na umaskini.

Alisema uwezeshaji huo wa wananchi ni pamoja na kuwajengea mazingira ya kupata mikopo kutoka katika mifuko mbalimbali ya uwezeshaji ili hatimaye, wawe na mitaji ya kufanya shughuli za kiuchumi.

Alisema hata hivyo wananchi, wamekuwa wakishindwa kufanikia malengo ya kupata mikopo na kwamba hiyo inachangiwa na tatizo la kutokuwa na shughuli rasmi.

Alisema kutokana na hali hiyo, Mkurabita imejikita kuwawezesha wananchi kwa kurasimisha mali walizonazo ili waweze kupata mikopo ambayo wanaaamini kuwa itawasaidia kupambana na umaskini.

"Tatizo letu ni kwamba zaidi ya asilimia 90 ya Wananchi wanafanyakazi katika sekta zisizo rasmi na vipato vyao ni vidogo, ikilinganishwa na wachache wenye vipato vya juu na ambao wanaweza kutumia fursa hizo kujipatia mikopo kwa urahisi," alisema Wassira.

Waziri huyo alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, Mkurabita itajipanga na kushirikiana na wadau wakiwemo wabunge na madiwani ili kutoa elimu kwa wananchi, kuhusu namna ya kurasimisha rasilimali zao ili ziwasaidia kupata mikopo.

Kauli hiyo ya waziri, imekuja huku kukiwa na malalamiko kuwa Mkurabita, haujaleta manufaa makubwa hasa kwa wananchi wa maeneo ya vijijini.

Inadaiwa kuwa hata katika maeneo ya mijini, ni watu wachache mno walionufaika na mpango huo ambao sasa unaingia katika awamu ya pili ya utekelezaji wake.
Chanzo: Mwananchi
********** 

Safari Yetu Bado ni Ndefu!

1 comment:

  1. Watakopesheka vipi wakati mmewadidimiza kwenye umasikini. Nawe Tyson hiyo sura duh!

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU