NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, December 10, 2010

FIKRA YA IJUMAA: INABIDI TUJIFUNZE KUYATAZAMA MAMBO KATIKA UJUMLA WAKE


"I know a man who gave up smoking, drinking, sex, and rich food. He was healthy right up to the time he killed himself"

Johnny Carson (1925 - 2005)
************
 Picha hii inapatikana hapa.
 • Ati, ni mara ngapi tunamakinikia na kukazania jambo moja tu na kusahau ule ukweli kwamba mambo mengi hapa duniani ni tata, yameshonana, kutegemeana na kukamilishana?
 • Ni kwa nini baadhi ya madhehebu, kwa mfano, hukazania kutekeleza amri moja tu au mbili hivi na kuzipuuza zile zingine pamoja na ukweli kwamba Biblia inatuambia wazi kwamba avunjaye moja kati ya hizi basi amezivunja zote?
 • Kwa nini tunachagua wenzi wa maisha kwa kuzingatia uzuri wa umbo tu bila kujali tabia na haiba za ndani zenye thamani zaidi kama utu, wema, ukarimu, uchapakazi na upole?
 • Kwa nini tunachagua viongozi kwa kuangalia sifa zao nusu nusu na ushabiki wa vyama vya kisiasa tu bila kujali hasa ni yupi anaweza kutupigania na kutuletea maendeleo ya kweli?
 • Kwa nini tunapenda kuyatazama mambo kivivu na hatimaye kuishia kuyakabili nusunusu? Inabidi sasa tujifunze kuyatazama na kuyakabili mambo katika ujumla wake.
Poleni na samahani kwa maswali mengi namna hii. Wikiendi njema. 
************

  4 comments:

  1. Ni maswali mazuri na ya kufikirisha ngoja ninywe kwanza vikombe vitatu vya chai na ntarudi na kujibu. Wikiend njema nawe pia kakangu!!

   ReplyDelete
  2. Hiyo ndiyo inaitwa `busara' kuangalia mambo kwa mapana kuliko kuangalia kwa ujumla wake...tungekuwa na busara, hakuna mtu angemnyoshea mwenzake kidole, kwani wote tungekuwa makini tukijua kuwa kosa la yule moja mimi nina makosa matatu...!

   ReplyDelete
  3. Shule hii ni TANI kilo elfu fulani Mkuu!Wikiendi njema Mkuu!

   ReplyDelete
  4. Walonitangulia wamesema
   Ila nichangie kwenye NUKUU kwamba yawezekana aliyeacha hayo yote, alikuwa na mapungufu ya akili yaliyompelekea kujiua.
   Ndio maana kuna umuhimu wa kutofuata kile usichojua mwisho wake.
   Kwa waliomuona mpaka siku moja kabla hajajiua na kama mpaka sasa hawajui kuwa alijiua, watadhani alikuwa tajiri sababu ya kuacha kutumia hayo, lakini kwa waliotambua kuwa alijiua, ndio maana nilisema "Hakuna kibaya kisicho na uzuri...... Yategemea umeachia wapi kuoanisha na tukio" (rejea http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/09/hakuna-kibaya-kisicho-na-uzuri.html)

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU