NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, December 6, 2010

HAKUNA MCHEZO "MZURI" KAMA HUU (SEKUNDE 39 TU)

 • Wanaijeria wana methali isemayo kwamba "hata kama una nguvu namna gani, lazima kuna mtu mwenye nguvu zaidi yako." Safari hii ukweli huu umejidhihirisha tena kwa Paul Williams, mwanamasumbwi anayeogopwa sana kutokana na staili yake ya kipekee ya kupigana na ugumu wake wa kuangushwa na makonde ya wapinzani wake. 
 • Safari hii hata hivyo, konde moja tu la kushoto kutoka kwa mpinzani wake aitwaye Martinez lilitosha kumfanya apoteze fahamu kwa dakika kadhaa na kuacha wachambuzi wengi wakiwa wameduwaa.  

 • Kuna jambo la kujifunza hapa hasa kutokana na tabia ya baadhi yetu ya kujiona kwamba sisi ndiyo sisi. Tukumbuke kwamba daima kuna akina sisi ambao siyo sisi lakini ni sisi zaidi ya sisi! Kamuulize Paul Williams atakwambia!

3 comments:

 1. mimi ni kati ya watu wenye iguvu ila ni mtu wa mwisho kupigana, na nafikiri mpaka nakufa, nitakuwa sijapigana kamwe

  ila masuala ya masumbwi, mwisho wa mastaa wotoe, huanza kwa kupigwa taratibus

  ReplyDelete
 2. Tukumbuke kwamba daima kuna akina sisi ambao siyo sisi lakini ni sisi zaidi ya sisi!

  Hapa umenikamata na nimejifunza kitu!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU