NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, December 6, 2010

MTOTO WA MKULIMA AKATAA SHANGINGI LENYE THAMANI YA MILIONI 280 !!!

 • Nimezisoma habari hizi za Mtoto wa Mkulima kulikataa shangingi lenye thamani ya shilingi milioni 280 kwa furaha na mshangao. Nimefuarahi kwa sababu kiongozi huyu ameonyesha kwa vitendo kwamba jina lake la "Mtoto wa Mkulima" hajapewa kwa kubahatisha. Ni mtoto gani wa mkulima anayeweza kuendesha gari la thamani ya milioni 280 wakati mama na baba yake kule kijijini hawana maji ya kunywa, umeme, zahanati wala elimu ya kuaminika?
  • Nimeshangaa kwa sababu sijasikia siku za hivi karibuni kwa kiongozi ye yote kukataa gari la kifahari na marupurupu mengine manono yanayoambatana na nyadhifa mbalimbali hususani ubunge. Na ninavyoijua jamii ya Kitanzania, si ajabu kuna wengine ambao pengine sasa wanamcheka na kumwona kwamba ni mchovu tu. Tunaishi katika jamii inayojikanganya, jamii masikini sana na inayojaribu kupambana na ufisadi lakini wakati huo huo bado inawaona watu wanaofisadika kama mashujaa. Ukishika wadhifa wa juu serikalini au chamani ukawa mwadilifu na halafu ukaja kuacha madaraka ukiwa na maisha ya kawaida, jamii inakucheka kwamba ulizubaa, ulikuwa mjinga, mshamba na kwamba ulifikiri mali ya taifa ni mali ya mamako.Falsafa inayotukuzwa ni ile ya "Chukua chako mapema!"
  • Fisadika, tajirika kupindukia na wewe ni shujaa; na siku ukipata misukosuko unapokelewa jimboni mwako kama shujaa.
  • Hongera Mtoto wa Mkulima kwa kuongoza kwa mfano. Ni viongozi wachache wenye uwezo wa kufungamanisha azimio na kitendo. Pengine wewe ni Sokoinne mpya. Pengine wewe ni Nyerere mpya; na kupitia kwako watoto wa wakulima wenzako wanaweza kupata tumaini. Lakini kama watangulizi wako hawa (ambao walishindwa), wewe utaweza? Je, juhudi hizi za peke yako zitafanikiwa? Na kama wewe ndiye kiongozi wa serikali, hii inamaanisha nini? Badala ya juhudi hizi za peke yako nawe ukiwa kama kiongozi wa serikali, mbona usipige marufuku ununuzi wa magari haya ghali? Nimechanganyikiwa!
  ****************
  • Makala ya Mwananchi kuhusu suala hili inapatikana hapa. Baadhi ya takwimu katika makala ya Mwananchi ni...
  • Mwezi Aprili 2008 jumla ya magari yote ya serikali nchini yalibainika ni kati ya 35,000 hadi 40,000.
  • Kati ya orodha hiyo magari ya kifahari ya Toyota Landcruiser Vx8 na VX, GX na aina nyingine ya Landcruiser yalikuwa kati ya 10,000 hadi 15,000.

  1 comment:

  1. Mbio za peke yake hazitamfikisha popote huyu. Kama ulivyosema hapo juu wenzake saivi wanamcheka tu and the society itself doesn't give a damn!

   Na akizidisha mbwembwe na kuwa very famous asishangae wakimKolimba au kumSokoinne. Aende akamwulize mwenzake Robert Ouko wa Kenya aliyejaribu haya mambo atamwambia. Chota chako kungali mapema. Ukija kuacha uwaziri mkuu na umasikini wako huo utachekwa sana si na akina Lowassa tu bali hata na mke na watoto wako. Shauri yako mtoto wa Mkulima.

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU