
- Hivi karibuni maoni mafupi ya Profesa Mbele kuhusu uzembe wa Watanzania, na uraia wa nchi mbili yalitundikwa katika blogu ya Issa Michuzi. Maoni hayo yalichangamsha watu sana na kama ilivyo kawaida, hoja za msingi ziliachwa na Profesa Mbele akaanza kuandamwa binafsi tena kwa matusi, kejeli na dhihaka (Nilishaligusia jambo hili hapa). Baada ya kuyasoma maoni hayo ya wachangiaji 76, nilianza kujiuliza maana hasa ya msomi. Ati jamani msomi ni nani? Ni lazima kuwa na shahada kuwa msomi? Vipi kuhusu babu jirani yetu kule kijijini (mganga wa kienyeji) anayefahamu karibu kila mti na matumizi yake tena bila kutumia daftari kuwekea kumbukumbu? Je, yeye ni msomi? Wewe ni msomi? Kuna faida ya kuwa msomi?

- Hapa chini ni maoni wakilishi ya mitazamo tofauti ya wadau mbalimbali kutoka kwa Michuzi kuhusu dhana hii ya "usomi"
**************************
(1). Tarehe Tue Feb 09, 07:14:00 PM, Mtoa Maoni:
- Prof, Kuhn-Tucker conditions unazijua wewe?? super and submodularity je?? Je, vipi kuhusu maximum principle na calculas of variations (CV). Niambie unawezaje kujua iwapo a twice differentaible function ni concave au ni convex!! Baada ya hapo naomba u-state transversality condition ya Infinite Horizons model!! Ukimaliza hapo nieleze matumizi na umuhimu wa ARCH and GARCH models especially as applied to high frequency financial data, kabla ya kumalizia na maelezo kuhusu procedures zilivyo katika ku-conduct augument dickey fuller test (ADF) na short comings zake. Ahsante
- Kidokezo changu: Kwa huyu mdau, huwezi kuwa "msomi" na kuweza kuanzisha wala kushiriki mjadala kama hukusoma kozi za juu za Uchumi na hatimaye kuweza kujibu maswali anayoyauliza hapa. Sina uhakika ni watu wangapi wanaweza kuyajibu maswali haya na hivyo kuonekana "wasomi". Je, tuupime usomi wa mtu kwa kuangalia uwezo wake wa kujibu maswali tata katika taaluma yake aliyosomea? Huyu mdau akiulizwa maswali kutoka katika taaluma zingine ataweza kuyajibu? Au pengine "Economics" ni taaluma bora kuliko zingine zote?
(2). Tarehe Tue Feb 09, 12:12:00 AM, Mtoa Maoni:
- Huyu ni Professor wa kiswahili, I wonder anajifanya anaijuwa siasa na uchumi! Ni miongoni mwa wale wanaodhani kujipendekeza sana kwa Kikwete basi huenda wakapata hata ubunge wa kuteuliwa!!! Nna mashaka na u professor wake! Na daima ntaendelea kuwa hivyo! Uwezo wake wa kufikiri na kujenga hoja hauna tofauti na Baba yangu aliyeshia darasa la nne la mkoloni! Of coz sikutegemea kusikia mchango wa maana kuhusu uchumi kutoka kwa Professor wa Mofimu, virai, viima na viarifu (kiswahili), lakini nilitegemea angalau anyamaze au afunguwe blog afundishe watanzania Kiswahili! Unapopiga kelele watanzania wanapiga soga wakati huna statistical data na wewe kama Professor si aibu hiyo, una tofauti gani na hao unaowalaumu (wapiga soga)...uliozungumza ni mazungumzo ya maandazi tu! Tanzania ina hasara sana kama ina Professors wa aina hii! Na kama huu ndo u professor, mungu mie usinijaalie kamwe kuwa professor!
- Kidokezo changu: Fundi Mangungo haamini kama mtu aliyesoma lugha anaweza kuanzisha mjadala wala kutoa mchango wa kitaalamu na wa kina katika mada zingine nje ya mofimu, virai, viima na viarifu! Vipi kuhusu mtu aliyesoma Jiografia, Udaktari, Fizikia, Historia, Sayansi ya Siasa au Kemia? Anaweza kutoa mchango wowote wa maana katika mijadala nje ya uwanja wake wa kitaaluma au pengine upungufu huu ni kwa "vilaza", "ngwini" na "mbumbumbu" waliosoma lugha tu? Tazama pia maoni kama haya ya Fundi Mangungo hapa.
(3). Tarehe Tue Feb 09, 12:43:00 PM, Mtoa Maoni: MADELA WA-MADILU
- Professor Mbele, Heshima mbele mkuu mwenzangu. Kama una nia ya kutumwagia matusi sisi akina MADELA WA- MADILU njoo pale kwenye jamvi. Wote tuko hapa Marekani tunaganga njaa, shule tumepiga kisawasawa lakini si wote shule zetu zinafanana na kufundisha kiswahili. Hesabu za majoka (Calculus) na Ngeli wapi na wapi???

- Kidokezo changu: Pengine kusoma hesabu za majoka (calculus) ni bora kuliko kusoma ngeli; na kufundisha hisabati ni bora kuliko Kiswahili. Pengine pia ni kweli kwamba mtu aliyesoma hesabu za majoka ni msomi kuliko aliyesoma ngeli. Na hesabu ni bora kuliko lugha!!!
*********************
Kulikuwa pia na maoni makini ambayo yalizingatia hoja. Mfano ni maoni ya Mdau Mkweli (Tue Feb 09, 01:49:00 AM) na ya mdau wa Tue Feb 09, 12:15:00 AM.
- Turudi tena kwenye fikra yetu ya leo: Kwako wewe msomi ni nani? Unaweza pia kusoma hadithi hii fupi kuhusu dhana hii ya usomi.
