NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, December 12, 2010

NONDOZZZZ !!!!!!

Hawa ni Chuo Kikuu cha Dodoma.

Hawa ni Chuo Kikuu cha Muhimbili.

Hawa ni Chuo Kikuu cha Fatih, Uturuki.
*************
 • Hongera sana mtunukiwa! Bila shaka watunuku hawa wanafahamu mchango wako. Hebu basi mchango wako huo na ukaonekane kwa Watanzania wa kawaida, ndugu zetu wa vijijini wasio na umeme, maji safi ya kunywa, shule za kuaminika wala zahanati za kuridhisha. Unayo miaka mitano zaidi ya kuipamba historia yako na kuiachia Tanzania urithi wa kumezewa mate na kupigiwa mfano. Katende!!!

7 comments:

 1. Hata Mzee Rukhsa kumbe naye ni mkuu wa chuo kikuu. Mtu darasa la saba anaconfer Ph.D degrees. Only in Tanzania my friend!

  ReplyDelete
 2. Huyu baba Nondozz zitamuua. Naoma tutakuwa tunamrefer kama Dr. Dr. Dr. Mh. J.K. Hata Nyerere angekuwepo angemwonea wivu

  ReplyDelete
 3. Digri zinatolewa kama vile njugu! Nadhani hatuelewi hata maana PhD. Nyerere akitunukiwa hata PhD ishirini nisingekuwa na neno. Lakini kutoa PhD kwa watu wasiostahili ni kubweteka.

  ReplyDelete
 4. Hata Mzee Rukhsa kumbe naye ni mkuu wa chuo kikuu. Mtu darasa la saba anaconfer Ph.D degrees!

  Sio kweli!

  Mzee Rukhsa ameongoza nchi, kama rais! Wewe, je?

  ReplyDelete
 5. Malkiory Matiya, tunangoja yako!

  ReplyDelete
 6. Matondo, tuwekee na picha ya Kikwete alipoanza kupa hiyo doctorate honoris causa hapo Kenyatta University.

  ReplyDelete
 7. Mimi sina ugomvi na ma-Ph.D haya ya bure kwani naamini vyuo vinavyomtunuku vinaelewa vinachofanya. J.K. ana miaka mitano ya kuweka historia, si tu ya kuwa na Ph.D nyingi bali kwa kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania. Na mwanzo mzuri ni kutelekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni! Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana ati!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU