NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, December 13, 2010

CHADEMA KUNAFUKA MOSHI ???


ZITTO AWATIKISA CHADEMA
 (Sunday, 12 December 2010)

Na Boniface Meena

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeunda jopo la wazee wa chama hicho, litakalosikiliza maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, kuhusu mgogoro kati yake na viongozi wenzake ndani ya chama.Imeelezwa kuwa kamati hiyo pia imemtambua rasmi Rais Jakaya Kikwete kuwa ni kiongozi halali na imewaagiza wabunge wa chama hicho, kushiriki katika shughuli zote za kitaifa.

Jopo hilo la wazee hao wa Chadema, litaongozwa na Profesa, Mwesiga Baregu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kupitia tiketi ya Chadema, amekuwa katika mvutano na viongozi wenzake ndani ya Chadema, tangu alipopinga hatua ya wabunge wa chama hicho, kususia hotuba ya Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa Bunge la Kumi, uliofanyika mwezi uliopita mijini Dodoma mwaka huu.

Akizungumzia kukutana na Zitto, Profesa Baregu alisema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa Zitto ni kiongozi wa chama na anahitaji kusikilizwa.

Alisema jopo hilo alikataloliongoza yeye, linawashirikisha pia mzee Nyangaki Shilungushela, Dk Kitila Mkumbo na Shida Salum ambaye ni mama yake Zitto.

"Tunazungumza ndani ya chama, ili kujenga maelewano na kuweka mambo sawa,"alisema Baregu.

Alipoulizwa kuhusu msimamo wa kamati kuu kumtambua Rais Kikwete, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa hakutaka kuzungumzia hilo na badala yake, alitaka lisubiriwe tamko rasmi la chama litakalotolewa kesho.

"Nani kasema hivyo, ni vizuri kwa gazeti makini kama Mwananchi mkasubiri taarifa kamili, itatolewa,"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema ni vizuri kusubiriwa tamko hilo ambalo alisema litatolewa katika mkutano wa waandishi wa habari.

"Sipendi muandike taarifa zisizo rasmi ningependa usubiri hadi keshokutwa (kesho). Kutakuwa na 'press conference (mkutano wa waandishi wa habari)," alisema Dk Slaa ambaye katika uchaguzi mkuu uliopita, alikuwa mpinzani wa karibu wa Rais Kikwete.

Juzi, Kamati ya Wabunge wa Chadema, ilimvua Zitto wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, lakini chama hicho 'kikapigwa jeki' baada ya mfanyabiashara maarufu, Mustafa Sabodo kukipa Sh150 milioni kwa ajili ya kujenga chuo cha maadili ya uongozi.

Matukio hayo mawili pia yaliambatana na kuugua ghafla kwa Zitto na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Amur Arfi, ambao walilazwa katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, kwa matatizo tofauti.

Katika siku hiyo Zitto, alipigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, hatua iliyofanywa na wabunge wa chama hicho katika mkutano wao uliofanyika mjini Bagamoyo, Pwani.

Wabunge hao pia walimtaka Zitto ajieleze kufuatia kitendo chake cha kupinga uamuzi wa pamoja wa kususia hotuba ya Rais Kikwete.

Uamuzi wa wabunge hao kumvua uongozi, ulikuwa ukitarajiwa na wengi baada ya Zitto kupinga hadharani kitendo cha wenzake, kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais, alipoanza kuhutubia.

Hatua hiyo ilikuwa na lengo la wabunge hao kuonyesha kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais,kushinikiza kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Uamuzi wa wabunge hao kususia hotuba ya Rais Kikwete, ulifikiwa baada ya mjadala mrefu uliokwisha kwa kupiga kura.

Zitto na wenzake tisa hawakuingia ndani ya ukumbi wa Bunge siku Rais, alipolihutubia. Baadaye, aliitisha mkutano na waandishi wa habari kueleza kupinga kitendo cha wenzake.

Baada ya Zitto na wenzake kutoingia kwenye ukumbi wa Bunge ili watekeleze uamuzi wa kutoka nje wakati Rais Kikwete akianza kuhutubia, Katibu Mkuu wa Chadema (Slaa), alisema waliosusia uamuzi huo, wangechukuliwa hatua na Kamati ya Wabunge wa Chadema.

Baadaye Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitangaza kumwandikia barua Zitto na wabunge wengine tisa ambao hawakuingia kwenye ukumbi wa Bunge, kuwataka wajieleze kwa maelezo kuwa walichofanya ni utovu wa nidhamu.

Wakati taarifa hizo za kuvuliwa uongozi wa Zitto zikibainika, mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alilkuwa ametoka katika Hospitali ya Aga Khan, alikokuwa amelazwa kwa ugonjwa wa tumbo.

Jana gazeti la Mwananchi lilichapisha habari zilizomkariri Zitto, akidai kuwa ugonjwa huo ulitokana na kula chakula chenye sumu.

Taarifa zilisema Zitto alilazwa katika wodi namba 57 iliyoko katika ghorofa ya tatu na alikuwa amechukuliwa vipimo vyote ili kutihibitisha kiini cha ugonjwa wake.

Hata hivyo madaktari katika hospitali hiyo, walisema hawakuona tatizo na kwamba wanasubiri kipimo kikubwa.

Akizungumza na gazeti hili akiwa hospitalini, Zitto aliwataka Watanzania kutokuwa na hofu na kuugua kwake kwa kuwa ni ugonjwa wa kawaida na kuwasihi wamuombee apone haraka.

"Watanzania wasiwe na wasiwasi na kuugua kwangu. Hii ni kawaida tu, madaktari wananipa matibabu niombeeni nipone haraka," alisema Zitto.

Kuhusu hatua ya chama hicho kumvua madaraka, Zitto, alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa rasmi kutoka chama chake mbali na kusoma kupitia katika vyombo vya habari.

Alisema hata hivyo, hakuwahi kuomba kupewa wadhifa huo na kwamba ikiwa watu waliomwona anafaa kufanya kazi na kumpa wadhifa huo, wakiamua kumnyang’anya siyo tatizo kubwa kwake.

“Kwa sasa nadhani suala la afya yangu ndiyo muhimu zaidi. Ngoja kwanza nitoke hapa na afya yangu iimarike na kama kutakuwa kuna sababu ya mimi kuzungumza, nitazungumza,” alisema Zitto:

“Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu, kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo.”

Alipoulizwa kuhusu madai ya Zitto kuvuliwa wadhifa ndani ya Bunge, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe,alisema chama kitatoa taarifa baadaye.

Chanzo: Mwananchi

8 comments:

 1. Haya haya uchaguzi umekwisha sasa kilichobakia nini nini? Ndio hayooo, kwani yatasaidia kuuza `maneno yetu..' mmmmmh, mwenye macho haambiwi tizama!

  ReplyDelete
 2. Naona wameanza kutiliana sumu tayari. Badala ya kujiandaa na kujiimarisha wilayani na vijijini tayari wanagombania pesa.

  Sasa wamemtambua Kikwete. Hiki ni chama cha watoto and I am happy kwamba walichakachuliwa hawa. Wangeshinda TZ ingewaka moto. Shame on Chadema and all the opposition hypocrisy. Kwa mtindo huu CCM will rule forever!

  ReplyDelete
 3. Hatima ya siasa za zitto hazitofautiani sana na ya Mrema kama hatakuwa mwangalifu. Binafsi nimekuwa nikifuatilia nyendo za Zitto kisiasa kwa karibu na nilichogundua ni kwamba bwana mdogo Zitto ni mtu mwenye tamaa ya madaraka na ni rahisi kurubuniwa. Hata hivyo nilihisi kutumiwa kwake na CCM kuimaliza Chadema. Proganda zote zilikuwa zikitumiwa na CCM chanzo chake ni Zitto, kusema Chadema ni chama cha udini na Wachaga.

  ReplyDelete
 4. Magazeti ya udaku tayari wanasema Zitto kawekewa sumu kwenye chakula. Sasa tuamini kipi, jana gazeti la mwananchi lilieleza kuwa ni Food poisoning. Hatuwezi kutofautisha food poisoning na kuwekewa sumu kwenye chakula. Watanzania kweli kazi tunayo!

  ReplyDelete
 5. Kwa tunaomjua Zitto hii si ajabu. Kijana ana tamaa kama fisi na isitoshe ni mnafiki hakuna. Anachezea bahati maana hata kwenye siasa zenyewe ameingia kwa bahati. Hana weledi kama wanaompa.

  ReplyDelete
 6. Chadema acheni kumwandama Zitto. I believe angekuwa Mchagga au mtu kutoka mikoa ya Kusini kusingekuwa na any problem. Chadema ni chama cha kikabila na Zitto anaonekana kuwa ni outsider.

  I am very disappointed kwa sababu Chadema kilileta matumaini. Sasa kuna pesa za Sabodo, kuna za ruzuku na tayari wanagombana kama mafisi. Huyo padri wao naye hakuna lolote la maana. Kwa mtindo huu CCM will rule FO EVAAA!!!

  ReplyDelete
 7. Typo hapo juu. Nilitaka kusema Angekuwa mtu kutoka mikoa ya Kaskazini...

  ReplyDelete
 8. Zitto = Mrema = CCM !!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU