NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 31, 2011

KUMBE MH. ROSTAM AZIZ NDIYE ATALIPWA MABILIONI YA DOWANS !?!?!??

Picha kutoka gazeti la The East African
 • Nimeisoma hii habari katika gazeti la The East African kwa mshangao na mshtuko kidogo kwani huko mbele Mheshimiwa Rostam Aziz aliwahi kukana kwamba hahusiki kwa namna yo yote ile na kampuni ya Dowans (na mzaziwe Richmond), na hata majina ya wamiliki wake yalipotajwa, jina lake halikuwemo. Kumbe ndiye anatakiwa kulipwa haya mabilioni ya walipa kodi na yeye ndiyo atayawasilisha huko kwa wenzake. Mungu Aibariki Tanzania !!!
Kutoka blogu ya Said Michael.

4 comments:

 1. Anasubiri nini kujiuzulu! huyu mtu kweli ni hatari kwa ustawi wa nchi na inaelekea anapigiwa kifua na viongozi wa juu wa nchi. Hivi kama Lowassa aliweza kujiuzulu huyu Rostam Aziz ni nani?

  ReplyDelete
 2. nilisoma gazeti la The East African tangu Jumamosi lakini hadi wakati huu bado nashindwa kuelewa nini dhamira yake kwa taifa hili ambalo tunaliita changa kutokana na uchanga unaosababishwa na watu wa namna hiyo.
  eeeeh Mungu Ibariki Tanzania na watu wake wenye mioyo safi!

  ReplyDelete
 3. Hapa tatizo si Rostam bali wakubwa walioko nyuma ya pazia wakimtumia. Yeye bila baraka za wakubwa, yeye ni nani hadi aiyumbishe nchi bila maslahi yao? Tunaweza kuwa tunamuandama dagaa ilhali tukiwapa mapapa kilio chetu tusijue lao moja! Jiulize ni kwanini wakubwa wameamua kukaa kimya? Kinachochekesha ni ile hali ya kuwa utapeli wa Richmond-Dowans hata kama unafanywa na watu wenye madaraka makubwa, umefanywa kitoto na kishamba. Inashangaza wakubwa hawa wasingekuwa wenye mzigo kuona utapeli rahisi kama huu kuiyumbisha serikali. Ila kwa vile wao ndio wao, hata utapeli wenye uwe wa kijuha vipi watalipa kwa vile wanajilipa.

  ReplyDelete
 4. Kazi ipo jamani!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU