NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, December 26, 2010

KWA WAKWE ZANGU SIKU YA KRISMASI KWEUPEE !!!

 Mzunguko wa Posta: makutano ya Boma road, Double road, na Railway road
 • Mila ya wakwe zangu (Wachaga) ya kwenda kijijini kwao kujumuika na kusherehekea sikukuu ya Krismasi pamoja na ndugu na jamaa ni mila nzuri inayopaswa kuendelezwa. Haipendezi kuona watu wakitumbua raha mijini na kusahau nyumbani walikotoka.
Barabara ya Tanesco
 • Siku ya Krismasi jana Moshi mjini kulikuwa kweupeeee kabisa kwani watu wengi walikuwa wamerudi milimani kusherehekea sikukuu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao. 
 Barabara ya Boma

 Hakukuwa na watu Moshi mjini.

Hata hivyo wapo wanaokerwa na tabia hii ya Wachaga kwenda Moshi hasa kama kunaambatana na kufanya matambiko. Picha zote na baadhi ya maelezo ni kutoka kwa Amani Masue.

4 comments:

 1. Hapa ndugu yangu umesema kwe kweli kabisaaa. Yaani sisi Wachaga bwana lazima tuende kuzini nyumbani Kirsimasi. Yaani lazima tuka riee mbee (Kunywa mbege ya kushare), Kunwya kisusio na kula nyama choma. Asante sana ndugu... Aisee kumbe umeoa kwetu. Karibu sana ndao!

  ReplyDelete
 2. Kufuenda-ro-mae? Nifonisha-da-mayanka! Hebu nipatia kata moja ya robo-ya-sumni......ikiwa nzuri ntaongeza pesa nane! Woii! usinletee uabunuasi ria mbeke maana kitalolo kinaningoja mgombani.

  ReplyDelete
 3. I love this! The street views bring back memories of Moshi Mjini. One thing I like about African American culture is the tradition of family reunion! Bravo to the Chagga Krismasi tradition--a time to recharge the batteries! Check this out:-
  Kufuenda-ro-mae? Nifonisha-da-mayanka! Hebu nipatia kata moja ya robo-ya-sumni......ikiwa nzuri ntaongeza pesa nane! Woii! usinletee uabunuasi ria mbeke maana kitalolo kinaningoja mgombani.

  ReplyDelete
 4. Kim asante sana na mie pia umenikumbusha mbali sana na kitalolo cha maharage na maziwa. Matondo asante sana kwa kutukumbuka wachaga.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU