NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, December 23, 2010

WATONGOZAJI NA WATONGOZWAJI - HEBU SOMENI "UTAFITI" HUU • Tafiti nyingi - hata zile zinazohusu mambo muhimu ya kiafya, kisiasa, kiuchumi na kijamii hufanyika nje; na matokeo yake pamoja na majumuisho mengi yanayotolewa huwa hayaakisi hali halisi ya Afrika. Ndiyo maana mimi huwa nazitilia shaka tafiti nyingi za aina hii. Kwa mfano huwa nashawishika kuamini kwamba pengine unene wa Mwafrika anayeishi kijijini, kula chakula kilichokuzwa kiasili na kufanya kazi za mikono kila siku una tofauti na ule unene wa mtu anayeishi New York katika maisha ya deko huku akila vyakula vilivyojazwa makemikali ya kila aina. Wataalamu wa shibe na tiba mnajua.  
 • Katika mkondo huu huu, utafiti mpya wa kidaku uliofanywa na tovuti ya kimapenzi ya Badoo.com (inayodai kuwa na memba wapatao milioni 90) unasema kwamba eti wanawake katika sehemu nyingi duniani hupenda sana kusifiwa kuhusu uzuri wa midomo yao, ingawa wanawake kutoka sehemu zingine hupenda kusifiwa vitu vingine mbali na midomo.
 • Wanawake wa Kimarekani, Kifaransa, Kiitalia na Kibrazil, kwa mfano, wao hupenda kusifiwa jinsi wanavyovaa wakati wanawake wa Kiingereza hupenda kusifiwa kuhusu uzuri wa miguu yao. Wanawake wa Kihispania wao hupenda kusifiwa kuhusu uzuri wa nywele zao huku Wanawake wa Kijerumani na Kikanada wakipenda kufagiliwa kuhusu unyororo wa ngozi zao. Wanawake wa Kidachi na Kireno wao eti hupenda kusifiwa kuhusu uzuri wa masikio yao.
  • Wataalamu wa Saikolojia wanasema kwamba midomo kushika namba wani haishangazi kwani wanawake hutumia muda mwingi sana wakipamba midomo yao kuanzia tu wanapobalehe; na wamekuwa wakifanya hivyo tangu enzi za Wamisri wa kale.

  • Nilipousoma utafiti huu niliwakumbuka hawa jamaa katika picha ambao niliwahi kuwadokeza hapa. Hapa wanaweza kuwa wanasifia nini? Ati, wanawake wa makabila mbalimbali wanapenda kusifiwa kitu gani? Au pengine ni sifa za ndani na za maana zaidi kama uchapakazi, upole, ukarimu na zinginezo za aina hii (Noeclexis). Watongozaji na watongozwaji leteni data tuzione. Ati, huko facebook nako mambo yakoje? 
  • Utafiti huu unapatikana hapa.

  5 comments:

  1. Wakati naiosoma hii tafiti nikafikiria sana sisi wanadamu tulivyo, kupenda unapenda sababu ya kiungo fulani cha mwili, hii ni kupenda au ni kuvutiwa, au ni kutamani...nilikuwa nawaza tu mkuu

   ReplyDelete
  2. Katika pitapita zangu mtaani nimepata matokeo haya kuhusu hawa dada zetu.
   1. wanapenda kusifiwa uzuri/ukubwa wa makalio yao
   2. wafurahi sana kusifiwa uzuri wa sura zao
   3. wanapenda kuitwa potable/slim lady
   4. uzuri wa macho na sauti zao

   pamoja na mengine mengi, mimi nafikiri kila mwanamke/binti ni mzuri kwa namna yoyote ile aliyonayo. hayo mengine ni maruirui ya kutongozea tu.

   ReplyDelete
  3. NJE YA MADA:
   Comment yangu hii iko nje ya mada. NINAPENDA KUWATAKIA KRISMAS NJEMA KABISA, YENYE FURAHA, AMANI NA UPENDO!
   Kwa muda mrefu kidogo nimekua "mwanachama wa vijiwe mbalimbali-lakini nikiwa anony".
   Ninakiri kwamba kuna mambo mengi nimejifunza kupitia mada zinazopostiwa na pia maoni mbalimbali yanayotolewa na wachangia mada!

   Bwana Mungu Awabariki wote! Amen.
   Arrah, Oslo.

   ReplyDelete
  4. Tafiti zaaina hiii zitazidishia watoto wa watu kuzidi kudanganywa!:-( Mtu anaweza kujikuta anasifia kitu asichopenda kisa kasikia tu vimwana wa nchi fulani ndivyo wapendavyo kusifiwa.

   Lakini hii ya Wadachi na Wareno ya kuhusudu kusifiwa masikio imenikechi ofugadi!:-)

   ReplyDelete
  5. Wanaume wengi wa Kitanzania wanahusudisha matako makubwa basi. Wewe hata uwe na sura mbaya namna gani kama una tako kubwa kama la Wanyakyusa au Wahaya basi ushamaliza. Nenda pale Posta Mpya ukaone jinsi wanavyoyashangaa kila yanayoshuka kutoka kwenye daladala za kutoka Mbagala na Vingunguti!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU