NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, December 7, 2010

MAUAJI YA VIKONGWE YANAENDELEA MKOANI SHINYANGA

Waua vikongwe, wawachoma moto

*Waliwatuhumu kuwa wachawi

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watu 10 wilayani Bukombe wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya kikatili ya wakazi wawili wa kijiji cha Ibamba wilayani Bukombe akiwemo mwanamke kikongwe mwenye umri wa miaka 90 waliohisiwa kuwa ni wachawi.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Charles Nyanda alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao hata hivyo hakuwataja majina, kunatokana na tukio la wanakijiji wenye hasira kuwashambulia kwa kipigo wanakijiji wenzao  na kusababisha vifo vyao na miili yao kuichoma moto.

Bw. Nyanda aliwataja waliouawa kuwa ni pamoja na Bi. Roza Kagoma (90) na Bw. Balandye Matulo (80) wote wakazi wa Kijiji cha Ibamba Kata Uyovu wilayani Bukombe mkoani Shinyanga. Bw. Nyanda alisema mauaji hayo yalitokea Desemba Mosi mwaka huu saa 5.00 asubuhi katika kijiji cha Ibamba baada ya wanakijiji hao kuwavamia wanakijiji wenzao na kuwaangamiza.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni imani potofu za ushirikina na kwamba mara baada ya uchunguzi juu ya tukio hilo kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji. 
Chanzo: Blogu ya Majira.
Unaweza kupata kipeperushi cha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuhusu suala hili hapa. Imani za kishirikina sasa zinazidi kupamba moto katika jamii yetu, na kama nilivyowahi kuuliza hapa, sijui kama tunarudi nyuma au tunasonga mbele!

2 comments:

  1. Habari kama hizi zinasikitisha sana tu!:-(

    ReplyDelete
  2. Nanyi Wasukuma mmezidi kwa kurogana. Mtakatana mapanga mpaka lini? Elimu mkoa wa Shinyanga unashika mkia and yet instead oc concentrating on the + side, solution yenu ni mapanga. Mtafika?

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU