NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, August 31, 2010

WAKATI WA "KUWAFURAHISHA" WAPIGA KURA NDIYO HUU!!!




Monday, August 30, 2010

WASUKUMA NJOONI HUKU TUJICHEKE: TUMETANIWA NA MHEHE!!!


CHEKA UNENEPE.

Msukuma mmoja alibahatika kwenda zake Uingereza, baada ya kufika alishangaa uzuri wa mji na majengo ya kushangaza.

Ili akirudi Tanzania awakonge wenzake kila alichokiona alitaka kujua kinamilikiwa na nani. Cha kwanza kuuliza kilikuwa kujua uwanja ule wa ndege unamilikiwa na nani. Alimuona Mzungu mmoja amesimama alimfuata na kumuuliza.

“Eti uwanja huu wa ndege ni wa nani?”
Speak English,” Mzungu hakumuelewa na kumuomba azungumze Kiingereza.

Jamaa baada ya kuelezwa vile aliondoka akiamini anayemiliki ule uwanja ni Speak English. Alipoondoka pale alikwenda hoteli moja kubwa na kuulizia ile ni ya nani, aliyemuuliza kwa Kiswahili hakumuelewa alimjibu “Speak English.”

Kila kona alielezwa vile, basi jamaa aliporudi Tanzani aliamini Speak English ndiye tajiri mkubwa nchini Uingereza. Kila kona aliwaeleza jinsi kila kona alipouliza watu kuhusu mmiliki wa vitu vya thamani aliambiwa Speak English.

Watu walimcheka na kumueleza Speak English siyo tajiri bali walimueleza azungumze Kiingereza kwa vile walikuwa hawamuelewi akizungumza kiswahili. Mmh, hii kali kujua lugha nako raha. 
Aliyetutania hivi anapatikana hapa.
*******************

Sunday, August 29, 2010

USHINDI UNAKUJA ATI!


Inaonekana CCM wamefanya "kufuru" kwa kununua "nyuso" hizi za magazeti ili kujitangaza. Ukiwa na vijisenti vyako haliharibiki neno ati! Kama nilivyosema jana, wapinzani kazi mnayo! Picha ni kutoka kwa Mjengwa.

Saturday, August 28, 2010

Friday, August 27, 2010

FIKRA YA IJUMAA: ARGUMENTUM AD HOMINEM

  • Argumentum Ad Hominem ni dhana muhimu katika taaluma ya Lojiki na Mantiki. Dhana hii hutumiwa kuelezea mashambulizi au hoja ambazo zinaelekezwa kwa mtu binafsi (mf. mwanasiasa) badala ya kumakinikia kile akisemacho (mf. sera zake). Pengine mifano bora kabisa ya Argumentum Ad Hominem niliwahi kuigusia hapa na hapa
  • Ingefurahisha kama nini kama wakati huu wa uchaguzi tungeacha kuwashambulia wagombea binafsi na badala yake tukamakinikia sera zao kombozi kwa jamii. Ati, kati ya wagombea wote wa urais, ni yupi mwenye sera zenye mashiko na zinazotekelezeka? Ni yupi ambaye ana uchungu na maisha ya Mtanzania wa kawaida? Ni yupi ambaye ameonyesha moyo wa kizalendo na kutetea sera zake kombozi, hata kama kwa kufanya hivyo imebidi afarakane na maswahiba wake? Yupi ni kiongozi bora ambaye ataisadia Tanzania kusimama kidete na kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania??? Kiongozi wa aina hii ndiye tunayepaswa kumchagua.
  •  Tuogopeni ARGUMENTUM AD HOMINEM kama ukoma!
Wikiendi njema

WAALIMU KAZI TUNAYO......

Thursday, August 26, 2010

CUF NA UBUNIFU WAO

USIKONDE. HATA "MAJUU" KUNA KUNGUNI KIBAO NG'WANAWANE !!!

Picha hii inapatikana hapa.
  • Marekani sasa inakumbwa na tatizo kubwa la kunguni na Jiji la New York ndilo linaongoza kwa kuwa na kunguni wengi huku likifuatiwa na Philadelphia, Detroit, Cincinnati, na Chicago. Kwa majiji mengine yanayoongoza katika sakata hili bofya hapa. Wataalamu wengi wanasema kwamba kunguni sasa limekuwa tatizo la kitaifa hapa Marekani na serikali kuu ya shirikisho imeshaombwa kusaidia katika baadhi ya sehemu zilizoathirika zaidi. 

MWALIMU ANASWA AKIJIANDAA KUFANYA NGONO NA MWANAFUNZI

  • Mwanafunzi asimamishwa masomo, lakini mwalimu wake aachwa akipeta
Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ya wasichana Maswa Chacha Mussa (28) amekutwa na mwanafunzi wake wa kidato cha tatu (jina tunalihifadhi) mwenye umri wa miaka (16), wakijiandaa kufanya mapenzi.

Tukio hilo lilitokea Agosti 7, mwaka huu saa 7:45 mchana baada ya uongozi wa shule hiyo kupata taarifa kwamba mwalimu Chacha alikuwa nyumbani kwake na mwanafunzi.

Baada ya taarifa hizo, Mkuu wa Shule Msaidizi, Paschal Athanas na mwalimu wa zamu waliamua kwenda nyumbani kwa mwalimu na kumbamba akiwa chumbani kwake na mwanafunzi huyo.
Aidha, kutokana na tukio hilo mwanafunzi huyo amesimamishwa masomo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuruhusu uchunguzi kufanyika.

Hata hivyo, mwalimu wake bado anaendelea na kazi ya kufundisha kama kawaida na hakuna hatua yoyote ya kisheria ikiyochukuliwa dhidi yake.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kamishina Msaidizi Daudi Siasi alisema kuwa baada ya tukio hilo kutokea polisi walipewa taarifa na kwenda kwenye shule hiyo ambapo mwanafunzi huyo alipelekwa kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya serikali ya wilaya ya Maswa na kuonekana kuwa alikuwa hajafanyiwa kitendo chochote na mwalimu huyo.

CHANZO: NIPASHE (25/8/2010)

Wednesday, August 25, 2010

CCM NA UBUNIFU WAO

  • Tovuti ya Mgombea wa kiti cha Uraisi (Mh. J.K)







Kwa ubunifu mwingine, bofya hapa.

CHADEMA NA UBUNIFU WAO

  • Na hapa hatujataja magwanda ya Kipiganaji na helikopita. Kazaneni!







KUANZIA MWAKA HUU WA MASOMO NGUO ZA SHULE NI LAZIMA HAPA NINAPOISHI

 Mabinti: Kija, Minza na Sumayi
  • Baada ya kuchoshwa na mitepesho, wanafunzi kujitoboa masikio, pua, midomo, ndimi na sehemu nyinginezo; na mashindano ya fasheni mpya za nguo mashuleni, hatimaye Wilaya ya Alachua (hapa ninapoishi) imeamua kwamba kuanzia mwaka huu wa masomo ulioanza juzi, wanafunzi wote wa shule za umma ni lazima wavae sare za shule. 
  • Hapo juu mabinti ndiyo mara yao ya kwanza kuvaa nguo za shule na walikuwa wanashangaa kweli. Wao wanataka wavae nguo za akina Hanna Montana, iCarly na wenzi-rika wao wengine wanaowaona kwenye runinga. Wao wanataka nguo na viatu fasheni mpya mpya ili "wapendeze". Ilibidi kuwakalisha chini na kuwaelimisha umuhimu na faida za kuvaa nguo za shule. 
Sumayi: shule ya vidudu
  • Niliwaambia kwamba, nguo za shule kwanza zinapendeza - hoja ambayo waliikataa katakata. Pili, zinatupunguzia mzigo sisi wazazi wa kununua nguo za shule mara kwa mara kulingana na fasheni mpya zinazovaliwa na marafiki zao shuleni. Niliwaambia kwamba tulikuwa tunapoteza pesa nyingi sana (hoja hii waliikubali) Tatu, nguo za shule zinasaidia kuondoa tofauti ya matabaka kwani kwa sasa watoto wa masikini wasio na uwezo wa kununua nguo za akina Hanna Montana na watoto wa matajiri watakuwa wanavaa nguo za aina moja. Kwa hivyo hakuna kuchekana (hoja ilikubaliwa). Nne, nguo za shule pia zinawatambulisha kuwa wao ni wanafunzi na kuwa mwanafunzi ni jambo la kujivunia (hoja ilikubaliwa nusunusu).
Minza - darasa la kwanza
  • Tano niliwaomba wanipe maoni yao kuhusu suala la wanafunzi wenzao wanaotoboa pua na midomo. Walisema kwamba hawapendi na walikuwa wanashangaa sana wanapoona mwanafunzi amejitoboa. Niliwaambia kwamba sasa kujitoboa kumepigwa mafuruku na kuvaa mikufu na mazagazaga mengine kumepigwa marufuku. Kuvaa nguzo zinazolegea (mitepesho) pia kumepigwa marufuku. Hata viatu vyenye magurudumu na mapambo nje navyo haviruhusiwi. Walipenda na kufurahishwa sana na mabadiliko haya mapya na maoni yao mwishowe yalikuwa ni ya kuunga mkono.
 Minza na Sumayi
  • Mpaka mwisho wa mkutano wetu naona nilikuwa nimeshinda na kila mtu alikuwa na furaha. Nyumbani mimi hata sikuwahi kujiuliza ni kwa nini tulikuwa tunavaa nguo za shule. Pamoja na kwamba kulikuwa na upinzani mkali kuhusu sera hii mpya (wazazi wakereketwa walikuwa wanadai kwamba uhuru wao unaminywa), nimefurahi kwamba hatimaye imepitishwa kwani ina faida nyingi kama ambavyo nimegusia hapo juu.

Tuesday, August 24, 2010

WANAWAKE SOMENI UTAFITI HUU KUTOKA HARVARD

  • Hizi ni habari nzuri kwa wanawake. Utafiti mpya uliofanywa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Harvard na kuchapishwa tarehe 17/8/2010 katika jarida la Circulation: Heart Failure unaonyesha kwamba kula chokoleti nyeusi yenye wingi wa kakao angalau mara tatu tu kwa mwezi kunaweza kuzuia magonjwa ya moyo kwa wanawake
  • Kula chokoleti nyingi (mfano mara mbili kila tu wiki) hata hivyo hakusaidii cho chote na kunaongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kwa asilimia 23. 
  • Katika utafiti huu watafiti hawa walizichunguza tabia za ulaji wa chokoleti nyeusi za wanawake 31,823 wa Sweden wenye umri kati ya miaka 48 na 83. Matokeo yanaonyesha kwamba kwa wanawake ambao walikula chokoleti nyeusi kidogo (gramu 20 - 30) mara tatu kwa mwezi, uwezekano wao wa kupata magonjwa ya moyo ulipungua kwa asilimia 32. 

  • Kwa habari zaidi kuhusu utafiti huu bofya hapa. Makala kamili ya utafiti huu yanapatikana hapa (pdf)

UTAINGIA KULA KWENYE HOTELI YENYE WAFANYAKAZI WALIOVAA NGUO ZENYE UJUMBE HUU?


  • Halafu kwenye jumba la makumbusho kumbe kulikuwa na Reggae usiku ule. Nilimkumbuka Mzee wa Changamoto.

Monday, August 23, 2010

KWELI YOTE HAYA NI KWA AJILI YA SIMU? KUNA TATIZO KATIKA JAMII YETU

Huyu "kibaka" eti ALITUHUMIWA kumwibia simu abiria mmoja aliyekuwa kwenye daladala lililokuwa likitoka Tandika kuelekea Mwenge.
 ************
(1) Raia mwenye hasira akimtwanga tofali


(2) Kijana hoi bin taabani


(3) Baadaye anafumbua macho na kuomba msaada

(4) Mgambo wanafika na kumwokoa

  • Kama nilivyosema katika maoni yangu kuhusu jambo hili katika blogu ya Pwani Raha, hili si jambo la kufurahia. Hii ni dalili wazi ya ndwele angamizi na nyemelezi ambayo inatutafuna kimya kimya huku tukijinadi kwamba tunaishi katika nchi ya amani. Watu wana hasira na ipo siku hasira hii itaripuka tu tutake tusitake. Tatizo ni kwamba wamiliki wa mfumo wanaonekana kutojali, pengine kutokana na ukweli kwamba wanaosulubishana kwa hii staili ya haki ya papo kwa papo ni walalahoi kwa walalahoi. 
  • Walalahoi hawa wakiamka siku moja na kuacha kubondana matofali wao kwa wao; kisha waelekeze hasira zao kwa wamiliki wa mfumo itakuwaje? Historia inaonyesha kwamba hatua hii ikifikiwa, hakuna jeshi hapa duniani linaloweza kurekebisha mambo. Tujihadhari!
NYONGEZA
Kibaka mwingine huyu hapa akichomwa moto!!!

  • Picha zote ni kutoka Global Publishers
Nyongeza

Tukio la hivi karibuni kule Musoma

Sunday, August 22, 2010

SAFARI HII NAONA "VIJANA" WAKO MACHO

  • Gari la Mheshimiwa lilipogoma kuwaka kipindi kile baada ya kuwekewa mafuta yaliyochakachuliwa, watu walishangaa na kulalamika kuhusu ulinzi wa Mheshimiwa. Kelele za wasiwasi kuhusu timu ya ulinzi wa Mheshimiwa pia zilipigwa baada ya gari lake kuchomoka tairi akiwa msafarani. 


  • Katika tukio hili la jana pale Jangwani naona "vijana" wako makini sana na walimdaka mapema.  Picha hii inatosha kabisa kuwaondoa hofu wale wote ambao walikuwa na wasiwasi kuhusu ulinzi wa Mheshimiwa. Poleni wanaCCM kwa mkasa huu. Nilikuweko jangwani mkasa kama huu ulipotokea mwaka 2005! 
  • Kwa habari zaidi tembelea blogu ya Pwani Raha. Tunampa pole Mheshimiwa pamoja na wanaCCM wote kwa mkasa huu. Mungu Ibariki Tanzania!

Friday, August 20, 2010

FIKRA YA IJUMAA: MASHARTI HAYA YA VIONGOZI YALIKUWA MTEGO WA RUSHWA???

Angalizo: siungi mkono rushwa lakini naomba tuliangalie swala hili kwa jicho la kibinadamu huku tukizingatia hulka na mahitaji ya binadamu kama mnyama!
**************
  • Masharti ya viongozi kama yalivyoainishwa katika Azimio la Arusha yanasema hivi:
VIONGOZI

1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au kikabaila.

2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.

3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.

4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi

5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
***************
  • Kimsingi kilichokuwa kinasisitizwa hapa ni kwamba, ili mtu aweze kuwa kiongozi (wa ngazi ya juu), ilikuwa lazima awe masikini. Kwa hulka ya binadamu wa kawaida (ukitoa akina Mother Thereza, Mahatma Gandhi na wengineo), umasikini na madaraka vinagongana. Wanasaikolojia wengi wanasema kwamba lengo la binadamu ni kujiendeleza na kujipatia uwezo wa kujipatia mahitaji yake katika viwango mbalimbali kwa urahisi.  Kama hivi ndivyo; ni wazi kwamba ni vigumu sana kwa mtu masikini kupewa madaraka makubwa mf. uwaziri au ukurugenzi wa shirika la umma na asiitumie nafasi hiyo kujiendeleza yeye na familia yake.  
  • Maswali: Lojiki ya masharti haya ya TANU ilikuwa ni nini? Je, hawa viongozi walitakiwa kuwa watakatifu na kuzikana hulka zao za kibinadamu? Masharti haya yalisaidia kuchochea rushwa kwa viongozi hawa masikini kuanza kuiba kisirisiri?
  • Katika nchi nyingi zilizoendelea, huwezi kugombea nafasi ya juu kama uko masikini; na nafikiri mfumo huu pengine unasaidia kuzuia hizi rushwa za mara kwa mara ingawa nao pia, (kutokana na uchoyo na tamaa) wanaiba na kula rushwa.
  • Mwisho: Masharti haya yalikuwa ni mtego usioepukika kwa viongozi hawa masikini?Ungekuwa wewe ungeuepuka?

MSICHANA WA SURA NZURI SANA - NA DAUDI KABAKA

  • Hapa sina la kusema

Thursday, August 19, 2010

MAMA YUPO KWENYE NDEGE, MTOTO ANALIA, MAMA KABEMBELEZA KACHOKA, AKAAMUA KUMZABA MTOTO KIBAO, ABIRIA WAKALALAMIKA...SASA ENDELEA

 Picha hii iko hapa.

****
...mfanyakazi wa kwenye ndege akamchukua mtoto,
Baada ya ndege kutua polisi wakaitwa,
wazazi wakahojiwa,
wakaonekana ni wazazi wazuri,
Wakaachiliwa na kuruhusiwa kuendelea na safari yao,
Na "ishu" ikamalizika.

Kuna la kujifunza hapa?

*********

Kwa habari kamili kuhusu kisa hiki soma hapa.

TUSIENDESHE HUKU TUKITUMA UJUMBE KWENYE SIMU ZETU. NI HATARI !!!

  • Baadhi yetu hatuwezi kujizuia kutuma ujumbe mfupi kupitia simu zetu kwenda kwa marafiki au kuweka katika kurasa za facebook na twitter. 
  • Kama vile nilivyowahi kuonyesha hapa, wanasayansi wameshathibitisha kwamba tabia hii ni ya hatari zaidi kuliko hata kuendesha ukiwa umelewa pombe au bangi. 
  • Suala hili limezuka tena baada ya daktari mmoja wa watu maarufu aitwaye Frank Ryan kuporomoka na gari lake na kufariki kule Malibu. Malibu ni sehemu ya milima mingi na barabara nyingi ni nyembamba na zenye kona kali. 
  • Polisi wamethibitisha kwamba, daktari huyu alikuwa anatuma ujumbe katika akaunti yake ya twitter juu ya mbwa wake kabla ya gari lake kuacha barabara na kuporomoka kwenye makorongo milimani. Daktari alifariki hapo hapo lakini mbwa wake alipona. Kwa habari zaidi kuhusu habari hii bofya hapa.

TUWE WAANGALIFU !!!

UREMBO - DHANA TATA AJABU

Video hii ni mwendelezo wa maangalizo juu ya dhana ya urembo yaliyowekwa hapa. Tusilazimishane kwamba eti mwanamke mrembo ni lazima awe kimbaumbau!

video

Wednesday, August 18, 2010

NILICHOJIFUNZA BAADA YA KUFUNDISHA HESABU WATOTO WA DARASA LA TATU HAPA MAREKANI

Picha hii inapatikana hapa.
  • Kama ambavyo niliwahi kudokeza katika maoni hapa, mwaka uliopita wa masomo (Agosti 2009 – Juni 2010) nilikuwa ninajitolea kufundisha hesabu wanafunzi 19 wa darasa la tatu hapa Marekani kwa masaa mawili kila wiki. Shule niliyokuwa nafundisha ni shule nzuri yenye wastani wa daraja la A (hapa shule hupewa alama A-F kulingana na mafanikio ya wanafunzi katika mitihani mbalimbali ya kijimbo, na vigezo vingine).
  • Lengo langu hasa la kujitolea kwangu, mbali na mwenyewe kujifunza na kujipatia ridhiko la kisaikolojia, lilikuwa hasa ni kujua mbinu zinazotumiwa na wenzetu katika kufundisha watoto wao hesabu na masomo mengine ya sayansi, masomo ambayo kule nyumbani yanaogopwa sana na wanafunzi na yamekuwa yakididimia mwaka hadi mwaka. Nilichagua hesabu kwa sababu ndiyo somo mama na lisiloepukika karibu katika kila nyanja hapa duniani (bofya hapa).
Kwa kifupi, mambo makuu niliyojifunza ni haya:
  • Hesabu hazifundishwi kavu kavu kama hesabu bali zimeingizwa na kuoanishwa na michezo ya namba katika kompyuta, vitabu mbalimbali, michezo ya watoto na hata nyimbo wanazoimba, ikiwemo kutunza na kuhesabu akiba zao za pesa (kila mtoto hutakiwa kujiwekea akiba katika kikopo na kuweka rekodi daftarini). Kwa hivyo watoto wanajifunza dhana za msingi kama kujumlisha, kutoa, kuzidisha na hata kugawanya kwa urahisi zaidi. Kati ya wanafunzi 19, ni wanafunzi wawili tu ambao walikuwa wakilalamika kwamba walikuwa hawapendi hesabu.
  • Badala ya kuzifanya hesabu kuwa somo kavu na lenye kuogopwa sana, kumbe inawezekana kulifanya liwe la kuvutia na hata kusisimua. Tofauti ni kwamba walimu hawa wana karibu kila kitu wanachohitaji na huwezi kuwalinganisha na walimu wetu ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu sana.
  • Kuna utaratibu mzuri sana wa tuzo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri karibu katika kila kitu darasani – kuanzia yule anayefanya mazoezi yake yote kwa wakati unaopangwa, kusaidia wenzake darasani, kujibu maswali kwa usahihi (na kwa haraka), kufanya miradi mizuri na mambo mengineyo. Tuzo hizi huwasisimua sana wanafunzi kwani wazazi pia hushirikishwa.
  • Wazazi ni sehemu muhimu ya elimu ya watoto wao. Wazazi hupewa barua na kuombwa kuwasaidia watoto wao katika kufanya kazi za nyumbani kwa kuhakikisha kwamba wanafahamu dhana inayolengwa katika kila zoezi la nyumbani. Hapa mtoto hawezi kufanya vizuri shuleni bila msaada wa wazazi. Kwa hakika kuna jambo la kujifunza hapa hasa kwa wazazi wetu ambao wamewahi kulalamikiwa kwa kutojihusisha kwao sana na elimu za watoto wao.
  • Wazazi pia huchochewa kuhudhuria baadhi ya shughuli za watoto wao shuleni kama michezo ya kuigiza na wakati wa uwasilishaji wa miradi yao ya sayansi na hesabu. Wazazi huja na maua na zawadi mbalimbali kwa watoto wao, picha hupigwa, video huchukuliwa kwa ajili ya kumbukumbu na wanafunzi hupongezwa na kuhongereshwa.  
  • Kuhusu sayansi, watoto huanza kufanya majaribio ya msingi tangu wakiwa bado watoto. Isitoshe sayansi, kama vile hesabu, haifundishwi kavu kavu kama tulivyofundishwa sisi. Wanafunzi wa darasa la tatu kwa mfano huanza kusoma vitabu vifupi juu ya historia fupi juu ya wanasayansi mbalimbali  - walizaliwa wapi na lini, utoto wao ulikuwaje, waligundua nini na kwa nini ugunduzi wao ni muhimu leo. Vitabu hivi huwasisimua sana wanafunzi na si ajabu kukuta wengine wakisema kwamba wanataka kuwa kama Isack Newton watakapokua, wapo wanaoapa kwamba ni lazima watagundua dawa ya kansa n.k. Sayansi, kama vile hesabu, inaweza kuwa somo la kusisimua sana kama ikifundishwa vizuri. Siyo ule mtindo wetu kule nyumbani ambapo tunakariri tu hata bila kuelewa tunakariri nini.
    • Wanafunzi hawa pia, hawana vipingamizi vya lugha kama ilivyo kwetu ambapo kusema kweli tunafundishwa katika lugha ambayo hatuielewi na dhana dhahnia kama vile gravity, atomic weight n.k. inakuwa vigumu sana kuzielewa. Walimu wetu pia nao, pengine kulingana na mazingira duni wanamofanyia kazi pamoja na maslahi yasiyoridhisha kusema kweli hawana muda wa kujaribu vitu vipya darasani mbali na mwongozo wa wizara husika unavyosema. Nilishangaa sana, kwa mfano, binti yangu wa miaka tisa, aliponieleza kwa usahihi kabisa jinsi mzunguko wa maji (water cycle) unavyofanya kazi na kwa nini sayari kama Mars hazina mvua! 
    • Ngoja leo niishie hapa. Mwaka huu nimejitolea kufundisha sayansi darasa la nne (masaa mawili kwa wiki) na lengo langu ni lile lile – kusaidia na hasa kujifunza zaidi mbinu wanazozitumia katika ufundishaji wao. Lengo langu ni kuandika kitabu chenye kutoa maoni na mwongozo binafsi wa ufundishaji wa hesabu na sayansi katika madarasa ya mwanzo katika shule zetu za msingi kule nyumbani!
    Hapa chini ni baadhi ya maswali ya mtihani na mazoezi ya nyumbani kwa wanafunzi wa darasa la tatu. Kwa mtu wa isimu (ngwini) kama mimi, baadhi yake yalikuwa “vigongo”  na ilinibidi nigangamare kweli ili kuyakokotoa!

    ********************** 
      (1) Pam gave her friend Tammy the numbe riddle below. Solve it.

      I am a 2-digit number less than 84. The sum of my digits is 9. The ones digit is twice the tens digit. What number am I?

      (2) Bill was staring across the street where bicycles and tricycles were stored. He counted a total of 13 wheels. How many bicycles and tricycles were in the lot?

      (3) The library at Miller Elementary School has an odd number of tables. Some tables will seat 4 students and some tables that will seat 6 students. A total of 32 students can sit at the tables with no empty seats. What is the number of tables of each type?

      (4) Amanda eats supper from 6:30 to 7:00. Then she watches a half-hour television program. She takes 5 minutes to brush her teeth, 15 minutes to take a bath, and 5 minutes to dress for bed. How much time is left for Amanda to read if she goes to sleep at 8:30?

      (5) A magician weighed his twin rabbits and identical hats together and got 18 pounds. He then weighed one hat and got 3 pounds. What was the weight of one rabbit?

      (6) A turtle crawls up a 12 foot hill after a heavy rainstorm. The turtle crawls 4 feet, but when it stops to rest, it slides back 1.5 feet. How many tries does the turtle make before it makes it up the hill?

      Tuendelee kujifunza na kwa anayetaka maswali zaidi ya hawa watoto wa darasa la tatu aseme….

      Tuesday, August 17, 2010

      WANABLOGU WENZANGU, NIMEULIZWA SWALI "GUMU": TUSAIDIANE KULIJIBU


      Wanablogu msikilizeni huyu mdau. Naliweka swali lake kama lilivyo. 
      **************

      Bwana Matondo. Naipenda blogu yako. Ni one of the blogs ambayo imepangwa vizuri na yenye uandishi wa pekee. Pia umefanya effort kubwa kuzicollect blogs mbalimbali na kuziarrange according to topics. Hii inasaidia kwa sisi tunaopenda kuperuse.

      My big problem/question is this: mbona hukuziweka adult blogs? Kuna za mapenzi na mahusiano but not zile za ngono. Why? After Ze Utamu, ina maana hakuna blogz za ngono za Kiswahili? Au wewe na bloggers wa Kiswahili mnabagua?

      If this is the case, this is NOT FAIR na mko wrong kwani blogz za ngono ndiyo popular. Nenda maofisini, mashuleni, vyuoni na sehemu zingine. Probably katika kila watu 10 walioko online, 8 of them watakuwa wanaangalia ngono. Kwa hivyo acheni unafiki washikaji. Mnavunga hampendi ngono wakati ndiyo waangaliaji wakubwa. Hivyo please add adults blogz za ngono kwenye list yako ili mambo yaende vema. Nitashukuru sana na natumaini hutaignore hii concern yangu anbayo naamini ni ya wadau wengi tu.

      Ni mimi mdau mkuu wa blogu yako

      J. Konga (a.k.a Mzee wa Mikong'oli) 
      Buguruni.

      HAWA NDIO WAGOMBEA RASMI WA UBUNGE (CCM) MKOA WA SHINYANGA (NA KWINGINEKO)

      Kama nilivyotegemea, mbunge wangu mpendwa ameshinda tena! Kule Mbeya, hata hivyo, Mwakalebela ametemwa kwa sababu ya tuhuma za rushwa wakati wa kura za maoni. CCM Oyee !!!

      ***************************
        14.MKOA WA SHINYANGA
         
        (i) Shinyanga Mjini: Steven  Julius  Masele
        (ii) Kishapu: Nchambi Seleman Masoud
        (iii) Kahama: James Daud  Lembeli
        (iv) Msalala: Maige Ezekiel Magolyo
        (v) Solwa:  AhmeD Ally Salum
        (vi) Bukombe: Emanuel Jumanne Luhahula
        (vii) Mbogwe: Masele Agustino Manyanda
        (viii) Bariadi Mashariki: Makondo Martine Kaunda
        (ix) Bariadi Magharibi: Chenge Andrew John
        (x) Maswa Mashariki: Bunyongoli Peter Edward
        (xi) Maswa Magharibi: Kisena Robert Simon
        (xii) Meatu:Salum Khamis Salum
        (xiii) Kisesa: Joelson Luhaga Mpina.

        Kwa orodha kamili ya wagombea wa CCM, tazama hapa na hapa.

        Friday, August 13, 2010

        FIKRA YA IJUMAA: KWA NINI ???????????

        • Kwa nini tulipigwa/tunapigwa/(tutapigwa) viboko kwa kuzungumza lugha zetu za mama, jambo ambalo kimsingi ni haki yetu ya kibinadamu? Kwa nini tuadhibiwe kwa kuzungumza lugha yetu ya taifa? Kwa nini tulazimishwe kuzungumza lugha tusiyoifahamu na ambayo hatukuandaliwa vizuri kuifahamu?  KWA NINI???

          Thursday, August 12, 2010

          HATUA ZA KUOMBA NAFASI ZA MASOMO UGHAIBUNI - NA ERNEST MAKULILO

          • Nimegombana na kukosana na watu wengi kutokana na hili suala la nafasi za masomo. Watu wengi wanafikiri kwamba kwa kuwa mtu uko huku Marekani au Ulaya basi ni rahisi kuwatafutia nafasi za udhamini, kazi na masomo. 
          • Ukiwaambia kwamba hii ni jamii ya uwazi na kila kitu kinafanyika kwa kufuata taratibu zilizopangwa hawaelewi na wanakuona kwamba una roho mbaya na hutaki kuwasaidia. 
          •  Ambacho hawakielewi ni kwamba hata kama ungekuwa mkuu wa chuo, usingeweza kumsaidia nduguyo ambaye hajatimiza masharti ya uombaji wa nafasi ya masomo. Kwa mfano, mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Florida, mkuu wa chuo cha udaktari alifukuzwa kazi baada ya kubainika kwamba alikuwa amemsaidia mwanafunzi mmoja kutoka familia ya kitajiri ambaye hakutimiza masharti sawasawa. Hapa hakuna cha shangazi wala mjomba na nafasi zote za udhamini na masomo zipo wazi mtandaoni. 
          • Hapa chini ni mahojiano ya mdau na mkereketwa wa masuala haya Ernest Makulilo aliyoyafanya na gazeti la Mwananchi la tarehe 10/8/2010. Ndugu Makulilo anagusia mambo ya msingi ambayo vijana wa Kitanzania wanaotafuta nafasi za masomo Ulaya na hasa Marekani inabidi wazingatie. Ukweli ni kwamba kuna nafasi nyingi za udhamini na masomo katika vyuo mbalimbali hapa Marekani. Blogu mbalimbali kama vile Makulilo, Wavuti, Naomba kazi na zinginezo zinajitahidi kuziweka wazi. Vijana wa Kitanzania amkeni kama wenzenu wa Kenya na kujaribu bila kuchoka kuomba nafasi hizi za udhamini. 
          ***********************
          ALIHANGAIKA kutafuta nafasi za masomo ya elimu ya juu, hatimaye akaja kuipata nafasi hiyo nchini Marekani. Baada ya kufanikiwa, Ernest Makulilo, Mtanzania anayeishi na kusoma nchini Marekani ameamua kuwasaidia wengine jinsi ya kuomba nafasi za masomo ya juu katika nchi za Ulaya na Marekani ikiwa ni mchango wake kama anavyoeleza katika mahojiano haya na mwandishi wetu.

          Swali: Sababu zipi zilikusukuma kuwasaidia wanaotafuta nafasi za masomo nje ya nchi?

          Jibu: Kwanza naomba niseme kuwa  nilianza kuitoa huduma hii rasmi Julai mwaka 2007, na huu ni mwaka wangu wa  tatu. Sababu kubwa ya kuingia katika huduma hii ni kwa kuwa nilihangaika sana kutafuta nafasi za masomo  hadi kufanikiwa kuja hapa Marekani. Hivyo nikawa na taarifa nyingi za mtu unawezaje kupata nafasi hizi kwa  Marekani na Ulaya.

          Sikuona kama ni jambo la busara  kwa kuwa mimi nimehangaika basi na wengine nao wahangaike, hivyo niliamua  kurahisisha njia ya watu wanaopenda kutaka kusoma zaidi kwa kupata udhamini ughaibuni.

          Kitu kingine kilichonisukuma kujikita katika suala hili ni kuwa na blog (gazeti tando) mahsusi kwa ajili ya kuweka taarifa za misaada ya masomo kwa watu wa nchi maskini.

          Niligundua kuwa blog nyingi zilizopo Tanzania zina vitu mchanganyiko, nikaonelea ni vema basi nianzishe kitu ambacho mtu akisema anataka nafasi za masomo basi ajue wapi pa kwenda na kupata msaada.

          Swali: Ukoje mwamko  wa Watanzania katika kupata taarifa za vyuo ambazo wewe umekuwa ukizitangaza?

          Jibu: Mwamko wa Watanzania ni mdogo sana tofauti na mataifa ya Afrika Magharibi, Amerika ya Kusini na Asia.  Watanzania wengi bado wana ile dhana na kasumba kuwa ili mtu aende Ulaya au Marekani kusoma ni lazima atoke katika familia tajiri au ya kisiasa. Hivyo wengi hukata tamaa mapema. Kitu kingine kinachosababisha mwitikio mdogo kutoka kwa Watanzania ni wengi wao kukosa ari   ya ushindani  kama ilivyo kwa Wakenya na watu wa nchi za Afrika Magharibi.

          Ukiachilia hayo, wengi hudhani upatikanaji wa nafasi hizi ni kitu rahisi mno. Ninapompa mtu taratibu za vitu gani ajiandae navyo ili aweze kuwa mshindani mkubwa na kufanikiwa kupata nafasi, wengi hukata tamaa. Baadhi ya Watanzania  tunapenda vitu mteremko sana wakati uhalisia si huo tena. Dunia hii ni ya ushindani, inabidi Watanzania tubadilike, tuendane na ushindani uliopo katika dunia ya  kibepari. Tuachane na fikra za kijamaa)

          Swali: Je wewe ni wakala wa vyuo  au unaiendesha vipi huduma hii?

          Jibu: Mimi si wakala wa chuo au taasisi yoyote ile. Na hakuna mtu, chuo au taasisi yoyote ile inayonilipa kwa huduma hii. Naiendesha huduma hii kwa imani kwamba kuna watu wana ndoto kubwa za maisha yao, lakini ndoto hizo mara nyingi hufa kutokana na ufinyu au ugumu wa upatikanaji wa elimu ya juu Tanzania na katika nchi nyingi zinazoendelea. Hivyo ninachokifanya ni kuhakikisha watu hawa wanatimiza ndoto zao za kielimu na maisha yao kijumla.

          Aidha nimekuwa nikizipitia  tovuti mbalimbali za vyuo na taasisi ambazo zinatoa udhamini wa elimu kwa watu wanaotoka nchi zinazoendelea. Nikishapata taarifa hizi, nazichuja kwa umakini na kuzihakiki kisha nazitangaza kwenye tovuti zangu ambazo ni   www.makulilo.blogspot.com pamoja na  www.scholarshipnetwork.ning.com. Kwa wale wenye maswali zaidi kuhusu taarifa fulani niliyoitangaza huniandikia barua pepe nami huwajibu kwa kutoa ufafanuzi husika.

          Swali: Nani hasa walengwa wa huduma zako na kwa nini?

          Jibu: Walengwa wakuu ni watu wenye nia na sifa ya kufanya shahada za Uzamili na Uzamivu, kwa Kiingereza Masters Degree na PhD. Kuna nafasi nyingi  za makundi haya mawili kuliko wale wanaotaka  kusoma shahada ya kwanza.

          Kwa digrii ya kwanza,  inakuwa ngumu kupata udhamini kwa kuwa sababu nchi  zote ambazo lugha mama si Kiingereza, hutumia lugha zao kama Kijerumani, Kifaransa na nyinginezo kufundishia  katika daraja hili.

          Hali hii huwa kikwazo kwa waombaji wengi kwa kuwa wanalazimika kujifunza lugha hizi na baada ya kufaulu mitihani ya lugha ndio upate nafasi. Nchi zinazotumia lugha zao za ndani ni kama Sweden, Denmark na  Ujerumani. Lakini kwa shahada ya pili na tatu, nchi hizi zimekuwa zikitumia pia Kiingereza

          Swali: Kwa hiyo unawaeleza nini Watanzania kuhusu hali hii?

          Jibu: Ninachowaambia  wasome shahada ya kwanza Tanzaniaa au katika  nchi nyingine za Afrika kisha shahada ya pili na tatu waende Ulaya, Marekani au nchi za mabara mengine.

          Swali: Kuna watu wengi wanaotumia njia hii ya mitandao kutafuta na kuomba  nafasi za masomo  bila mafanikio, nini sababu?

          Jibu: Kuna sababu nyingi zinazomfanya mtu akiomba asipate. Hili nitalifafanua kwa kirefu.Kwanza watu wafahamu kuwa kupata nafasi za masomo ughaibuni si jambo la bahati bali vigezo na kufuata taratibu husika. Kwa kukosa vigezo au kwa kushindwa kufuata masharti, wengi wamekuwa wakikimbilia kusema kuwa hawana bahati au kuna upendeleo.

          Kwa mfano ili mtu aweze kupata udahili na kisha udhamini, vitu vifuatavyo ni muhimu:Mosi, matokeo bora ya vyuo, vyuo vingi vinataka wastani wa daraja la pili la juu yaani Upper Sercond kwa Kiingereza.Pili, mwombaji aandike malengo yake kwa  umakini na ufasaha kupitia kitu kiitwacho Statement of Purpose/Interest. Ukiandika kwa kulipua hata kama una matokeo mazuri, sahau kupata udhamini.

          Tatu, kuna kitu kinaitwa  Writing Sample, hii ni kazi ambayo umeshawahi kuandika kama insha au utafiti wowote ule wakati unasoma. Lengo lake wanataka kujua uwezo wako wa kuandika mambo ya msingi. Nne,ni barua ya kukupendekeza kutoka kwa walimu wako au mahala unapofanyia kazi.Hawa nao wanapswa waiandike vizuri, waonyeshe uwezo wako wa taaluma na kazi.

          Pia kuna zoezi la kupima uwezo wa lugha kwa muombaji. Uingereza wana mitihani ya TOEFL na IELTS, wakati Marekani wana mitihani kama GRE na GMAT. Waombaji wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa uhalali na wakili au mahakama kama si nakala halisi.

          Baada ya hatua hii na ukishakuwa na vigezo, omba vyuo ila kumbuka vyuo unavyoomba viwe  vimeshatangaza udhamini wa masomo kwa wanafunzi  kutoka nje ya nchi husika. Lakini pia mwombaji asitosheke kuomba chuo kimoja. Anatakiwa kuomba vyuo zaidi ya ishirini ili kuwa na uhakika wa kupata udhamini mkubwa na ulio mzuri.

          Swali: Unanufaika vipi   kama mtu binafsi kwa kuendesha huduma hii?

          Jibu: Mafanikio makubwa ninayopata ni kuwa na furaha ya kweli kutoka moyoni. Ninafurahi sana watu wanapozipitia tovuti zangu,  kuzifanyia kazi na kisha kufanikiwa. Furaha hii ni zaidi ya pesa kwangu, maana mimi kujua mbinu hizi si kwa ujanja au werevu nilionao kwa wengine. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu kanipa maarifa haya, sina budi kuyafikisha kwa wengine wanaotafuta elimu au maisha.Moyo huu ndio ulionisukuma pia  kuanzisha mfuko wa kijamii utakaoitwa  Makulilo Foundation kwa lengo la kuongeza  wigo wa taarifa na mbinu zaidi za upatikanaji wa nafasi za masomo.

          MAMA, WHAT DO YOU LIKE AGAINST THE WALL?

          • Sijui huyu mama atajibu nini akipigwa swali kama hili na huyu binti yake. Watoto ni wadadisi sana na kila tunachokifanya wanakiiga kwani sisi (wazazi) ndiyo walimu wao wa kwanza. Tuwe waangalifu!

          KUNA ULAZIMA KWELI WA KUWEKA TANGAZO NAMNA HII?

          JIANDIKISHE HAPA

          Enter your email address:

          Delivered by FeedBurner

          BLOGU ZA BURUDANI NA UREMBO