NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, December 22, 2010

BAADA YA MIAKA 1O YA NDOA, HATIMAYE LEO NIMEPATA MAUA WARIDI KWA MARA YA KWANZA. KULIKONI ???

(1) Ati, kipi ni bora? Maua waridi (Roses) au mchicha ili tuje tule wote?


(2) Ati, kulikoni ??? Kwa nini maua baada ya miaka 10 ya ndoa? Na Wanaume twaruhusiwa kuhoji kama huyu mke wa Hagar the Horrible hapa chini?


(3) Au pengine tusome na kuzingatia 1 Wakorintho 13:4 - 8


4. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5. haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6. haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7. huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8. Upendo haupungui neno wakati wo wote...

*************
Asante sana mama watoto wangu mpendwa. Asante kwa kunishangaza namna hii. Asante sana kwa wema wako usio na kikomo. Asante kwa kuwa rafiki yangu wa kweli. Asante kwa kila kitu. Mungu Aendelee kutubariki katika safari yetu hii tunayosafiri pamoja hapa duniani!!!

*************

Acheni nifurahie maua yangu mimi...tena na Noeli juu!!!

12 comments:

  1. Huhitaji kushangaa ila kurudisha upendo mara dufu kwa mkeo. Japokuwa utamaduni wa maua kwa wengine huonekana ni wa kigeni na kuuiga. Kinachojalisha hapa ni kitu gani psychological ulikifikiria mara baada ya kupewa maua hayo.

    Mimi ni mmoja wa wale ambao hata mtu akinikabidhi ekari ya bustani ya maua waridi hakuna mshipa wowote utakaonicheza. Lakini kwakuwa mwenza wangu anajua kipi ninachoamini basi kazi kwake kunishangaza kwa lolote lakini si kwa maua. Si ulisikia wale maarusi waliopeana roses 9,999.... mwenza alifurahi sana lakini kwa mwingine huo ni ufujaji wa pesa.

    Yote kwa yote mkeo kakupa alichoamini hata wewe utakifurahia miaka 10 ya ndoa si mchezo. Ndoa nyingine huvunjika usiku wa honey moon. CONGRATULATION

    ReplyDelete
  2. Hongera Mkuu! Miaka kumi ya ndoa si mchezo!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Matondo kwa kutuelimisha kupitia mahusiano ndani ya familia yako

    ReplyDelete
  4. duhu bila shaka ushakuwa fundi na msanii wa kutosha kama wewe ni mwaminifu! ua ukiliangalia kisayansi au kikemia ni jitu tu lipo, lakini ukiliangalia iupendo ni zuri, ni waridi au lini fragilance

    ReplyDelete
  5. Ni kama mwaka mmoja vile! lakini nami nasema hongera. labda mnamo mwaka fulani nikiolewa na mie nitatimiza miaka 10 kama wewe...LOL

    ReplyDelete
  6. Hongereni kwa kuadhimisha miaka 10 ya ndoa yenu.

    ReplyDelete
  7. Mwl. Matondo hongera kwa kutimiza miaka kumi katika ndoa. Pia nakutakieni Xmas njema na heri ya mwaka mpya hasa kipindi hiki unapoadhimisha adhimisho hili takatifu.Mungu awawezeshe muadhimishe hata miaka 80 ya ndoa. Kila la heri.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana kaka Matondo. Mumejitahidi sana miaka kumi! Wengi wanakuwa wameshaachana baada ya muda mdogo tuu kwenye ndoa. Au sio marafiki tena wanalea watoto tuu ndani ya ndoa na kufanya yao nje. Ndoa ni kitu cha muhimu tunachosalia mara kwa mara na kufunga ili Mungu atubarikie ndoa hapa ulimwenguni.
    Kupata maua ni symbol nzuri sana kwamba bado mnaheshimiana na kujaliana katika ndoa yenu.

    ReplyDelete
  9. Wapendwa wetu;

    Asanteni sana kwa shukrani zenu. Ndoa ni mtihani mgumu na miaka 10 iliyopita imekuwa yenye mafunzo, mafanikio na zaidi ya yote Furaha na Matumaini yasiyopimika. Naamini kwamba binti huyu mrembo wa Kichagga ndiye niliyeandikiwa na naamini kabisa kwa asilimia 100 kwamba upendo wetu huu uliovumilia mengi utadumu daima. Lengo letu ni kuvilea vibinti vyetu hivi mpaka viweze kusimama dede na kuukabili ulimwengu.

    Wapendwa, tuko pamoja na asanteni sana kwa sala na maombi yenu!!!

    ReplyDelete
  10. Seba agutongele!
    Hongera sana rafiki yangu. Nimefurahishwa sana unavyohabarisha na kuelimisha kupitia blog yako.Lakini kilichonigusa zaidi ni hii miaka kumi ya ndoa yako takatifu na picha ulipiga na mama yako mzazi, siendelei zaidi maana historia inanikumbusha Makutopora.

    Siku nyingine ukija bariadi ufika na Mwanza maana barabara kutoka bariadi hadi mwanza si muda mrefu itakuwa lami

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU