NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, December 9, 2010

NGELEJA: HOJA SI KUJIUZULU


Ngeleja: Hoja si Kujiuzulu

Na Lucy Lyatuu

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema tatizo sio kujiuzulu, bali ni jinsi ya kutatua kero za umeme na kuhakikisha mgawo wa umeme unakwisha nchini.

Ngeleja alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na madai ya kutakiwa kufanya hivyo kama ambavyo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila alivyodai kupeleka hoja binafsi bungeni ya kutokuwa na imani naye.

Ngeleja alisema hayo ni mawazo ya Mbunge huyo na kamwe hawezi kuzuia mtu kutoa maoni yake kwa kuwa ana hisia kali kama ambavyo yeye (Ngeleja) anazo.

Madai ya Kafulila aliyatoa wakati alipotangaza kuwa anakusudia kupeleka hoja binafsi katika Mkutano wa Pili wa Bunge, Februari mwakani kutaka serikali iwajibike kwa kuliingizia Taifa hasara kwenye sekta ya umeme, kutokana na hukumu ya kesi ya Dowans na Tanesco ambayo Tanesco inapaswa kulipa Sh bilioni 185.

Kafulila pia anakusudia katika hoja hiyo, kulitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini, kwa madai kuwa ameshindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati na Mpango Kabambe wa Usambazaji wa Umeme nchini.

“Tatizo sio kujiuzulu, bali tatizo ni kufuatilia na kutatua kero za umeme zinazowasumbua wananchi.

Aliyosema Kafulila yanatokana na adha ambayo anakutana nayo kama ambavyo na mimi inanikumba,” alisema Waziri huyo aliyerejeshwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza tena wizara hiyo.

“Nayaheshimu mawazo ya mheshimiwa mbunge.., siwezi kuzuia yeye kutoa maoni yake, ila aelewe kuwa serikali inaendelea kutatua tatizo hilo kwa nguvu kubwa,” alisema Ngeleja.

Kuhusu Dowans, alisisitiza kuwa liko mikononi mwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo yeye ndiye atakayeshauri na kuamua kama kampuni hiyo italipwa ama halipwi.

Alisema Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya sheria na maoni ya watu binafsi hayawezi kuongelewa.

“Kwanza sitaki kufungua ukurasa wa suala hili, nchi hii inajielekeza katika misingi ya sheria, hivyo sheria zilizopo zitatumika pamoja na kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu,” alisema Ngeleja.

Alisema kwa sasa faili liko kwa Mwanasheria Mkuu ili aweze kulipitia kutoa mawazo na ushauri wake juu ya suala hilo ila ifahamike kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya sheria na utawala bora.

Kwa mujibu wa Ngeleja, kwa sasa serikali haiwezi kuzungumzia hisia za watu, bali hatima yake itaamuliwa na Mwanasheria Mkuu na kukanusha taarifa iliyoandikwa katika moja ya vyombo vya habari nchini, kuwa serikali yajivua zigo la deni la Dowans na kusema endapo Mwanasheria Mkuu akitoa maoni ya Dowans kulipwa, watakaa na kulitazama zaidi na kama Tanesco inaweza kubeba mzigo huo.
Chanzo: Habari Leo

4 comments:

 1. Ajiuzulu ACHEKWE?
  Unajua tofauti ya kipato kati ya MANENO na MSHAHARA?
  Jiulize UKISEMA INAMUUMIZA NINI na AKIJIUZULU ATAKOSA NINI?

  Hii ndio Tanzania yangu....Yenye wabunge wawanyonyao wananchi na si kuiendeleza nchi (kama nilivyoeleza nawe kushiriki hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/02/tanzania-yanguyenye-wabunge-wa-wananchi.html)

  SHAME ON THEM

  ReplyDelete
 2. kwa nchi nyingi...hili suala ukijumlisha na mgao vilitosha kumfanya waziri kujiuzulu

  ReplyDelete
 3. Acheni hizo. Ngeleja ni waziri kijana ambaye anajitahidi sana. Mgao wa umeme siyo kosa lake na kwa kuwa ameonyesha kwamba anaweza kuchapa kazi tuangalie mbele sasa. Natumaini kwamba hakutakuwa na mgao tena. Amecharuka mafundi wamefanya kazi usiku na mchana na everything is OK.

  Let us look forward guys.

  And you know what. Given power ningependa kuwapa uwaziri nyie complainers ambao hamjui nchi hii inavyoendeshwa. The problem hapa is the system itself. Mtu unapewa wizara na unakuta system yote ni iko rigged, and you cannot do anything. Trust me, I was in the government and it is very frustrating. You talk to the prez. na unaambiwa don't do that. Na wakiona kwamba you are not working with dhem, wanakutema.

  The system is rigged and very complicated ndo maana shida zetu haziishi. Problem siyo mtu it is the system and until I begin to see solutions targeting the system itself, I will continue believing that we are not even close to finding a real solution to our problems.

  Haya let us remove Ngeleja and put you guys there. NOTHING WILL CHANGE BECAUSE THE SYSTEM IS THE SAME!!! So kuandika comments za kukandia iz very easy but that is the truth!

  ReplyDelete
 4. Resigning and taking responsibility is not our culture. Ndo maana ukichemsha huku unahamishiwa kwingine ili huko ukaharibu. Unakuta minister au mkuu wa shirika anazungushwa weee and everywhere he/she goes kazi yake ni kuharibu...That is our culture...

  Lowassa must be applauded for resigning ingawa inasemekana kwamba aliahidiwa kwamba atarudi muda si mrefu. Naona imekula kwake!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU