NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, December 6, 2010

MKAPA ATAKA VYUO VIKUU KUEPUKA UFISADI


Mkapa ataka vyuo vikuu kuepuka ufisadi

Na Raisa Said, Lushoto

RAIS mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kuzingatia dhana ya uwazi, ukweli na uaminifu ili kuepuka vishawishi vya kutumia ujuzi wao kujipatia kipato kwa njia zisizokubalika kimaadili na kitaaluma.

Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu kishiriki cha Sebastian Kolowa (SEKUCo) mwishoni mwa wiki, Mkapa ambaye katika utawala wake alisisitiza juu ya dhana ya uwazi, ukweli na uaminifu aliwataka wahitimu hao kuacha kutumia njia za mkato zinazowasababisha kuwa mafisadi.

Jumla ya wahitimu 132, wakiwemo wanaume 75 na wanawake 57 walitunukiwa shahada ya kwanza ya elimu maalum.

Alisema ufumbuzi wa matatizo na mafanikio ya maisha ni kujifunza utamaduni na kujiwekea malengo ya kila mwezi na hata kwa mwaka.

“Ukishajiwekea malengo na kuyapanga kwa uzito kwa kulingana na umuhimu wake, muda, fedha au rasilimali ulizonazo utaona mafanikio mazuri zaidi kazini kwako na kwa maendeleo yako wewe na jamii nzima ya Watanzania,” alieleza Mkapa.

Mkapa alisisitiza kuwa wataalamu, hasa wa elimu maalumu sharti wawe mfano bora wa kuigwa na jamii ya Watanzania na popote watakapokuwa.

“Utumishi bora unadai mjiepushe na kauli ya ‘njoo kesho’. Nendeni mkawe mabalozi wazuri wa chuo hiki,” alisisitiza.

Akizungumzia juu ya kuongezeka kwa mahitaji ya elimu ya juu katika soko la ajira kutokana na mabadiliko makubwa yanayoendelea duniani, yakiwemo maendeleo ya sayansi na teknolojia, alikipongeza chuo hicho kwa kujiandaa vema katika mwelekeo wa kutoa elimu katika fani mbalimbali ikiwemo fani ya teknolojia ya habari kwa lengo la kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kutoa huduma bora kwa jamii katika mazingira mapya ya kiuchumi, soko huru, mabadiliko makubwa ya teknolojia na utandawazi.

Alitoa rai kwa wadau wote wa elimu nchini na duniani kote kuendelea kuunga mkono na kusaidia kwa dhati juhudi zinazofanywa na chuo hicho kutoa elimu yake. Chuo hicho ni chuo kishiiriki Chuo Kikuu cha Tumaini.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Profesa John Shao aliwataka wahitimu kutoridhika na taaluma waliyo nayo na kuwataka kujua kuwa uaminifu na uadilifu katika kazi ni moja wa vigezo vitakavyowafanya wathaminiwe sehemu watakazofanya kazi.

Pia aliwataka kuwa tayari kutumika na kuishi na kufundisha maadili mema na kukabiliana na tamaa ya ufisadi, kuendelea kwa ugonjwa wa ukimwi na mwenendo wa kutopenda kufanya kazi kwa moyo na ubunifu.

Chuo cha SEKUCo kilianzishwa mwaka 2007 na ni chuo pekee ambacho kimeanzishwa na kuendesha mafunzo ya elimu maalum. 
Chanzo: Mwananchi 

7 comments:

 1. na hakuna wa kuzomea!!! kweli sie ni kondoo!!

  ReplyDelete
 2. Wewe Matiya wewe. Mwogope Mungu na usidhani kwamba huko uliko ni mbali. Kuna njia za kistaarabu za kupingana na mtu na siyo hayo maneno yako ya kipuuzi. Eti go to hell! Pengine wewe ndiyo uende huko Hell.

  Kwa taarifa yako hakuna rais aliyefanya kazi proper kama Mkapa. Alirithi nchi iliyokuwa bankrupt kutoka kwa Mzee Rukhsa na akaleta discipline, mpaka tukaweza kuanza kujikusanyia pato letu wenyewe. History is on his side and later on, when you and me are gone, he will be revered.

  Kuna makosa yalifanyika katika ubinafsishaji wa mashirika na alishasema kwamba he regrets it lakini kosa moja doesn't make him to deserve this kind of mud you are throwing at him.

  Tuwe wastaarabu na kujifunza kuargu kwa heshima jamani otherwise we look stupid.

  Na hata nyie wenye blogu, msitumie uhuru wa habari vibaya. Comments like this one hata iwe deleted ni sawa. That is why I love Michuzi for his censorship pamoja na kwamba ni mtu wa CCM.

  And for your information, the day CHADEMA comes to power, tribalism will spring forth and the peace that we love in our country will cease to exist. I know kwamba wewe ni Mmbulu kama Dr. Slaa mzinzi nambari wani mporaji wa wake za watu with no morals whatsoever na umeumia sana kwake kushindwa. Ulikuwa umekuwa promised uwaziri au ubunge wa kuteuliwa nini. Basi baba imekula kwako na CCM tunapeta tu. Jikaze kiume na huo ndo ukubwa.

  Mkapa dear, don't listen to this non sense coming from losers who are coming from people who are out of the country. We know what good you did to our country and History is on ur side. May God Bless Tanzania!

  ReplyDelete
 3. Mmmh Dada Mwanaidi!! Sina la kusema mimi... Maoni yako umeyaanza vizuri kwa kutoa dondoo za msingi lakini umeharibu mwisho kwa kumpaka mbovu Dr Slaa. Kwahiyo wewe na mheshimiwa hapo juu hamna tofauti yoyote. Msiwe na chuki binafsi bali tumieni uhuru huu kuwaelimisha wengine. Ungemalizia kwa dondoo kama ulivyoanza. Mjue hasira hasara...

  ReplyDelete
 4. Mpaka sorry Mkapa can't be serious or be taken seriously so to speak.

  ReplyDelete
 5. Oh Boy! Mkapa. What is wrong with you???

  ReplyDelete
 6. Mkapa baba. Asante sana kwa wosia wako. Sasa nenda ukapumzike katika hoteli lako la kifahari kule South Africa, hoteli ambalo hata Mandela alikataa kuja kulifungua kwa kumheshimu Mwalimu Nyerere!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU