NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, December 14, 2010

WATANZANIA WA NJE WALALAMIKAJI - NYALANDU

Watanzania mlioko nje: Dongo hilo la Mh. Nyalandu. Mnajiteteaje?
***************

Nyalandu: Watanzania wa nje walalamikaji 
(Sunday, 12 December 2010)

Na James Magai

NAIBU Waziri wa Viwanda,  Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu, amesema sehemu kubwa ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi, wamekua walalamikaji tu kuhusu taratibu za uwekezaji,  lakini hawachukui hatua.

Nyalandu alitoa kauli hiyo wiki iliyopita, wakati akizungumza na Mwananchi  baada ya kuzindua Kampuni ya Ndege ya Bold Air, inayomilikiwa na John Ndunguru, Mtanzania anayeishi Marekani. Uzinduzi wa kampuni hiyo, ulifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,  jijini Dar es Salaam.

“Watanzania waache kulalamika tu kwenye mablog. Wengi wamekuwa walalamikaji tu, lakini hawachukui hatua,” alisema Nyalandu.

Naibu waziri huyo aliwataka Watanzania hao, watumie muda wa kukaa kwenye mitandao, kuangalia taarifa zinazohusu fursa za uwekezaji zinazopatikana pia hata kwenye mtandao wa Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania na kusaidia shughuli za  uwekezaji hapa nchini.

“Kitendo cha kulalamika bila ya kuchukua hatua ni ishara kwamba wengi wao sio wabunifu. Nampongeza ndugu yangu John Nduguru, kwa kutumia fursa hiyo na kuanzisha kampuni hii,” alisema.

Nyalandu alimpongeza Ndunguru kwa uamuzi wa kuja kuwekeza nyumbani, jambo ambalo alisema litasaidia katika kuinua uchumi wa Tanzania.

"Pamoja na kwamba Ndunguru amekuwa akifanya biashara zake nchini Marekani, lakini ameona umuhimu wa kuwekeza nyumbani jambo ambalo litasaidia kuinua uchumi na kutengeza ajira kwa Watanzania wenzake," alisema Naibu waziri.

Kwa upande wake, Ndunguru aliishauri serikali iangalie na kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali za uwekezaji ukiwemo mlolongo mrefu kuhusu mchakato wa uwekezaji.

Alisema mchakato wa uwekezaji nchini ni mrefu, jambo linalowafanya Watanzania wengi walioko nje, wakate tamaa, na kwamba hiyo inachangiwa na tatizo la kutakiwa kutumia muda mrefu katika kumilisha taratibu za uwekezaji.

“Tataratibu zetu bado ni ngumu, maana mtu anatumia muda mrefu na gharama na kubwa, jambo linalowakatisha tamaa Watanzania wengi kuja kuwekeza nyumbani," alisisitiza.

Alisema ameamua kuwekeza katika usafiri wa anga kwa kuwa kuna nafasi nyingi za kufanya biashara na kwamba wakati umefika kwa watanzania, kuachana dhana kwamba huduma ya usafiri wa ndege ni ya watu maalum tu na wenye fedha nyingi.

“Zamani biashara hii ilitawaliwa na Wahindi na Waarabu ambao walitujengea hisia na dhana kwamba huduma hiyo ni ya gharama kubwa sana na kwa hiyo ni ya watu maalumu tu. Hii si kweli,  hata Mtanzania wa kawaida anaweza kumudu gharama za usafiri huu,” alisema.

Kwa upande wake, Nyalandu alisema ni azma ya Serikali ya Awamu ya Nne, kuwaandalia Watanzania mazingira bora ya uwekezaji kama ambavyo imekuwa ikifanya, ili kila Mtanzania aliyeko nje na mwenye uwezo wa kuwekeza, aje kufanya hivyo.

Alisema kwa sasa serikali iko katika mchakato wa kuangalia mfumo mzima wa kodi za uwekezaji, ikiwa ni hatua ya kuboreesha zaidi mazingira ya uwekezaji, ili kuwavutia wawekezaji wengi wakiwemo wazawa.

Kampuni hiyo ya Bold imeingiza ndege mbili kwenye soko, moja ikiwa ni ya aina ya Cessna 310 na nyingine aina ya Seneca 1, zote zikiwa na uwezo wa kuchukua abiria sita kila moja kwa wakati mmoja.
Chanzo: Mwananchi

16 comments:

 1. Hivi kweli mtu unaweza ukalalamika kama cha kulalamika hakipo! Hivi kweli unaweza ukapanda mbegu kwenye mwamba...hivi kweli...sijui hebu nyie mliopo nje jibuni shutuma hii, manake mimi nipo ndani nakula vumbi, jibuni kitaalamu!

  ReplyDelete
 2. ok nadhani kama wote tukiwa na "internal connections" tutaweza kuwekeza. Lakini kama wengine tunapiga box all year long halafu vijisenti vyangu nivilete nyumbani kuwekeza kwanza nitafuata njia gani?? na pia ninamjua nani ndani ya "utawala"? Kuleta mzigo tu kwa kawaida ndugu zangu wanalipishwa pesa zadi ya mzigo nilivyonunua. So kama ninataka kuwekeza je wananihakikishia kuwa everything will follow "safe" procedures au mpaka nimjue mtu??? Acheni kutudanganya bwana hayo mengine ni madili yenu wenyewe na sasa mntafuta watu kujifanya kuwa ni mali zao....
  Mdau US

  ReplyDelete
 3. Huyo Ndunguru mwenyewe kasema imemchukua karibu miezi mitatu akizungushwa huku na huko kutafuta kibali kupeleka hivyo vindege vyake viwili. Inaonekana naye hakuwa na mtu anayemjua kwani angekuwa anamjua mtu basi ingechukua chini ya wiki moja.

  Tanzania haitaweza kujikwamua bila kuacha undugu, kujuana, rushwa, ufisadi na ukiritimba usio na sababu.

  Mimi nasubiri fisadi moja linipe pesa nizitumie kuwekeza huko halafu faida tunagawana. Lowassa, Mramba na Rostam, tuwasiliane please. Mimi sintawarusha mabilioni yenu. Nina bussiness proposal tayari.

  ReplyDelete
 4. Nyalandu has a point. Wabeba maboksi wengi kazi yao kulalamika tu kwenye ma-blog lakini la maana hakuna. Wengi hawana makaratasi therefore hawana kitu na wanaogopa kurudi home kwa sababu watakuja kuchekwa na sisi vichaa walotuacha huku na suprisngly tupo tu tunapeta bila noma. Rudini tu washikaji msione aibu kwani yote maisha tu. Who knows pengine mngebakia hapa wengine mngekuwa mshakufa na umeme.

  ReplyDelete
 5. @Kevin: pengine wewe ni fisadi lakini kwa sie tunaojua mifumo mibovu na ya kijinga inayosendesha tasnia yoyote ile!

  Kati ya mawaziri wajinga huyu naye yumo kwa kuwa ni ujinga ulomsukuma kufanya arusi ya zaidi ya TZX 60 milioni...ndio, nasema ujinga kwa kuwa sioni mantiki hapo. Kiukweli, mawaziri wa JK wanaboa na kati ya alowateua wenye mvuto kwa wananchi nikiwamo mie ni 3 tu!

  Hivo sishangai anachokisema huyo jamaa. Wanapenda sana kuzungumzia matukio kuliko issues!

  Ni hayo tu.

  Wako: Ihayabuyaga!

  ReplyDelete
 6. Wengine wanajishaua kwambawanaipenda nchi hii. Huko waliko wanavaa hadi chupi za bendera ya taifa lakini ukiwauliza uzalendo wao uko wapi hawana la kusema. Hawakutaka kurudi huku kwa imani kwamba maisha huku ni jehanamu, lakini watu waliomaliza nao shule pamoja na wakabaki TZ mambo yao ni bomba wanamiliki usafiri na mijengo wao wakirudi hufikia nyumba za wazazi wao ama ndugu zao. Ni aibu kwenu enyi mjiitao wawbeba mabox kwani mna tofauti gani na wale wanaosema ni bora kuzaliwa hayawani ughaibuni kuliko kuzaliwa binadamu Afrika. Acheni hizo. Mtavaa sana chupi zenye bendera ya nchi mlizotoka lakini ndani ya miyoyo yenu ni wababaishaji tu, msijipendekeze mkajifanya mna mapenzi na uchungu na nchii hii. Sijasikia hata mmoja wenu kachangia ujenzi wa shule yoyote ama ununuzi wa madawati kijijini kwao.

  Kwani nyie mnatofauti gani na mafisadi waliopo TZ? Mmesomeshwa kwa hela ya walipa kodi na hata kurudisha hela ya mkopo mliosomeshewa hamjarudisha eti mnajishauwa kwamba mnabeba mabox huko kwani wakati mnachukua mikopo na kusoma vyuo vikuu ilikuwa serikali inawasomesha ili mbebe mabox na kutawaza watoto wa kizungu huko mlipo? Mishipa ya aibu imewakatika?

  Kama ni wazelendo wa dhati unganeni fanyeni kitu cha pamoja tuone matunda yenu si hizi blahblab bum bum for nothing! GUY BE REALISTIC

  ReplyDelete
 7. Wivu tu ndio unaowasumbua watanzania. Kuna haja gani yakuwa na mtizamo hasi kwa watanzania waishio nje. Nyalandu na wenzake akina Kelvin amkeni.

  ReplyDelete
 8. Nyalandu ametuonea tunaoishi ughaibuni kwa kutoa hitimisho la jumla. Hata hivyo tusimchukie wala kumlaumu kutokana na kulewa madaraka yatokanayo na kujikomba kwa Salma Kikwete. Bahati mbaya sana. Nyalandu anadhani watu wote ni walalamishi wasio na sababu. Anasahau kuwa ukiona watu wanalalamika ujue kuna tatizo. Hivi tukimuuliza yeye alipochimba hiyo shs. 60,000,000 ya kufanyia harusi na nyingine zisizojulikana za kukodisha helkopta atajibu nini zaidi ya kujing'ata?
  Ni vizuri wote wenye mawazo mgando kama ya Nyalandu kuelewa kuwa si wote tuishio nje tunabeba mabox au tulikuja kwa njia za panya na hatuna elimu ya kutosha. Tuna taaluma zetu na tumeongeza na kuishi vizuri. Isitoshe hatuiishi kwa kutegemea ufisadi na ukatili kwa halaiki kama ilivyo sasa nchini mwetu kwa wenye madaraka akiwamo Nyalandu. Ila Nyalandu afahamu kitu kimoja-madaraka yanalevya na yana mwisho na mwisho ukifika atajikuta amepigwa butwaa asiamini aliyowahi kupayuka.
  Kama Nyalandu anawalenga wenzake waishio nje walioamua kujigeuza mbwa koko kwa kujikomba kwa CCM na kufungua matawi kila mahali hiyo shauri yake. Heri awambie kama wana uchungu warejee huko wakafanye siasa zao badala ya kujificha ugenini na kujikomba kwa Chama Cha Mafisadi.

  ReplyDelete
 9. Napenda kumjibu anony. wa December 15, 2010 10:20 AM kama ifuatavyo:

  (1) Upendo kwa Tanzania: Ni haki yetu kama waTazania. Hata tuvae chupi za Tanzania na kupeperusha bendera ya Tanzania ni sawa. Ni haki yetu hii na kamwe haistahili kusailiwa unless kama nawe ni fisadi au mtoto wa fisadi ambaye bado unadhani kuwa Tanzania ni yenu na mnaweza kufanya as you like. Mambo yameanza kubadilika yakhe na soma alama za nyakati. Tanzania ni yetu sote hata kama tuko huku nje tukitafuta maisha!

  (2) Kuhusu kununua magari na kujenga nyumba Bongo: Pengine nianze kwa kukuuliza kwamba, wewe una nyumba na gari ughaibuni mf. hapa Canada ninapoishi? Kama huna, ni logic gani
  inayokufanya uamini kwamba Mtanzania aliyeamua kuishi ughaibuni ni lazima awe na gari na nyumba Tanzania? Kwa nini unafikiri ni lazima tuwe na usafiri na kujenga nyumba huko wakati hatuna mpango wa kurudi?. Kama mimi naishi hapa Canada na familia yangu, kwa nini unataka ninunue gari Tanzania? Nimwachie nani? Nyumba nijenge halafu iweje? Nyumba niliyomjengea baba kijijini Tanga nadhani inatosha kabisa. Binafsi hata kama ningekuwa nakaa Dar sidhani kama ningenunua gari kwani hakuna hata mahali pa kuliendeshea. Halafu, ni kweli pia kwamba nyote mliobakia Bongo mna nyumba na magari?

  (3) Kuhusu ajira kwa washikaji niliosoma nao: Kwanza washikaji wengi niliokuwa nao sekondari wengi wameshaondoka na UKIMWI. Waliobakia wengi wao wanabangaiza maisha ya Bongo tu kama kawaida. Wengi wamejibanza katika NGO zisizo na mbele wala nyuma na wengine hawana ajira kabisa. Pengine hujui shida ya ajira ilivyo kali kwa wahitimu wetu wa vyuo vikuu. Tatizo ni kwamba elimu inayotolewa haiwapi vijana uwezo wa kujiajiri na ajira zenyewe zinatolewa kwa kujuana. Kama jina lako linaishia na Makamba au Nnauye basi utajichagulia ajira na hata u-DC utaupata lakini kama wewe ni mtoto wa mkulima kama mimi ndiyo imekula kwako. Kwa ujumla marafiki zangu tuliokuwa nao na ambao wamefanikiwa kujenga nyumba na kujinunulia magari hawazidi watatu na wengine wapo tu wanachacharika. Kwa hivyo hilo dai lako kwamba eti nyote mlioamua kubakia huko (pengine kwa kukosa nafasi na uwezo wa kutoka nje) mmeukata si kweli. Hili kwangu si neno kwani maisha ni popote tu ali mradi mtu una furaha na ridhiko. Ni lazima mtu anunue gari na kujenga nyumba ndiyo aishi???

  (4) Kuhusu kurudisha mikopo: Nipo tayari kurudisha hizo pesa hata leo lakini kwanza naomba unihakikishie kwamba hizo hela nitakazozirudisha zitaingizwa katika mzunguko na kusaidia wanafunzi wengine. Lakini kama hela hizo zitakwenda kununulia nyumba nyingine ya Lowassa kule London, kamwe sitazilipa na hata mahakamani tutapelekana.

  Mimi binafsi nimejitahidi sana na nimejenga ofisi ya walimu kijijini kwetu, nimechimba kisima cha maji, nasomesha vijana watatu na nina programu inayopeleka vitabu katika maktaba za mashule mbalimbali katika wilaya ya Muheza. Na wewe je, umefanya nini mbali na kuchangia harusi za kifahari za akina Nyalandu (60,000,000), michango ya kampeni za kisiasa na kunywa bia Dar es salaam wakati wazazi wako kijijini hawana hata kisima cha maji wala asprin katika kizahanati chao pale kijijini? Halafu siku ukifa na kupelekwa huko ukiwa katika jeneza la gharama kubwa watu wanakushangaa (japo umeshaKUFA). Inaendelea...

  ReplyDelete
 10. (5) Kwa taarifa yako, wengi wetu tumeamua kukaa huku nje kwa sababu kuu tatu:

  Kwanza ni elimu bora ya wanetu. Elimu Bongo imeoza na hata hizo academy zenu ni bure tu. Elimu ndo urithi bora kabisa kwa watoto wetu na hili, kwa baadhi yetu ni jambo nambari wani kabisa katika maisha yetu. Watoto wangu wawili wanasoma katika shule bora kabisa hapa Canada na elimu wanayoipata ni ya daraja la kwanza, elimu ambayo huko Tanzania pengine ni watoto wa mafisadi pekee wanaoweza kuimudu. Hata wewe unayejifaragua hapa sidhani kama una uwezo wa kusomesha watoto wako Ulaya. Hili la elimu my friend ndiyo sababu ya kwanza ambayo imetufanya wengi wetu tubakie huku - wanetu wasome vizuri na wapate elimu itakayowakomboa.

  Pili ni huduma za afya: Hapa ninapokaa naweza kwenda mwenyewe kwa miguu na nikafanyiwa operesheni ya moyo na hata ubongo bila wasiwasi wo wote. Huo ubabaishaji wa huko nyumbani
  ambako watu wanacheza na maisha ya watu ni vigumu kuzoea ukiingia katika mfumo wa afya wa hawa wenzetu

  (tazama hapa: http://swahilitime.blogspot.com/2010/12/muhimbili-wanahitaji-fluoroscopy-x-ray.html).

  Mungu apishie mbali lakini hata wewe subiri siku moja wewe au familia yako mpatwe na tatizo kubwa la kiafya kama kansa au operesheni kubwa ya moyo ndiyo utajua ni nani anamiliki hiyo nchi. Kama huna uwezo wa kukimbia South Africa au India kutibiwa basi umekwisha my friend na hakuna anayejali. Wakati huo huo hao mabosi wenu hata wakipiga chafya tu wanakimbia London na Marekani kwenda kufanyiwa uchunguzi. Halafu eti unaniambia nirudi, kufanya nini?

  Tatu: Huduma nzuri za kijamii, malipo mazuri ya kazi na hali ya juu ya maisha kwa ujumla. Haya mambo ni self explanatory na sitapoteza muda kuyafafanua. Anony, yuache kutishiana na kutoleana sababu za kitoto hapa. Maisha ni popote na kubakia Bongo kusiwe eti ndiyo kigezo cha uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu. Mara nyingi sisi tulioko huku nje tunafanya mambo mengi zaidi kusaidia jamii yetu kuliko hata nyie mlioko hapo Bongo mkihangaika na kitchen party, send off, miharusi ya kifahari na kunywa bia kila siku wakati wazazi na ndugu zenu mliowaacha vijijini wakiishi katika maisha ya dhiki. Kalagabaho!!!

  ReplyDelete
 11. Mweee,
  sijawahi ku comment hapa but nimekupenda Binti Kombo.
  Asante, japo mi nipo nala vumbi kimwili, lakini kiroho na kimatamanio na kimipango ni mbeba mabox tena kwa sababu hizo hizo tatu ulizosema.

  Yaani!
  Uzalendo huu karibu utatushinda. Sina hata nguvu ya kusema zaidi maana yanayojiri humu nchini mwetu hata kuamini ni vigumu.

  ReplyDelete
 12. Huyo jamaa kachemka kweli kweli nadhani hata akija huko mamtoni ni wa kumtenga tu hajijui anadhani analenga kundi fulani kumbe anajilenga mwenyewe. Amelewa madaraka na anayeona kwamba Tanzania hii ni ya watu kama yeye na wengineo wenye kujipendekeza kwa wakubwa. Hata hivyo ajiangalie kwani atakuja kujutia kwa kauli zake za kukurupuka.

  ReplyDelete
 13. Kweli maisha ni popote aliyosema huyo binti au hata Anony.yana ukweli ndani yake si kwamba binti uko %100 sahihi wala %100 vinginevyo na the same applies to your counter part. Lakini popote tuishipi ifike mahali tujivunie kuwa wa Tanzania na Tanzania itajengwa na sisi wenyewe.

  Kwanini watu hupenda zaidi kuwa Dar? Kutokana na imani kwamba Dar is far better than sehemu watokazo (interior)vivyo hivyo kwa wanaoakaa nje ya nchi sababu na visingizio ni hivyo hivyo. Hata kama mtu ataishi kwa kudhalilika akiwa Dar ama nje ya nchi ilimradi tu moyo wake umeridhika. Yote kwa yote ikiwa hata tu wako ndugu uliowaacha kijijini nawe unaisha Dar au Ughaibuni ni vipi wafurahia na kubeza huduma mbovu wanazozipata? Bado una nafasi ya kubadilisha mambo. Sote tukiungana na tukiwa na moyo wa dhati tunaweza kubadilisha mambo badala la kukaa na kubeza na kusifia mambo ya wenzetu. Wenzetu walithubutu na kufika walipo. Sasa nyie wabarikiwa mlioweza kuyaona hayo mazuri ya wenzetu basi tumbukize nasi ili kwamba tuweze kuifurahia hii dunia.

  Ni wazi kwamba pamoja na mabaya yote ya Tz huwezi kubeba ukoo wako eti ukawapeleka huko uishipo na wengi wenu mkifa hurudishwa huku huku kama waishio mjini na mauti kuwafika na kuridishwa kwao na aibu inayowapata ni sawasawa.

  Kingine kinachoniudhi kwa baadhi yenu muishio huko ni tabia mbaya ya kurubuni wasichana wadogo na wavulana wadogo kuwashawishi kupiga picha chafu zinazoldhalilisha utu kwa maelezo kwamba watapatiwa ujira mnono. Ndo maana tuna wasiwasi na huo u so called uzalendo. Nyinyi kufika na kujifanya MARKETING MANAGERS kwa kuwarubuni vijana wadogo hwo are naive ni mbaya sana na mnatuzalilisha watanzania wenzenu. Hatukatai maisha ni magumu lakini si kwa kuacha nyuchi za watoto wakitanzania wazi ndo tuweze kujenga maisha.

  Tafadhali bado kila mwenye mapenzi mema abadilishe nchi hii kwani itajengwa na sisi wenyewe. Tutaishia tu kusifia mazuri ya Canada na kwingineko huku kwetu kunaangamia? Tuamke bado nafasi ipo as long as tunapumua.

  Ciao

  ReplyDelete
 14. @Anony. wa mwisho (December 17, 2010 9:47 AM);

  Naona ulikuwa unajaribu kutumia Core-Periphery model katika hoja zako lakini ukafika mahala ukakwama na hoja zikaanza kudandiana.

  Sina wasiwasi na kusifia ya wenzetu kama nasi tutajibidisha na kuyafikia ingawa kusema kweli sina matumaini sana. Nchi yetu inaendeshwa kibinafsi na inafaidiwa na watu wachache tu nasi tumekaa na kuchekelea mambo ya kitchen party na bashasha za kitoto. Nchi yetu ni tajiri sana na kama kweli tungekuwa na viongozi makini leo hii tungekuwa wapi? Ni kweli kungekuwa na mtoto anayekalia jiwe darasani? Ni kweli tungekuwa na wanawake wanaotembea maili sita kila siku kwenda kutafuta maji ya kunywa? Ni kweli tungekuwa na wagonjwa wanaokufa hovyo kama wanyama kwa kukosa huduma za kiafya?
  Don't get me started my friend. Please don't get me started!!!

  Ajira hizi za kujuana? Leo Tido Muhando amepigwa chini TBC kwa sababu ya kujaribu kutoa usawa katika kurusha kampeni za wagombea wakati wa uchaguzi na hasa kile kipindi cha midahalo ya wagombea majimboni, kipindi ambacho wazee wa kaya walikiona hakifai na wakapiga stop wagombea wao kushiriki? Kweli? TBC ni mali ya nani? Ni nani anayeigharamia? Ni Makamba?

  http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/7490-tido-mhando-atemwa-tbc

  Hilo la kuwarubuni vijana wadogo kupiga picha za ngono sijalisikia na itabidi nilifanyie uchunguzi zaidi lakini si jambo la kushangaza kutokana na hii globalization. Na sitashangaa kugundua kwamba vijana hawa (naamini wengi wao ni wanafunzi wa shule za sekondari) wanapiga picha hizi kwa kuiga wanayoyaona mtandaoni. Hii nayo ni changamoto nyingine tunayobidi kukabiliana nayo.

  Jambo pekee la muhimu katika hiyo comment yako hapo juu ni hili, na hapa nanukuu "Tafadhali bado kila mwenye mapenzi mema abadilishe nchi hii kwani itajengwa na sisi wenyewe" Hapa nakubaliana nawe kwa ASILIMIA 100!!!

  Kauli hii ya Nyalandu - tajiri wa kutupwa ambaye alikuwa anafanya kampeni zake kwa kutumia helikopita za kukodi pamoja na ile harusi yake ya milioni 60 - ina lengo la kuwagawa Watanzania. Kama nasi tutaingia katika mtego huu na kuanza kuzodoana eti wewe kwa vile unakaa nje na mimi niko hapa Dar Nagida bia zangu basi wewe uliye nje si mzalendo basi atakuwa amefanikiwa. Mimi napenda nimalizie kwa kumkemea. Nyalandu, hebu na ushindwe na ulegee katika jina la Bwana. Na kama alivyosema mwalimu Nyerere, Tanzania itajengwa na wenye moyo - popote pale walipo. Na kamwe haitajengwa na matajiri kama akina Nyalandu ambao hata hatujui utajiri wao wameupataje! Kalagabaho!!!

  ReplyDelete
 15. Bi Kombo pamoja na kuunga mkono hoja zako zenye mashiko, naomba nikuongezee kitu kimoja kwenye nukuu yako toka kwa Mwalimu Nyerere. Ongezea: Tanzania ilijengwa na wenye moyo wenye meno wakaitafuna hadi ikabomoka. Tulioko ughaibuni tusitishwe na wanaotubeza na kutaka turejee kushindana nao kuifisidi nchi yetu. Kila mtu kwa namna yake ashikilie malengo yake. Kwani tulipokuja huku tuliomba ushauri wa akina Nyalandu? Ni hao hao waliofanya kupata pasi ya kusafiria ya Tanzania kuwa rahisi kwa wahindi na wasomali lakini mwiko kwa wazalendo. Leo wanatunyima uraia wa nchi mbili wakati wahindi wengi wanao wa nchi mia kidogo.

  Kwanini kusakama wanaoishi nje ilhali kuna watanzania wanaishi nje ya Tanganyika ambayo ni Dar es salaam? Kwanini Nyalandu kama angekuwa na uchungu asikae kwao Singida alikochaguliwa akaondoe umaskini wa kunuka?

  ReplyDelete
 16. Kazi kwelikweli. Watanzania kweli mnapiga makelele kwenye mablogu !

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU