NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, January 26, 2011

MTOTO UMLEAVYO......Hii niliiona kwa Dr. Phil. Wazazi kazi tunayo !

11 comments:

 1. Nilipofungua tu kukumbana na hii nikajikuta nakwepa na kuguna na mara nikapata na maumivu ya tumbo. Kwa kweli wazazi kaazi tunayo tena kuuubwwaaa tu. Mama we kumzamba mama/baba yako kofi....

  ReplyDelete
 2. Na malezi ya siku hizi ambapo watoto tunawalea kama wazungu. Muda si mrefu na sisi wataanza kutuzaba vibao kama huyu mama - na tutakuwa hatuna la kufanya.

  Wote mnaopiga makelele ya kuondolewa kwa viboko mashuleni MSHINDWE na MLEGEE kwa jina la Bwana!

  ReplyDelete
 3. Wow!! hii kali na inasikitisha sana. Kwa mtizamo wangu nadhani ni mambo ambayo yamekuwa yakiendelea katika hii familia kwa muda mrefu. Natumaini Dr. Phil aliweza kuisaidia familia hii.

  ReplyDelete
 4. Mkiyaonyesha hayo hapa bongo, haitachukua muda utasikia imetokea hivyo...mungu atuepeshilie mbali!

  ReplyDelete
 5. natamani namimi nikaitwange mialimu na milezi yangu iliyonichapaga viboko, TUMBAFu

  ReplyDelete
 6. Mtoto umlevyazo lazima alewe

  ReplyDelete
 7. Kimsingi katika malezi unapata kile ulichotoa. Ukipanda mbigiri usitegemee kuvuna sufi-itakuchoma tu. Hivi hapa mwenye kustahili lawama ni nani kati ya muadhibuji na muadhibiwa? Kama utaangalia hili tukio bila makengeza au ubinafsi, unagundua kuna mgogoro. Katika taaluma ya utatuzi wa migogoro hii tunaiita Quid pro quo. Ingawa inasikitisha, huo ndiyo ukweli na hali halisi yenyewe. Kuna haja ya kufanya mambo kwa kuanglia nini yatakuwa matokeo yake hasa wale tulioko huku kwenye nchi za magharibi. Kuna hatua fulani jamaa zetu wa kiarabu walioko huku na baadhi ya waswahili hufanya. Wakiona kitoto kinazidi unakirejesha nyumbani yaani Afrika, kinanyooshwa na kurejeshwa kikiwa kinajijua.
  Nakumbuka Ngugi wa Thiong'o. Siku moja watoto wake waliozaliwa na kulelewa Marekani walimshangaa alipowaambia kuwa alikuwa akitembea kilometa zaidi ya kumi kwenda shule. Walimuuliza. "Kwanini baba au mama yako alikuwa hakupeleki kwa gari? Jibu lake ilikuwa ni kuwapeleka kijijini kwake Kamilithu na kukaa kwa miaka miwili wakiishi maisha aliyoishi. Waliporejea US walikuwa na jibu.

  ReplyDelete
 8. Waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  Nakubaliana na Mr Mhango. Tatizo silo la mtoto ila nila wazazi na sheria zilizopo, japo sizijui vizuri sheria za Marekani zinazohusu watoto, hata hivyo sheria za nchi zilizoendelea kwa ujumla zinafanana. Tatizo katika nchi zilizoendelea, watoto wamepewa uhuru zaidi ya wazazi wao katika maswala ya malezi. Haishangazi kuona mtoto anamzaba kibao mama wakati mama harusiwi kisheria kufanya hivyo, na kama ikionekana anafanya hivyo, kuna hatari ya watu wa kitengo cha ustawi wa jamii kumwondelea mtoto wake,kosa wanasema ''child abuse''. Kutokana na hizi sheria wazazi wanakuwa hawana sauti katika malezi ya watoto wao. Kwa upande mmoja, nakubaliana na hizi sheria kwa sababu, nchi nyingi zilizoendelea zimejaa wazazi wasafihi, lakini kwa upande mwingine, sheria hizi zimeingiza hata wazazi ambao nia kuu ni kuwafundisha na kuwajengea mazingira mazuri ya baadaye watoto wao ili wajue maana ya ubinadamu halisia. Kutokana na hizi sheria, malezi ya watoto yanazidi kuporomoka kizazi na kizazi, inafikia hatua mtoto akisha kuwa mtu mzima anakuwa hajui lipi baya na zuri katika jamii ya kibidamu harisia.
  Nguyu yangu Mhango, hata huyo Ngugi wa thiong'o alikuwa na bahati kuwa watoto wake walikubaliana naye wakaishi kijijini kwa miaka miwili. Ninazijua kesi ambazo wazazi wamejalibu kuwapeleka watoto wao nyumbani(Afrika) na watoto wakalalamika na ubalozi wa nchi yao ukachukua jukumu la kukawarudisha nchini mwao.
  Hii ndio athari ya maendeleo, ambayo Tanzania ya leo viongozi wake wako mbioni kuanzisha sheria hizi kutokana na neno''Pressure from western donorS''. Tanzania ya leo ni kama dodoki.
  Ukishangaa ya Musa, utaona ya firauni.

  ReplyDelete
 9. Itabidi tuanze kufuatilia parent abuse inayofanywa na watoto kama huyu. Matondo unasemaje kuhusu hili?
  Ng'wanamapalala nashukuru kwa mchango wako.

  ReplyDelete
 10. Kweli kazi ipo lakini huwezi kujua mara nnyingine huenda alikuwa anaulizia baba mzazi. Maana na sisi akina mama wengine sina hata la kusema

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU