NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, December 29, 2010

TUMEVUNJA REKODI YA BARIDI ILIYOWEKWA MWAKA 1925!!!

 • Najua kuwa wakazi wa sehemu zenye baridi kali kama vile Minnesota, Maryland, Cambridge, kule Ulaya (Da Mija na Candy1) na nchi za Skandinavia (Mtakatifu, Matiya, Yasinta na Edna) mtacheka mtakaposoma hapa lakini hata sisi huku Florida hali ya hewa imetuchachia kiasi kwamba rekodi ya baridi iliyowekwa mwaka 1925 (nyuzi 24F) imevunjwa usiku wa kuamkia leo joto liliposhuka na kufikia nyuzi 21F
 • Kama picha hiyo juu inavyoonyesha, jimbo la Florida ni mzalishaji mkuu wa matunda hasa machungwa na malimao na barafu kama hii inaweza kuleta hasara ya mamilioni ya dola kwa wakulima. 
 • Tatizo jingine ni kwamba karibu miti yote ya maua tunayopanda hapa huwa haivumilii baridi kali kama hii na unaweza kuona kwamba hata michikichi nayo imeanza kunyauka. Watoto kwa upande wao, walifurahia kuona vibonge hasa vya barafu pengine kwa mara ya kwanza maishani mwao.
 • Kutokana na baridi hii iliyotanda sehemu mbalimbali duniani, wapinzani wa ile dhana ya kuongezeka kwa joto duniani wanaonekana kufurahia huku wakidai kwamba baridi hii inaonyesha kwamba makelele yaliyokuwa yakipigwa kuhusu kuongezeka kwa joto duniani yalikuwa ni ya uwongo.
 • Hapa chini ni picha mbali mbali zikionyesha baridi hii iliyovunja rekodi hapa kijijini ninapoishi.
****************
Kwa picha zaidi nilizopiga mwenyewe kuhusu hii barafu hapa Florida bofya HAPA.

8 comments:

 1. Kaka matondo baridi ni baridi tu poleni sana. naona mwaka huu ni mwaka wa baridi si umeona hata uingereza si kawaida sana kuwa na baridi kiasi hiki mpaka wanaacha kucheza mpira. Ni labda siku za mwisho....

  ReplyDelete
 2. niwapongezeni tu wakati Bukoba tukiwa na hali ya hewa ya kawaida huku dar wakisota kwa joto! HOngereni

  ReplyDelete
 3. Pole sana Matondo, mwaka huu yaelekea ni global cooling, hapa kwetu wametabiri kuna siku itafika nyuzi -50deg. C.

  ReplyDelete
 4. kukiwa na baridi wengine wanatengeneza fedha tokana na maguo ya kuhifadhi joto mwilini....lol!

  kimbembe ni pale itakapozidi na kuleta watoto wasiotarajiwa teh teh teh teh!

  ReplyDelete
 5. Da Yasinta na Matiya - pengine nyinyi huko mmeshazoea kwani nikiona picha kwenye blogu zenu barafu imerundikana mpaka kufunika miti kabisa. Sasa hata hayo magari sijui mnayaendeshaje. Ikifikia -50deg.C kuna kutoka nje kweli au ni kukaa ndani tu na kujitwika mavodka?

  Kamala - ndiyo joto la Bukoba kwa kawaida huwa ni safi sana. Naukumbuka upepo mwanana wa Ziwa Nyanza pale Kahororo.

  Ng'wanambiti - nani alikwambia kuwa baridi inaleta watoto wasiotarajiwa? Mbona nchi za Skandinavia ndiyo zinaongoza kwa "upungufu wa watoto" pamoja na ukweli kwamba ukizaa mtoto huko unalipwa maelfu ya pesa?

  Kuhusu biashara ya maguo ya joto hapo umesema kweli. Kila kitu kwa hawa jamaa ni biashara!!!

  ReplyDelete
 6. Matondo, Wafini ni woefu sana kwa kucheza na snow, unakumbuka wavyowapiga maadui zao Russia pamoja na Wafini kuwa wachache kwa idadi. Iikuwa ikiitwa winter war, askari wa kifini walikuwa wakivaa kombati nyeupe kama barafu wakati wenzao warusi walivalia magwanda ya kawaida, hapo utaona ni jinsi gani warusi walivyoangamia. Si utani barafu hata ishuke kwa mwaka mzima hapa hakuna kitakachosimama, zipo nyezo za kila aina.

  Pili, umempatia Ng'wambiti ile mbaya, maana huwa namwaminia kwa kujenga hoja, hasa za kuwamaliza mafisadi.

  ReplyDelete
 7. Oi poleni!!! Baridi mwaka huu yaani dah, halafu ikiisha, unatazamia winter nyingine unaomba isiwe baridi sana but for some reason it just gets worse...weird stuff I swear!...n they say there is "GLOBAL warming..."...seriously...I don't think it is "global"

  ReplyDelete
 8. Matondo kama na kwenu imefikia hivyo basi ni hatari. Uingereza snoo ilianza November yaani hatari tupu, lakini wiki hii naona tumepumzishwa kidogo tunaomba Mungu iendelee hivi..

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU