NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, December 7, 2010

ZOFA WANGU ANAZIDI KUCHANJA MBUGA: ASHINDA ZAWADI YA UCHORAJI

 • Mchoro huu umeshinda zawadi bora ya uchoraji na Zofa alikuwa mmojawapo wa wanafunzi wawili tu ambao michoro yao ilichaguliwa kwenda kuonyeshwa katika maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa katika Taasisi ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Florida.

  • Kila mwanafunzi pia alitakiwa kuandika maelezo mafupi na Zofa aliandika maneno haya (chini) kwenye kadi iiyotumwa nyumbani pamoja na barua rasmi. Kama mzazi niliguswa sana na maelezo haya ya malaika huyu wa darasa la kwanza ambaye bado anajitafuta na ndiyo kwanza talanta zake zimeanza kujidhihirisha.
  • Zofa, Mungu Aendelee kukubariki na kukushika mkono binti yangu mwema ili ukaendelee kujipambanua na hatimaye kuwa mwanamke wa shoka atakayeleta athari chanya hapa duniani.

  9 comments:

  1. Hongera sana Shangazi Zofa na pia hongera nyingi sana kwa wazazi/walezi. Na mwenyezi Mungu akubariki.

   ReplyDelete
  2. Mtoto wa nyoka ni nyoka na huo ni unyoka mzuri binti yangu. Hongera baba mtoto kwa kuwa na kichwa kinachochemka. Muhimu mwelekeze kwenye mambo makubwa zaidi ya sanaa. Nielewe. Simaanishi kuwa sanaa ni nzuri. Inaweza kuwa kazi ya ziada baada ya mambo mengine.
   Hongera Zofa ila huo uwe mwanzo tu.

   ReplyDelete
  3. Khaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!
   Hivi wivu ni dhambi? Ama ni CHANZO CHA UTENDAJI WA JUHUDI ILI NAWE UPATE?
   Hapa NIMETAMANI maendeleo haya yasiwe kwako na kwangu tu, bali kwa wazazi wote wema wawekezao kwa wana wao
   HONGFERA MWANA

   ReplyDelete
  4. Ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Wazazi tunatakiwa kuwa karibu na watoto ili tuweze kuwapa mwongozo na mwelekeo chanya. Hongera Zofa, hongera Matondo pamoja na familia yako.

   ReplyDelete
  5. Binti yetu Zofa anaendelea katika njia bora kabisa. Namtakia kila la heri.

   ReplyDelete
  6. Asanteni nyote. Tutazidi kugangamara naye hivyo hivyo na kwa msaada wa Mungu, binti huyu atakua na kuwa mwanamke wa shoka katika cho chote kile atakachoamua kukifanya hapa duniani. Tuko pamoja!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU